Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mi naona tuwatag hapa, watakuja!Shida tupo wachache wanabukoba walio humu jf ni wengi sana ila kwenye mambo kama haya uwa hawapo.sijui tulilogwa na nani yaani kila mtu angekuwa anatoa hoja tungekuwa mbali sana mi nadhani stendi ingeshafika nusu katika ujenzi ila mbunge,katibu wake hata mayor sijawahi kuwaona vinginevyo mjadala huu hautaleta mafanikio
iiwee.....!kwa kidongo icho,hata kwa dawa sikai bukoba
Umeniuliza na mie nimekuuliza dada, ilikuwaje ukanipotezea?Ni kweli kabisa na hasa kama masterplan mpya itatekelezwa; stand na barabara mpya ambazo ziko ktk mpango
Instanbul usichoke japo sie wengine ni kama tumeshajichokea tayari. Mji wa Bkb ni mchafu kama jiko la wafungwa, barabara zake ni vyembamba kama ulimi wa nyoka. Mitalo ni ya kizamani na imebomoka nahisi ni ya tokea enzi ya mkoloni, nilivyomuuliza jamaa mmoja hapa mjini kanambia eti miji ya kihistoria huwa ni kuweka kumbukumbu. Nikamuuliza kumbukumbu ndo uchafu hivyo, mbona London ni mji wa kihistoria lakini ni msafi na unapendeza?, hakujibu. Majengo ya binafsi yamekuwa meusi utafikiri ya enzi za Uhuru (1961), ofisi za serikali zimejaa utandu wa vumbi na buibui utafikiri magereza ya kitengule. Vibaraza vimetoboka kama kama miamba ya volcano na stand sahivi ni kama (oluju lwenkoko) a.k.a banda la kuku.
Madaraja ya bukoba club na government ni yale ya mbao ya toka enzi za wadachi ukipita misumari imechungulia kama meno ya ngiri, hata majengo ya nssf na lile la bugabo house ya juzi juzi tu nayo yameshachakaa utafikiri yalijengwa wakati wa azimio la Arusha. Ukiwaangalia watu nao wamechakaa hata mtu akivaa suti bado utadhani katokea kwenye kichuguu, juu hadi chini ni vumbi utafikiri yuku migodi ya nyarugusu. Vibarabara vya kuingia mitaani ni vichafu utahisi ni njia za kupita ng'ombe kwenda josho na mazizini, na huwezi amino kama ni njia za kupitisha watu na magari yao. Kwa sahivi watu wote wamekubali kuishi maisha ya kutosumbuana wala kuulizana kuhusu lolote, si vijana wala wazee, mpaka viongozi. Mtu yuko radhi maji ya kinyesi yatiririke mbele ya kibaraza chake lakini si kuhoji, na hata sijuhi ma bwana afya wa mji wako kwa ajiri ya nini hasa. Siku moja nilipita kwenye vi hoteli mshenzi nyuma ya gurio la mabasi kidogo nianguke kifafa, kule ni sawa na dampo la kukuzia nzi na papasi, yaani ni kuchafu heri ya choo changu ni kisafi.
Ya Bukoba ni mambo ya ajabu kuwahi kuripotiwa katika karne hii, mji wote unanuka lakini ukiwasikia wanaoishi ni wajuaji ni balaa. Bado majungu na upuuzi vinawatafuna kila siku wanaongea siasa na kusifiana mpaka Leo. Wanaongea vyama badala ya maendeleo ya mji wao, hawajafahamu mpaka leo kwamba siasa ndo imekuwa sumu kwao na hawataki bado kujifunza. Majani na magugu ni ishara tosha huu mji umekanda na unaelekea kuwa kijiji kikubwa chenye umeme
Yote haya ni kweli hakuna hata chenga ya uongo tena siku hizi kuna ongezeko la watu sijui tunaelekea wapi viongozi wako wapiInstanbul usichoke japo sie wengine ni kama tumeshajichokea tayari. Mji wa Bkb ni mchafu kama jiko la wafungwa, barabara zake ni vyembamba kama ulimi wa nyoka. Mitalo ni ya kizamani na imebomoka nahisi ni ya tokea enzi ya mkoloni, nilivyomuuliza jamaa mmoja hapa mjini kanambia eti miji ya kihistoria huwa ni kuweka kumbukumbu. Nikamuuliza kumbukumbu ndo uchafu hivyo, mbona London ni mji wa kihistoria lakini ni msafi na unapendeza?, hakujibu. Majengo ya binafsi yamekuwa meusi utafikiri ya enzi za Uhuru (1961), ofisi za serikali zimejaa utandu wa vumbi na buibui utafikiri magereza ya kitengule. Vibaraza vimetoboka kama kama miamba ya volcano na stand sahivi ni kama (oluju lwenkoko) a.k.a banda la kuku.
Madaraja ya bukoba club na government ni yale ya mbao ya toka enzi za wadachi ukipita misumari imechungulia kama meno ya ngiri, hata majengo ya nssf na lile la bugabo house ya juzi juzi tu nayo yameshachakaa utafikiri yalijengwa wakati wa azimio la Arusha. Ukiwaangalia watu nao wamechakaa hata mtu akivaa suti bado utadhani katokea kwenye kichuguu, juu hadi chini ni vumbi utafikiri yuku migodi ya nyarugusu. Vibarabara vya kuingia mitaani ni vichafu utahisi ni njia za kupita ng'ombe kwenda josho na mazizini, na huwezi amino kama ni njia za kupitisha watu na magari yao. Kwa sahivi watu wote wamekubali kuishi maisha ya kutosumbuana wala kuulizana kuhusu lolote, si vijana wala wazee, mpaka viongozi. Mtu yuko radhi maji ya kinyesi yatiririke mbele ya kibaraza chake lakini si kuhoji, na hata sijuhi ma bwana afya wa mji wako kwa ajiri ya nini hasa. Siku moja nilipita kwenye vi hoteli mshenzi nyuma ya gurio la mabasi kidogo nianguke kifafa, kule ni sawa na dampo la kukuzia nzi na papasi, yaani ni kuchafu heri ya choo changu ni kisafi.
Ya Bukoba ni mambo ya ajabu kuwahi kuripotiwa katika karne hii, mji wote unanuka lakini ukiwasikia wanaoishi ni wajuaji ni balaa. Bado majungu na upuuzi vinawatafuna kila siku wanaongea siasa na kusifiana mpaka Leo. Wanaongea vyama badala ya maendeleo ya mji wao, hawajafahamu mpaka leo kwamba siasa ndo imekuwa sumu kwao na hawataki bado kujifunza. Majani na magugu ni ishara tosha huu mji umekanda na unaelekea kuwa kijiji kikubwa chenye umeme
Tatizo lingine ya manispaa hii ni kutojali miundombinu iliopo mfano mzunguko Wa mgomba zamani ulikuwa mzr lakini siku hizi ni moja ya majalala mjini sijui wafanya usafi Wa mji wako wapi na kazi yao ni ipi inabidi itengenezwe kwa maua na maji yatiririke kama ilivyokuwa zamani yaaaaaaan nooooo tumechokaBukoba Park 2012, nani anakumbuka?
![]()
Mkuu hii ni Tanzania yetu sote bukoba ni sehemu ya Tanzania hivyo tumeanzisha mjadala huu kuikumbusha serikali wajibu wake.Na wewe haukatazwi kuanzisha Wa kwako hakuna sehemu ya tz ambayo haina matatizo nadhani umenielewaNapenda kuuliza, hivi kama staff wa JF mmo humu je mtu akiweka kitu au hoja ya mkoa wenu labda kutoa ushauri au kusema ambayo yamefichika juu ya viongozi wenu.. mtaacha yasomwe wenzenu wayajadili au mtayafuta!?
Mnakaribishwa sana maana watayasikiaNapenda kuuliza, hivi kama staff wa JF mmo humu je mtu akiweka kitu au hoja ya mkoa wenu labda kutoa ushauri au kusema ambayo yamefichika juu ya viongozi wenu.. mtaacha yasomwe wenzenu wayajadili au mtayafuta!?
Bila shaka mkuu, kwanini tuyafute?Napenda kuuliza, hivi kama staff wa JF mmo humu je mtu akiweka kitu au hoja ya mkoa wenu labda kutoa ushauri au kusema ambayo yamefichika juu ya viongozi wenu.. mtaacha yasomwe wenzenu wayajadili au mtayafuta!?
Ahsante kutufahamisha mbona taarifa ya maendeleo ya miradi hamleti hapa kama mwanzo au mipango haipo tenaAsili ya Neno "BAHAYA" na "BUKOBA" na H. Cory
Wilaya ya Bukoba ya sasa ina machifu wanane na wanyeji wake huitwa Bahaya. Mwanzoni watu hao wote waliishi kati ya Ziwa Victoria na Mto Kagera, Karagwe na Kimwani hawakua wakiitwa jina moja; wala nchi yenyewe haikua ikiitwa kwa jina moja. Watu walitengana katika sehemu ndogo ndogo kwa kufuata hali ya utawala wa nchi ijapokuwa sasa majina ya Buhaya na Bukoba yanatumika sana na yanakubaliwa na wenyeji. Lakini majina ya asili ya makabila hayakupotea:-
Wenyeji wa utawala wa Kianja ni Bahamba
Wenyeji wa utawala wa Kiamtwara ni Bahyoza
Wenyeji wa utawala wa Bukara ni Bakara
Wenyeji wa utawala wa Kiziba ni Waziba
Wenyeji wa utawala wa Bugabo ni Bahendangabo
Wenyeji wa utawala wa Ihangiro ni Banyaihangiro
Wenyeji wa utawala wa Missenyi ni Babumbiro
Wenyeji wa utawala wa Karagwe ni Wanyambo
Banyambo hawakufikiriwa kuwa ni Bahaya safi kwasababu ya hali yao ya Kirundi na pia kuna hitilafu katika lugha yao.
"Bahaya" mwanzoni lilikua ni jina walilopewa wavuvi waishio pwani ya Ziwa na nimeambiwa kwamba lilikuwa tusi kidogo kabla ya kufika kwa Wazungu mtu kuitwa Muhaya, kwasababu wavuvi walifikiriwa kuwa watu wa hali ya chini na wasio na mali halisi. "Uhaya" ilikua ni sehemu za Kishebuka na Bwahama, lakini hata wakati huo jina hili lilikua limekwishatumiwa na makabila ya ujirani kwa nchi yote hiyo. Kwahiyo si ajabu kwamba jina hili lilikubaliwa na wadachi.
"Bukoba" lilikua jina la ukoo ulioishi katika eneo la mji wa sasa wa Bukoba na Kizingira chake. Katika ramani ya zamani ya Wadachi ya 1892 jina "Bukoba" laonekana hasa sio jina la mji (ambao haukuwepo wakati huo) bali jina na eneo lenye vilima vizungukavyo bonde la mto Kanoni.
![]()
Mkuu hawa jamaa watakuchosha bure, huoni walivyokaa hata wao wenyewe? Wataleta taarifa zipi wakati wako fragile hivi, just leave it.Ahsante kutufahamisha mbona taarifa ya maendeleo ya miradi hamleti hapa kama mwanzo au mipango haipo tena
Tushirikishane ulikua ni mradi wa miezi 9 ambayo tayari imekwisha. Mwezi huu nitaleta taarifa ya jumla ya mradi. Aidha jukwaa hili ni la kujadili mipango yote ya maendeleo ya jimbo la Bukoba. Mimi nahusika na sehemu ya "Tushirikishane" tu, vingine naleta kama nyongenza.Ahsante kutufahamisha mbona taarifa ya maendeleo ya miradi hamleti hapa kama mwanzo au mipango haipo tena