Huu umekuwa mjadala wa kwanza Tanzania wa dini za Abraham(Abrahamic religions), Ukristo na Uislamu kwa pamoja wakipewa changamoto na waamini dini za asili na wenye mashaka kabisa ya mungu wa Abraham (agnostic).
Chionda na mwenzake anaitwa Semvua waliupiga mwingi sana mpaka waamini mungu wakabaki wamepoteana na wengine wanahuburi tu.
Kijana mmoja muamini mungu alionekana ana uelewa wa big bang, historia kwa upana na theology ya dini yake vizuri na alikuwa anaweza sana wa kujenga hoja huku jasho lilimtoka.
Mchungaji na kijana mwingine muamini walibaki wanahuburi tu kama wako kanisani. Ustadh/Sheikh aliyekuwepo yeye alikuwa kama mtoto wa shule ya msingi ameingizwa kwenye darasa la Calculus la chuo kikuo, alibaki anasema Subhanahu wa taala tu na porojo za hapa na pale muda mwingi akiwa kimya kusikiliza.
Pongezi nyingi kwa Denzo production kuandaa mjadala.
Ingieni YouTube muangalie wenye dini walivyotokwa jasho wakimpambania mungu wao.
View attachment 3699235