TARIFA YA MAENDELEO YA MRADI WA TUSHIRIKISHANE KWENYE JIMBO LA NZEGA MJINI KATIKA KIPINDI CHA MWEZI OCTOBA 2016 MPAKA JANUARY 207
MAENDELEO YA MRADI
1. Kusimamia ukamilishaji wa ujenzi wa kituo kipya cha mabasi Nzega
Katika tarifa iliyopita ya mwezi September mpaka Octoba, ilielezwa kuwa Kuanzia tarehe 17/10/2016 Halmashauri ya Mji wa Nzega ilianza kutoa fomu kwa ajili ya maombi ya zabuni ya ujenzi wa vibanda vya biashara katika kituo kipya cha mabasi Sagara, Nzega. Zoezi hilo lilikamilika tarehe 19/10/2016, na hatua nyingine za ukamilishaji wa upataji wa zabuni unaendelea.
MAENDELEO MAPYA KATIKA KIPINDI CHA MWEZI OCTOBA 2016 MPAKA JANUARY 2017
Zoezi la kupata wazabuni katika awamu ya kwanza umekamilika na wazabuni sitini na moja (61) wamekidhi vigezo vya kupewa zabuni kama washindi. Hivyo muda wowote kuanzia sasa majina yao yatatanganzwa ili waweze kuanza ujenzi
Kutokana na ukubwa wa eneo lililotengwa kwa jili ya ujenzi wa vibanda kuwa kubwa, Halmashauri iliamua litegwe mara mbili na kila moja liwe na mchakato wake wa zabuni. Kukamilika kwa zabuni ya kwanza kumetoa fursa kwa zabuni ya eneo jingine kutangazwa tarehe 19/01/2017. Mchakato wa tathmini ya kuwapata washindi wa zabuni wa awamu hii bado unaendelea
Vile vile, mwezi huu wa kwanza, kumefanyika jaribio la kupima kiwango cha maji kinachotoka kwa saa kutoka katika kisima kilichochibwa hapo kituoni ili kutambua mashine za aina gani zinaweza kufungwa kwa ajiri ya kusukuma maji katika mantaki ambayo yatatumika kusambaza maji kwa watumiaji hapo kituo cha mabasi.
2. Kuhakikisha ujenzi wa nyumba ya Daktari katika kituo cha Afya Nhobora unakamilika
MAENDELEO MAPYA KATIKA KIPINDI CHA MWEZI OKT. 2016 MPAKA JANUARY 2017
Kazi ya upauaji wa nyumba ya Daktari kwa kiwango kikubwa imekamilika kama habari-picha mbali mbali zinavyooneka katika tarifa zetu za kila wiki. Hatua iliyobaki ambayo ndiyo inayofuata ni kupiga lipu.
3. Kusimamia ukamilishaji wa mpango wa muda mfupi wa upatikanaji wa maji safi na salama –Nzega kwa kuongeza mita za ujazo 1300
MAENDELEO YA MAPYA KATIKA KIPINDI CHA MWEZI– OKT. 2016 MPAKA JANUARY 2017.
Kazi ya ujenzi wa machujio ya maji matatu umekamilika. Machujio yote kwa sasa yanafanya kazi. Vile vile mashine za kusukuma maji zote tatu zimefungwa na zinafanya kazi. Lakini kutokana na ukarabati wa miundombinu ya maji kwa watumiaji, mashine moja imesimamishwa kwa sasa.
Vile vile idara ya maji bado inaendelea na ukarabati wa miundombinu ya maji katika mitaa mbali mbali ya Nzega Mjini. Mfano tanki lililopo Pakingi lililokuwa halimfanyi kazi kwa muda mrefu sasa limeanza kufanya kazi. Pia magati ambayo yalikuwa hayatoi maji, likiwemo gati la Pakingi sasa yanafanyakazi. Hii imewezesha upatikanaji wa maji kwenye maeneo mengi kuwa ya uhakika kulinga na ratiba. Haya ni maendeleo na ni tofauti na siku za nyuma ambapo baadhi ya maeneo yalikuwa yanakosa maji katika siku yao ya kuwa kwenye ratiba ya mgao.
Tarifa ya mwezi wa pili, mwaka huu kuhusu maendeleo ya mradi huu itakuja na majibu ni kiwango kipi cha ujazo wa Maji umeongezeka kwa sasa tangu ukarabati huu miundombinu ya maji uanze kwani hivi sasa bado miundombinu ajakamilika vizuri
4. Kukamilisha mabweni na madarasa ya kidato cha tano na cha sita katika shule ya sekondaro Bulunde.
MAENDELEO MAPYA KATIKA KIPINDI CHA MWEZI – OKT. 2016 MPAKA JANUARY 2017
Ujenzi wa mabweni mawili ya wanafunzi katika shule ya sekondari Bulunde, ujenzi huo mwezi huu wa kwanza 2017 umendelea kwa mabweni hayo mawili kueezekwa kwa bati, hivyo hatua hii inafanya kuwepo na madarasa mawili ya kusomea ambayo yamekamilika pamoja na mabweni ya wanafunzi mawili ambayo yamepauliwa hivyo basi hatua inayofuatia baada ya upauaji wa mabweni haya bado ofisi husika inayohusika na usimamizi wa ujenzi huu ambayo ni ofisi ya serikali ya mtaa wa nzega mashariki hawajaitoa Siku wakitoa mtaipata kupitia tarifa zetu za kila wiki.
Imeandaliwa:
Joseph Sanga
Afisa mawasiliano wa mradi-Nzega