Mjadala wa kwanza wenye dini za Abraham (Ukristo na Islam) dhidi ya wasio nazo na wenye mashaka ulifana sana

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
64,960
Reaction score
111,265
Huu umekuwa mjadala wa kwanza Tanzania wa dini za Abraham(Abrahamic religions), Ukristo na Uislamu kwa pamoja wakipewa changamoto na waamini dini za asili na wenye mashaka kabisa ya mungu wa Abraham (agnostic).

Chionda na mwenzake anaitwa Semvua waliupiga mwingi sana mpaka waamini mungu wakabaki wamepoteana na wengine wanahuburi tu.

Kijana mmoja muamini mungu alionekana ana uelewa wa big bang, historia kwa upana na theology ya dini yake vizuri na alikuwa anaweza sana wa kujenga hoja huku jasho lilimtoka.

Mchungaji na kijana mwingine muamini walibaki wanahuburi tu kama wako kanisani. Ustadh/Sheikh aliyekuwepo yeye alikuwa kama mtoto wa shule ya msingi ameingizwa kwenye darasa la Calculus la chuo kikuo, alibaki anasema Subhanahu wa taala tu na porojo za hapa na pale muda mwingi akiwa kimya kusikiliza.

Pongezi nyingi kwa Denzo production kuandaa mjadala.

Ingieni YouTube muangalie wenye dini walivyotokwa jasho wakimpambania mungu wao.

Screenshot_20261025-205651~2.jpg
 
Unajua kwenye hiyo mijadala ni rahisi mtu anaeamini dini kutolewa kwenye reli kwasababu ya kuogopa kukufuru au kukosea juu ya iman yako

Yaani unavyodhid kutetea ndiyo unaona ubongo wako unatoka nje ya mstari
 
Huo haukuwa mjadala sadifu
Ulipangwa kinyemela kwa kuita watu wenye upeo mdogo wa dini na sayansi
Ni ujinga
Hao ma atheist wa mchongo mimi ningewakalisha chini na higgs bosson na ghost particle ya Neutrino wajieleze Dark matter na Dark energy ni nini?
 
Dini za Abraham?
Kwamba kabla ya abraham hakukuwa na dini si ndio?
 
Huenda anamaanisha Judaism iliyozaa ukristo na uislamu.
Ataelewa wapi huyo kilaza,
Mtu ambaye hajui hata Abrahamic religions ni zipi au inamaanisha nini ni wa kumpuuza tu.
 
Imekaririshwa vitu ambavyo havipo kijana

Nimekuuliza uitaje hiyo dini moja iliyozaa nyingine mbili

Tafadhal husipanic
 
Huu umekuwa mjadala wa kwanza Tanzania wa dini za Abraham(Abrahamic religions), Ukristo na Uislamu kwa pamoja wakipewa changamoto na waamini dini za asili na wenye mashaka kabisa ya mungu wa Abraham (agnostic).

Chionda na mwenzake anaitwa Semvua waliupiga mwingi sana mpaka waamini mungu wakabaki wamepoteana na wengine wanahuburi tu.

Kijana mmoja muamini mungu alionekana ana uelewa wa big bang, historia kwa upana na theology ya dini yake vizuri na alikuwa anaweza sana wa kujenga hoja huku jasho lilimtoka.

Mchungaji na kijana mwingine muamini walibaki wanahuburi tu kama wako kanisani. Ustadh/Sheikh aliyekuwepo yeye alikuwa kama mtoto wa shule ya msingi ameingizwa kwenye darasa la Calculus la chuo kikuo, alibaki anasema Subhanahu wa taala tu na porojo za hapa na pale muda mwingi akiwa kimya kusikiliza.

Pongezi nyingi kwa Denzo production kuandaa mjadala.

Ingieni YouTube muangalie wenye dini walivyotokwa jasho wakimpambania mungu wao.

View attachment 3699235
mi ningewaalisha chini mapema
 
Ngoja nikautazame huo, mjadala.
Asante kwa taarifa
 
Back
Top Bottom