Mjamzito msaada

Mjamzito msaada

utafiti

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2013
Posts
12,783
Reaction score
7,667
Habari wana jf, kuna ndugu mmoja wa familia yangu ni mjamzito ila anatatizo lakuumwa na kichwa sana mpaka anakua hajielewi, hua anatumia dawa za hospital, sijajua kama kuumwa huko kuna uhusiano wowote na mimba yake, kwa anaefahamau kidaktari zaidi;
Natanguliza shukrani
 
mpe pole je ni miezi mingapi huo ujauzito...?
 
Ameenda clinic na kueleza hilo?! Nashauri aende na watamfanyia vipimo.Sometimes kuumwa kichwa huwa inawapata wajawazito.Lkn anything in extreme hapo kuna mashaka
 
Ni mimba yake ya ngapi? Na ana umri gani? Je ameolewa au kaipatia tu nyumbani? Dr D.o.D
 
Aende tu hospital huko atapimwa na kujulikana kama ana ugonjwa(Most Likely itakuwa Migraine Headache) au ana 'wenge'(Mauzauza yasiyoweza kupimwa na kuonekana kitabibu lakini yanamsumbua mgonjwa).

Kama ni ugonjwa wa kawaida atatibiwa tu hospitali ila kama ni 'wenge' huenda atashauriwa atumie njia mbadala kama kupumzika tu nyumbani, 'Kupigwa machine aka Pipe', Kuliwazwa, Dua, Maombi nk.

'Wenge' ni Common sana kwa wanawake hususani wenye mimba hasa ya Kwanza na kama ni mimba changa.
 
Oookey ujue nini! Ki kawaida mimba huwa zinakuja na mambo mengi sana kitabia (sio ugonjwa) ila kwa huyo ndugu yako hebu jaribu kumpeleka hsptl hapo mtamueleza dkt kwa kina kisha atajua ni dawa gani atampa kwa huo muda hadi atakapojifungua :Nb asimeze dawa kiholela bila ushauri wa kitaalamu akiwa ktk hali ya ujauzito dr D.o.d
 
Asante dr d.o.d
 
Anywe maji mengi,mm pia nilikua na hilo tatizo,nikashauriwa kunywa maji,kila siku nakunywa lita tatu,na sijaumwa kichwa tena!
 
Anywe maji mengi,mm pia nilikua na hilo tatizo,nikashauriwa kunywa maji,kila siku nakunywa lita tatu,na sijaumwa kichwa tena!

Yah hilo kweli watu wengi hawanywi maji ya kutosha na hata kupata usingizi wa kutosha pia.
 
Back
Top Bottom