TARIFA YA KUKAMILISHA MPANGO WA MUDA MFUPI WA UPATIKANAJI MAJI SAFI NA SALAMA -
NZEGA KWA KUONGEZA MITA ZA UJAZO 1300
Tarifa hii itagusia zaidi ukamilishwaji wa ahadi ya maji ya uhakika ambayo ilikuwa moja ya kipaumbele kwenye
mpango kazi wa Mradi wa Tushirikishane katika Jimbo la Nzega. Ahadi hii imekamilika kwa kwa asilimia mia.
Na hatua hii imefikiwa ndani ya miezi saba tu ikiwa ni miezi miwili mapema zaidi ya tarehe iliyopangwa.
Katika ahadi ya maji ya uhakika, lengo liliwekwa kuwa na vyanzo vyenye uwezo wa kuzalisha na kusambaza
mita za ujazo 1300 kwa siku. Matokeo ndani ya miezi saba yanadhihirisha kufanikisha na kuvuka lengo kwani
sasa bwawa la Uchama linasabaza maji safi na salama zaidi ya mita za ujazo 1700 kwa siku.
Kwa mujibu wa makubaliano ya wadau na kalenda ya mradi, mpango kazi huu ulipaswa kukamilika mwezi
Aprili, 2017.
Tarifa ifuatayo ni majumuisho ya ukamilishaji wa ahadi ya maji ya uhakika katika Jimbo la Nzega Mjini.
1. Umefanyika ujenzi wa mfumo wa kuzahisha maji (slow sand filter) wenye uwezo wa kuzahisha maji
kiwango cha kubiki mita za ujazo 1200 kwa siku
2. Umejengwa mfumo wa kusafisha maji kwa kiwango cha kubiki mita za ujazo mita 30-40 kwa saa sawa
na wastani usiopungua kubiki mita za ujazo 600 kwa siku
3. Zimenunuliwa pumps za kuongeza ujazo wa Maji ghafi kwenye mfumo wa kusafisha (70m3/hr)
ingawaje baada ya kuamua kutumia bwawa la Uchama pump ya TUWASA imeendelea kubakia hapo
kwani ina uwezo wa kutosheleza mfumo mzima bila kuegemea bwawa la Uchama (140m3/hr)
4. Zimefugwa (bulk meter) kwa maji ghafi na maji yanayozalishwa ili kujua uwiano wa uzalishaji na
usambazaji
5. Kumerekebishwa mfumo wa pump za kusafirisha maji ili kuwa na uwezekano wa matumizi ya pump
tatu.
6. Umefanyika ukarabati wa tank la maji la parking (135m3) ambalo lilikuwa halitumiki kabisa kwa sasa
linatumika na kufanya Gati la parking kutoa huduma ya maji masaa yote 24.
7. Yamefungwa matanki matatu ya (5000Ltd) kwenye vituo vya maji Ipilili, Maporomoko na Uswilu
8. Vile vile zimenunuliwa pikipiki mbili kwa ajiri ya kusaidia shuguli za uzalishaji na usambazaji maji katika
halmashauri ya mji wa Nzega.