TUSHIRIKISHANE Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Bukoba Mjini

TUSHIRIKISHANE Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Bukoba Mjini

Mwonekano wa Stand Kuu ya Mabasi Tarehe 9 March, 2017.

9bc10d6cc78601be95aa2ff17d107a72.jpg
92650aee2e68dcc3adae807498d93adf.jpg
2edeccdb627a20024a50244db49463e5.jpg
Dada siku hizi unapotea sana. Nilitembelea bukobanyumbani.com nikaona mahojiano uliyoyafanya na mfanyabiashara mmoja hivi. Huyu bwana alikwambia yeye ni Chadema lakini hawaamini si viongozi wala mbunge wake, kumbuka naye ni Chadema pia. Ulivyomuuliza akakwambia aliwatusi wafanyabiashara na waendesha boda boda.

Any way, mbunge wetu aliyetakiwa kuaminika na kuwa upande mmoja na wapiga kura wake ndo anayesemwa hivyo na ndivyo anavyotafsiriwa. Mbunge wetu haongeleki vizuri sana si tu kwa walio kambi ya jirani, hata kwa wa kambi yake pia. Mbunge wetu.
 
Dada siku hizi unapotea sana. Nilitembelea bukobanyumbani.com nikaona mahojiano uliyoyafanya na mfanyabiashara mmoja hivi. Huyu bwana alikwambia yeye ni Chadema lakini hawaamini si viongozi wala mbunge wake, kumbuka naye ni Chadema pia. Ulivyomuuliza akakwambia aliwatusi wafanyabiashara na waendesha boda boda.

Any way, mbunge wetu aliyetakiwa kuaminika na kuwa upande mmoja na wapiga kura wake ndo anayesemwa hivyo na ndivyo anavyotafsiriwa. Mbunge wetu haongeleki vizuri sana si tu kwa walio kambi ya jirani, hata kwa wa kambi yake pia. Mbunge wetu.
Mbona bukobanyumbani haipo hiyo tovuti?
 
MWONEKANO WA MJINI WA BUKOBA MWEZI FEBRUARY

69514a96224f1b7c6156448d20e0187b.jpg
b0db4f7bc7603eb4feae2331c4368276.jpg
218e182b694ef3b6c45838a55792ea3e.jpg
5346d327abd9c7ad7b1a27fbc1b73020.jpg
b25b36f29bbc8fecb0fd94447fbe572d.jpg
Hapa mbona huwapongezi Meya na Mbunge?

Kiufupi Bukoba inaharibiwa na Halmashauri....suala la elimu limetokea by coincidence tu kutokana na mipango uliyokuwepo muda mrefu toka enzi za Kagasheki.

Uongozi wa sasa wa Halmashauri bado haujafanya jambo likaonekana. Tunategemea waboreshe miundombinu..
 
Halafu hivi ukiuliza hii manispaa kweli ina uongozi? Unafanya kazi gani, hivi mbunge hata hivi vidogo tu vimemshinda? Stand imekwama, soko nalo hamna kitu, hata barabara za mjini tu nazo zimemshinda kweli?
Viongozi wa hapo Halmashauri/Manispaa kazi yao ni kupiga pesa tu maana wanajua hawarudi 2020. Si Mbunge wala Meya Kalumuna...kwahio wanajijenga tu. Bukoba mmepigwa hasara ya miaka 05.

Mlimnyima Kagasheki kura eti mnamkomoa mmemchoka...mkampa Lwakatare eti 'katumue nawe alye'. Wanabukoba perception yao towards development ndio hiyo...wanaamini viongozi wakipewa madaraka ni 'kula' na sio kuwatumikia.

Wakina Lwakatare wanalifaham hilo ndio maana wana amass wealth wakijua wanabukoba hawaeleweki...na bahati mbaya kama kiongozi usipo amass wealth ktk uongozi wako hawakuelewi wanakunyooshea vidole 'kileebe kifeela tikiinakantu okyo kikaba kili kibunge...enaku zimuteile'
 
Viongozi wa hapo Halmashauri/Manispaa kazi yao ni kupiga pesa tu maana wanajua hawarudi 2020. Si Mbunge wala Meya Kalumuna...kwahio wanajijenga tu. Bukoba mmepigwa hasara ya miaka 05.

Mlimnyima Kagasheki kura eti mnamkomoa mmemchoka...mkampa Lwakatare eti 'katumue nawe alye'. Wanabukoba perception yao towards development ndio hiyo...wanaamini viongozi wakipewa madaraka ni 'kula' na sio kuwatumikia.

Wakina Lwakatare wanalifaham hilo ndio maana wana amass wealth wakijua wanabukoba hawaeleweki...na bahati mbaya kama kiongozi usipo amass wealth ktk uongozi wako hawakuelewi wanakunyooshea vidole 'kileebe kifeela tikiinakantu okyo kikaba kili kibunge...enaku zimuteile'
Waliingia choo cha kike wakakutana na usanii wa kuzungusha mikono. Wazee wa "mabadiriko" na sasa sijuhi hapo Bukoba kama kuna hata vidariri vya hayo "mabadiriko' waliyoyakimbilia pasipo kujua.

Lwaka ni bonge la msanii
 
Mbona bukobanyumbani haipo hiyo tovuti?
Samahani niliipata kupitia you tube subscribe, Bukoba: maoni ya wananchi juu ya ahadi za mbunge wao. Utampata huyo jamaa akiwa amesimama dukani kwake
 
Wahamiaji haramu wanarudisha nyuma maendeleo ya mkoa wetu.
Tena hawana shida sana mkuu, angalia wanachokifanya Kg na Tabr. Kila siku wanaingia na siraha, wanaiba na kuua hata mchana kweupe tena mijini. Kagera tunao ila kwa mijini ni mazingira mazuri sana ya kufanya biashara na wizi wizi hakuna.
 
MAFANIKIO YALIYOFIKIWA KATIKA KIPAUMBELE CHA MIKOPO KWA WANAWAKE NA VIJANA

MATEGEMEO SACCOS (VIJANA)

1. Mpaka sasa vimekopeshwa vikundi 19 na vi3 vinasubili.

2. Marejesho yako vizuri kutokana na mikataba yao kuwa na mkazo mkubwa na faini kwa wazembe.

3. Pesa hiyo inakopeshwa kwa kipindi kisichozidi miezi sita unatakiwa kuwa umemaliza marejesho na riba ni 5% tu.

4. Changamoto ni kwamba pesa haipo ya kutosha kiasi kwamba wanachoomba vikundi hawapati kiasi sahihi kwa vile wanalazimika kuzigawagawa ili kuwapatia wote.

5. Mwezi January ndiyo mara ya mwisho *MATEGEMEO SACCOS* kupokea pesa za manispaa ili hali ilisemekana zitakuwa zikipelekwa kila mwezi.

6. Mwisho wameomba tuzidi kuhamasisha umma hasa vijana wafuate utaratibu wa vikundi ili wakapate mkopo uwasaidie kujikwamua.

WANAWAKE TUINUANE SACCOS.

Vikundi vilivyokwisha nufaika na mikopo ni 11 na vinavyotarajiwa kukopeshwa mwezi huu ni vi 3.

Pesa zilizokwishaelekezwa na manispaa kwa saccos hii ni jumla ya Tshs. 40,227,000/=.

Mara ya mwisho kupokea fedha za halmashauri ni tarehe 03/03/2017 ambapo wamepokea kiasi cha fedha Tshs. 6,172,657.50/=

Marejesho si haba na si ya usumbufu sana kwa sababu vikundi vilihakikiwa vizuri kabla ya kupewa mikopo hivyo ufuatiliaji ni mwepesi.

CHANGAMOTO.

1. Vikundi vingi vilivyosajiliwa na manispaa ni vikundi hewa, hivyo yalikuwepo mazoea ya kuchukua mikopo ya halmashauri kirahisi na kuitafuna na kupotea, kwa sasa kikundi kinahakikiwa vilivyo hivyo kuondoa mianya ya wapiga dili.

2. Siasa zinaingilia ufanisi wa shughuri nzima ya utoaji mikopo, wanasiasa katika maeneo yao wanawasukuma wananchi wakaombe mikopo hata kama hawana sifa na vigezo vya kukopeshwa wanasiasa wanataka kusimamia makundi hayo yapewe pesa kwa masrahi yao ya kisiasa hata kama vikundi hivyo havikidhi vigezo.

3. Taarifa zinazotolewa na manispaa kwa umma kuhusu mikopo ni za kimalengo lakini ni tofauti na uhalisia, pesa hazipelekwi kwa wakati na hata cheki zinapokuwa zimesainiwa kunakuwa na uzungushwaji mpaka kuipata, wakati huo wananchi hawayajui wao wanachotaka ni pesa na wanakuwa wameshaelezwa kuwa pesa inapelekwa kila mwezi jambo ambalo sio kweli.

4. Riba iliyopangwa na manispaa ni ndogo ukilinganisha na garama ya uendeshaji wa huduma kwa vikundi.

5. Vikundi vinakuwa na wanachama wengi na pesa inayokuwepo inakuwa kidogo kiasi kwamba haziwatoshi, mf. kikundi cha watu 20 unawapa mil 2 au 3 zinakuwa kidogo sana na vikundi vinakuwa ni vingi na vyote vinahitaji. Na kingine ni kwamba pesa hazipelekwi kila mwezi.

6. Kwa sababu za msingi bila shaka, manispaa imezitaka saccos hizi ziwasilishe majina ya vikundi vilivyoomba mikopo ili yajadiliwe kwenye kamati ndogo ya mikopo ya manispaa na kupitishwa kupata mikopo, saccos kwa mjibu wa sheria za ki ushirika wana miongozo yao namna ya kuvijua vikundi, sifa na vigezo na zinaouwezo wa kwenda mpaka maeneo ya waombaji ili kujiridhisha kabla ya kukopesha, hivyo hawaoni sababu ya vikundi hivyo kupitiwa na kujadiliwa tena jambo ambalo linaweza kuua ufanisi wa huduma kwa sababu kamati inaweza kupendekeza kinyume. Majadiliano juu ya jambo hili bado yanaendelea ili kupata muafaka.

MAONI

1. Saccos hizi kama zilivyoaminiwa na kupewa mikataba basi ziachwe huru kutekeleza huduma kwa wananchi kwa kuzingatia vigezo na masharti, kuingiliwa na wanasiasa kwa kutaka vikundi flani vipewe kipaumbele hata kama havikidhi vigezo kutaua ufanisi wa huduma.

2. Halmashauri kuingilia utaratibu wa saccos katika kuvipitisha vikundi kupata mikopo kunaweza kuleta mwanya wa kuchomeka vikundi hewa hivyo kusababisha upotevu wa pesa za serikali jambo litakalosababisha wadhamini wa saccos kupoteza mali/dhamana zao ili kufidia pesa zilizopotea.

3. Uhamasishaji na uelimishaji kwa wananchi kuunda vikundi halali uendelee ili kuchukua nafasi ya vikundi hewa lukuki vilivyosajiliwa manispaa ili umma mkubwa unufaike na mikopo hiyo.

4. Pesa zielekezwe kwa wakati kwenye saccos ili kukidhi uhitaji wa vikundi.

5. Riba ya 10% isitafsiriwe kwa kigezo cha muda, kama ulivyo mkataba baina ya halmashauri na saccos ni kwamba riba itakuwa 10% kwa mwaka na kama ni miezi 6 itagawanyika kwa mbili na kuwa 5% na kama ni miezi 3 itakuwa 2.5%. Saccos inaomba 10% iwe uniform bila kujali muda.

Imeandaliwa na Katibu wa Mbunge

Alex Xavery
 
BARABARA MPYA YA MTAA WA KILIMAHEWA - KASHAI

Hii ni barabara mpya iliyojengwa na wananchi wa mtaa kilimahewa na kusadiwa mhe Lwakatare awamu ya kwanza 0.7km tayari imekamilika
d0d94ef0d8bd0c52548437065192be20.jpg
85c53c29e783a9a343b409ef69193c1c.jpg

34d5323310fc16da048268db058504fd.jpg
84dff8ac896e47b22e47f86be283c891.jpg
17f31b4f663e7f72234cbdc789b829af.jpg


Awamu ya pili ni kuondoa nyumba iliyukutwa katikati ya barabara na hivyo kuwa kigingi katika mwendelezo wa ujenzi wa barabara hii
87ede44ea4a6534409d1cb29e143fd1d.jpg

7bb37be8fcf3e78b72375f41a71b45c1.jpg
2b2dc5fcc47f0f73b9e76b4b33fb78d4.jpg
e982dd9b7a79d9656037bb5102fcc2bf.jpg
7f8de72f8c9bcce25dd51453f2384d47.jpg


Tayari halmashauri imempatia mwenyenyumba hiyo kiwanja na anajengewa nyumba na manispaa ili apishe barabara, msingi wa vyumba 4 tayari umekamilika.

8b4347a75e93eeed48ad5c4a8b887a18.jpg
9c3d511eca9e4c7c0366fc3eda74f785.jpg


Hii ni baadhi miradi inayotekelezwa na wananchi kwa kuhamsishwa na WDC ikiongozwa na Diwani Kata kashai

Video ya Diwani wa Kashai akielezea kuhusu barabara hii uploading[emoji116] [emoji116]
 
Tunaomba mtupe na mrejesho wa vipaumbele vya kituo cha mabasi na soko kuu
 
Buwasa wamekatiwa umeme na Tanesco kwenye vyanzo vya maji tokana na kudaiwa. Manispaa ya Bukoba hatuna maji siku ya tatu sasa.
Buwasa wanadai ni deni la mkandarasi aliyefunga mtambo na wizara ndio inatakiwa kulipa. Na wizara haina pesa wanakimbia kimbia. Ni sheeeda - Jimmy Kalugendo, naibu meya
f5a096a163076e886054413a732d9dd7.jpg
975aac44e274b617f392340778162701.jpg
79d36fae766aacf64d588acab9ea1950.jpg
c6a5190570c89b5953baa951fa88955b.jpg
2ed857c313c73e3f5af84265cc3a8b28.jpg
7f66b66e1c1e416411163324e7b6505c.jpg
 
Buwasa wamekatiwa umeme na Tanesco kwenye vyanzo vya maji tokana na kudaiwa. Manispaa ya Bukoba hatuna maji siku ya tatu sasa.
Buwasa wanadai ni deni la mkandarasi aliyefunga mtambo na wizara ndio inatakiwa kulipa. Na wizara haina pesa wanakimbia kimbia. Ni sheeeda - Jimmy Kalugendo, naibu meya
f5a096a163076e886054413a732d9dd7.jpg
975aac44e274b617f392340778162701.jpg
79d36fae766aacf64d588acab9ea1950.jpg
c6a5190570c89b5953baa951fa88955b.jpg
2ed857c313c73e3f5af84265cc3a8b28.jpg
7f66b66e1c1e416411163324e7b6505c.jpg
Msiwe na wasiwasi waliokata umeme ktk mitambo ya maji watawasha hali ya uchafu itakapo wafikisha wao wenyewe kukimbia nyumba zao kwa sababu ya harufu na uchafu. Bukoba mnashanganaza sana kwa kujitumbukiza ktk operesheni ambazo mtu mwenye akili timamu hawezi unga mkono ujinga!
 
Back
Top Bottom