Mjadala wa kitaifa: Tuziainishe faida na hasara za uraia-pacha (dual citizenship) kwa Tanzania yetu

Mjadala wa kitaifa: Tuziainishe faida na hasara za uraia-pacha (dual citizenship) kwa Tanzania yetu

What a load of trollop. Raia ni raia, iweje tena kuwe na mipaka? Inapofika vita vya Nduli Iddi Amin, mathalani, tukitakuwa kuchangia damu, si anaweza kusema kuwa mue sina ardhi? Kama huko atokako ana ardhi, atawapenda zaidi? Sikubta Olympic atachezea njinipu? Kwa nini inapojiri asiibe ndege zetu na makanikia yetu kama kina tundulissu na fatmakarume kuwatetea mabeberu KKY (kama kwaida yao)? Tumefunga Serengeti kupitia Bologonja au Mlina Kilimsnharo kutojea Tsavo, kama yeye ni raia kwa nini asipite na watalii wake? Imagine if a man and his wife have dual marriages, I mean, married in each dual country, itakuwaje?
Ushamba wako ndiyo unakuongoza. Jaribu kusafiri au hata kufanya reserch nchi nyingine uone mambo yalivyo.
 
Mimi nilikuwa na kazi yangu nzuri tu nafanya, hao recruiters wakawa wananitaka, kwa hiyo niliendelea tu na kazi yangu.

Ila ningefanya pale hata miaka miwili tu baada ya hapo ningekuwa hot cake sana, ukiwa katika industry huku na uzoefu wa kufanya kazi Benki Kuu unakuwa hot cake.

Hilo jambo ni moja ya mambo yaliyonifanya niachane na kusubiri habari za uraia pacha niendelee na maisha yangu kivyangu na kuchukua uraia huku niliko.

Maana unaweza kujifanya mzalendo halafu opportunities zinakupita, na huo uzalendo wako haukusaidii wewe wala nchi yako.

Kuna kazi nyingine nyeti unahitaji kuwa na "security clearance" kuzifanya. Na kuna level fulani ya "security clearance" huwezi kuzipata ukiwa si raia.

Nikasema kitovu changu kipo tu Bandari ya Salama, Misheni Kota kwetu, Mwanza kwetu, hata kama nachukua makaratasi ya ughaibuni.
Biden yupo better kumlinganisha na Trump?.

Naongelea kukubalika kwake na ile overall efficiency.
 
Ujamaa ni msingi wa haya maamuzi ya kukataa uraia pacha. Bado kuna zile mentalities za Nyerere kwamba adui mbaya hayupo kati yetu bali ni yule anayetokea nje.

Wizi mkubwa mkubwa kama ule wa EPA, ESCROW wahusika ni watanzania wenye kuishi humu humu nchini waliolelewa wakiambiwa mzalendo ni wa ndani na wa nje ni adui.

Tutakuja kubadilika kwani kuna ongezeko kubwa la watanzania wa diaspora na ndipo tutakapogundua ukubwa wa fursa tulizozipoteza kwa miaka mingi.
Mnadiss ujamaa as if ni mfumo mbovu kwa 100%.

Mna akili za kipumbavu sana. Na hii ni kwasababu hamjawahi kuuishi ubepari 100%.

Msichokijua hata huko kwa mabepari bado kuna practice kadhaa za kijamaa.
 
Mnadiss ujamaa as if ni mfumo mbovu kwa 100%.

Mna akili za kipumbavu sana. Na hii ni kwasababu hamjawahi kuuishi ubepari 100%.

Msichokijua hata huko kwa mabepari bado kuna practice kadhaa za kijamaa.
Pole kwa kukukwaza. Lakini ndio ukweli wenyewe, hatujaipokea dunia pana kwa kigezo cha usisi wetu kuwa shakani kama tukijichanganya.

Ubepari ni unyama kwa mujibu wa malezi yetu ya kisiasa lakini dunia hubadilika na sisi tunapaswa kuondokana na hiyo mitazamo ya kilofa.
 
Tatizo la hii nchi ni ushamba na kutojiamini. Wengi wanaamini mtu akiwa na uraia pacha basi ataihujumu TZ na kuipa faida nchi nyingine, tunaacha kujiuliza kwanini mtu huyo huyo asihujumu nchi nyingine na kuleta maendelea bongo. Hatuamini uwezo wa watu wetu kushindana kwenye soko la kimataifa? Kama hatuwaamini ina maana tunatengeneza watu incompetent huku tukijua fika ni incompetent.

Tukienda ki-namba, mchango wa diaspora kwenye pato la taifa yani remittances za nchi kama Kenya na nchi zingine limeongezeka maradufu baada ya kuruhusu uraia pacha. Katika hizo nchi remittances zinachangia a substantial amount kwenye pato la taifa sababu watu wanawekeza heavily kwao huku wakiwa na imani na mali zao kwamba hawatazipoteza kwa sababu ya kigezo cha uraia.

Ukija bongo mtu unawaza kuwekeza nyumbani mara tu ukichukua uraia wa nchi nyingine. Aidha uanze kuandika majina ya ndugu kwenye mali zako au usitishe kabisa kuwekeza nyumbani kitu ambacho hakisaidii nchi kwa ujumla.

Kingine ni kasumba ambayo wabongo wamemezeshwa miaka nenda rudi kwamba nchi yao tu ndo ina mali na wengine wote wanawaonea wivu. Wanaamini wakiruhusu uraia pacha wageni watakuja kutumia mali asili zao kwa faida yao. Mali asili zipo kwa faida ya wote duniani so long as sheria na taratibu zinafuatwa. Leo hii nchi zenye less natural resources na dual citizenship zinaingiza pesa nyingi na zipo mbali kuliko sisi tunaozikumbatia maliasili kama viazi.

Nchi isiyo ruhusu uraia pacha, isiyo na viwanda vyenye kuzalisha ajira za kutosha, yenye mifumo kandamizi yakufanya malipo online is doomed to fail katika ulimwengu wa leo.
Mpaka sasa bila bila. Hakuna mTanzania awaye yote ambaye ana uraia anazuiwa kuwekeza nyumbani. Ukiwa na uraia wa nchi nyingine, ili mradi una damu ya kiTanzania unawekeza bila wasi wasi wowote. Hiyo kusema huwezi kuwekeza ni kujengeana na kueneza hisia za hofu.
 
Biden yupo better kumlinganisha na Trump?.

Naongelea kukubalika kwake na ile overall efficiency.
biden-v-trump-approval-2-1024x654.png

 
Mpaka sasa bila bila. Hakuna mTanzania awaye yote ambaye ana uraia anazuiwa kuwekeza nyumbani. Ukiwa na uraia wa nchi nyingine, ili mradi una damu ya kiTanzania unawekeza bila wasi wasi wowote. Hiyo kusema huwezi kuwekeza ni kujengeana na kueneza hisia za hofu.
Mkubwa watu hawataki ku risk investment yao kwa huruma au mazoea. Wanachohitaji ni uhakika wa Kisheria ama kwa dual citizenship au residence permit yenye hadhi ya kufanya investment bila bugudha.
 
Kwa muda mrefu sasa kumekuwepo na mijadala kuhusu Tanzania kuruhusu uraia pacha. Wapo wanaopendekeza Tanzania kama nchi ikubali uwepo wa uraia pacha ili kuzipata faida zitokanazo na uraia wa aina hiyo. Wapo wenye mtazamo kuwa muda wa Tanzania kuwa na uraia pacha bado haujafika. Hivyo basi, wanauunga mkono msimamo wa Serikali wa kutokubali na kuanzisha uraia pacha hapa nchini.

Uraia ni jambo la kisheria. Endapo Serikali itaridhia kuanzishwa kwa uraia pacha, lazima sheria inayosimamia masuala ya uraia ifanyiwe marekebisho kukidhi matakwa ya mabadiliko hayo. Ilivyo sasa, uraia unaokubalika hapa nchini ni uraia wa nchi moja: kama ni raia wa Tanzania au la. Raia wa Tanzania, ilivyo sasa, haruhusiwi kuwa raia wa nchi nyingine yeyote duniani. Ikitokea hivyo, raia husika itampasa kupoteza uraia mmojawapo: ima wa Tanzania au wa hiyo nchi nyingine.

Kwa kuwa mimi si mbobezi wa masuala ya kimataifa na kiuraia na naamini JF ni nyumba ya wabobezi wa mambo hayo na mengine, naomba kuwasilisha hoja na wito kwa waungwana kuziainisha faida na hasara za kuwa na uraia pacha hapa nchini kwetu Tanzania. Kujua faida na hasara kutachochea au kupooza wito wa wananchi wa kutaka uwepo wa uraia pacha kwa watanzania.

Karibuni waungwana wa JF...

Mie nafikiri wasomi wetu wanasheria ndo wanatuangusha kusema uraia pacha hauruhusiwi Tanzania, kitu kinachopelekea hata police wetu kuanza kuandama watu ndivyo sivyo.

Uraia pacha Tanzania naamini unaruhusiwa ktk katiba hii hii ila tu haijapata mtu wakuitaka mahakama ielezee kwa undani zaidi. Nitachukua snap chache hapa kuonesha hilo.
Kinachotakiwa ni watanzania kurudishiwa haki yao, ambayo imebainishwa ktk katiba, ila watu ama ni ignorant ama kwasababu zao wanakomalia katiba hairuhusu. Wasomi wa sheria naomba mnitafsrie vifungu vya katiba hivi hasa ninapotilia mkazo.

Hii ya kwanza naelewa mimi kama mleyi kwamba mtu aliyeoa na akapata uraia wa huko anaruhusiwa kuendelea na uraia wa Tanzania-dual.
1623181767375.png


Na hapa chini pia
1623182164033.png
 
ili mradi una damu ya kiTanzania unawekeza bila wasi wasi wowote.

Unawekeza kama mwekezaji toka nje au kama mzawa wa TZ na mwenye haki zote kama raia wa TZ bila vibali vya foreign investor?
 
Write your reply...mimi siamini kabisa kama kuna diaspora mwenye uwezo wa kufanya uwekezaji wa maana.... wanalilia uraia pacha ili maisha yakiwashinda huko nje , warudishe majeshi nyumbani kama le mutuz... miaka 20 us karudi na dola 500 mgpgmqgrg
 
Unawekeza kama mwekezaji toka nje au kama mzawa wa TZ na mwenye haki zote kama raia wa TZ bila vibali vya foreign investor?

Hizo ni formalities tu. Wakiona jina la directors kama Sanga, Mwakighonjola, Mutahabwa, Kweka etc wala hawaendelei kukuuliza zaidi. Ni permits & rights unapaTa tu
 
Write your reply...mimi siamini kabisa kama kuna diaspora mwenye uwezo wa kufanya uwekezaji wa maana.... wanalilia uraia pacha ili maisha yakiwashinda huko nje , warudishe majeshi nyumbani kama le mutuz... miaka 20 us karudi na dola 500 mgpgmqgrg
Sasa ndugu yangu, wewe tatizo lako ni dharau kwa Diaspora(kama kufanya ligi vile),Vs wale waliobaki Tz.. kwamba uwezo wa 'diaspora' kuwekeza ni sifuri, au ni chuki yako tu kwa sababu watz hao wanaishi nje ya Tanzania..... Kaazi kwelikweli.....
 
Mkubwa watu hawataki ku risk investment yao kwa huruma au mazoea. Wanachohitaji ni uhakika wa Kisheria ama kwa dual citizenship au residence permit yenye hadhi ya kufanya investment bila bugudha.
Kibaya zaidi kila rais anakuja na approach tofauti kuhusiana na suala hili la watanzania wa diaspora kuwekeza kwao.

Kunakuwa na ile hali ya diaspora kusimangwa na kutazamwa kwa chuki kama vile wanaombewa kwa Mungu wanachotaka kukifanya TZ kishindwe kabla hata hakijaanzishwa.
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Hizo ni formalities tu. Wakiona jina la directors kama Sanga, Mwakighonjola, Mutahabwa, Kweka etc wala hawaendelei kukuuliza zaidi. Ni permits & rights unapaTa tu

Kumbe Unaongelea hisani na mazoea.

Mtu anayetaka kuwekeza kiasi cha kutosha hawezi kurisk kufanya biashara kwa kutegemea kudra na uzembe wa wabongo. Moreover, unajiumiza zaidi wewe mwenyewe kwa kufanya mambo kinyemela. Huwezi kufika mbali.

Fuatilia michango ya diaspora Kenya kabla na baada ya kuruhusu uraia pacha uone exponential increase of remittances. Leo hii banks za Kenya zinazunguka dunia nzima kuwaomba diaspora wawekeze KE na wao wanafanya hivyo sababu hakuna tena vikwazo.
 
Sisi tunapata "the worst of both worlds".

Yani kwenye kufuata Ujamaa hatupo kamili, tunapata mabaya ya kufuata Ujamaa, bila kupata mazuri ya kufuata Ujamaa.

Ndipo hapo unakuta mambo ya low investment, kuogopa "maadui wa nje", bila subsidized healthcare, education etc

Kwenye Ubepari nako hatupo kamili, tunapata mabaya ya Ubepari bila kupata mazuri ya ubepari.

Ndipo hapo unakuta watu wameuziana nyumba za umma, wameuziana viwanda, wamepiga hela EPA bila kuzuiwa na mazuri ya ubepari kama free press, labor unions, strong opposition, open market etc.

Tunapigwa kutoka pande zote.

Kama nchi, tutapata hasara za kutokuwa na uraia pacha kwa kukosa connections za maana na investment, bila kupata faida za kuwa na uraia mmoja tu ambazo ni za mazingaombwe zaidi.

Wewe nchi mpaka utawala wa Kikwete Ikulu ilikuwa inatumia email ya Yahoo, hapo unahitaji raia wa kigeni aingie nchini kuku compromise?

Kila siku tunasikia watu wanafanya mambo mitandaoni, bado watu wanashikilia uraia kuwa ndiyo kitu kitakachowahakikishia usalama?
"A very carefully curated mentality that keeps the masses blind, loyal, and bound for the benefit of the few"

Ukisoma Animal Farm utagundua mengi sana.
 
Kiukweli hata mie naona faida ni nyingi kuliko hasara kwa TZ. Kwa mfano ili uweze kuekeza au kumiliki ardhi TZ ni lazima uwe raia. Sasa fikiria diaspora wote wa TZ wataweza vipi kuekeza ? Au akija anakuja kama mtalii au inabidi afanye pirika ili aweze kukaa TZ, maana sio raia.

Nadhani wanasiasa wametizama maslahi yao binafsi na kuwatia watu khofu kama waarabu/mabeberu watarudi kuja kutawala 🤷‍♂️ Pure non-sense.
 
Back
Top Bottom