Sisi tunapata "the worst of both worlds".
Yani kwenye kufuata Ujamaa hatupo kamili, tunapata mabaya ya kufuata Ujamaa, bila kupata mazuri ya kufuata Ujamaa.
Ndipo hapo unakuta mambo ya low investment, kuogopa "maadui wa nje", bila subsidized healthcare, education etc
Kwenye Ubepari nako hatupo kamili, tunapata mabaya ya Ubepari bila kupata mazuri ya ubepari.
Ndipo hapo unakuta watu wameuziana nyumba za umma, wameuziana viwanda, wamepiga hela EPA bila kuzuiwa na mazuri ya ubepari kama free press, labor unions, strong opposition, open market etc.
Tunapigwa kutoka pande zote.
Kama nchi, tutapata hasara za kutokuwa na uraia pacha kwa kukosa connections za maana na investment, bila kupata faida za kuwa na uraia mmoja tu ambazo ni za mazingaombwe zaidi.
Wewe nchi mpaka utawala wa Kikwete Ikulu ilikuwa inatumia email ya Yahoo, hapo unahitaji raia wa kigeni aingie nchini kuku compromise?
Kila siku tunasikia watu wanafanya mambo mitandaoni, bado watu wanashikilia uraia kuwa ndiyo kitu kitakachowahakikishia usalama?