Tripple MM
JF-Expert Member
- May 31, 2023
- 417
- 567
km mama yao atadhulumiwa wana kila sababu ya kudaiWatoto wa nje ya Ndoa wa mke wa Mrema wakija kudai mali za Mama yao alizochuma na mume wake wa ndoa hapo inakaaje kaaje?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
km mama yao atadhulumiwa wana kila sababu ya kudaiWatoto wa nje ya Ndoa wa mke wa Mrema wakija kudai mali za Mama yao alizochuma na mume wake wa ndoa hapo inakaaje kaaje?
wana haki si ndo maana mh. jaji kaamua nao waingizwe kwa mirathihaki ya mtoto wa kambo kurithi hapo ipoje
Mama yao si ndio kafariki, halafu sasa waende kwa mume na watoto halali wa marehemu mama yao kudai mali, mali ambazo mume halali kachuma kwa msaada wa mke wake na watoto wake. hiyo inakaaje kaaje. Ukizingatia baba yao ambae ndiye mchepuko tu kwa marehemu mama yao nae ndio anasubiri wapewe mgao ili achukue mali ambazo hajachuma kupitia watoto wake haramu?km mama yao atadhulumiwa wana kila sababu ya kudai
...MIEZI MITANO na Siku Kadhaa....Walichuma Nini ??...amekosa aibu, ndoa yenyewe haikufikisha hata mwaka mmoja halafu anataka mirathi na huku hakuachiwa mtoto
Huyo ni mungu wa IsraelNdio maana Mungu alisema anachukia wana ndoa kuachana
Malaki 2:16
“Ninachukia kuachana,” asema BWANA, Mungu wa Israeli, “pia nachukia mtu anayejivika jeuri kama vazi,” asema BWANA Mwenye Nguvu Zote.Kwa hiyo jihadharini wenyewe katika roho zenu, wala msije mkavunja uaminifu##Ukisha achana na mke au mume kinachofuata ni vurugu tu,hasa kama mna watoto...
hajajumuishwa "ajajumuishwa" ni kiswahili cha BURUNDI.Mahakama Kuu ya Tanzania, masjala ndogo ya Temeke jijini Dar es Salaam, imemaliza mvutano kuhusu nani wanastahili kunufaika na mali za aliyekuwa mwanasiasa mkongwe, Augustino Mrema aliyefariki Agosti 21 mwaka
jana.
Katika hukumu iliyotolewa jana na Jaji Augustine Rwizile, amewataja wanufaika hao kuwa ni pamoja na Doris Mkandala, maarufu kama Doreen Kimbi, aliyefunga ndoa na Mrema Machi 24, 2022 na Mrema akafariki siku 150 baada ya ndoa. Doris Mkandala, maarufu kama Doreen Kimbi, aliyefunga ndoa na Mrema Machi 24, 2022 na Mrema akafariki siku 150 baada ya ndoa.
Ndoa hiyo ilifungwa katika Parokia ya Uwomboni, Jimbo Katoliki la Moshi, wakati huo Mrema akiwa na umri wa miaka 77 na Doreen akiwa na umri wa miaka 38, ndoa ambayo ilipata umaarufu mkubwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii.
Hadi umauti unamkuta, Mrema alikuwa Mwenyekiti wa Taifa wa Tanzania Labour Party (TLP) na alishawahi kushika wadhifa wa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Ndani na pia Waziri wa Kazi na Ajira na Mbunge wa Vunjo.
Jaji Rwizile katika hukumu yake hiyo, amewajumuisha pia watoto watatu wa Mrema waliozaliwa nje ya ndoa kama wanufaika wa mali za mwanasiasa huyo sambamba na watoto wa marehemu ambao walizaliwa ndani ya ndoa.
Watoto hao wa nje ya ndoa ni Elizabeth Mrema (52), Elizabeth Mrema (43) na Goodlove Mrema (18), wakiungana na watoto wengine wa Mrema, Mary Mrema (48), Cresensia Mrema (45), Michael Mrema (40) na Edward Mrema (38).
Katika orodha hiyo ya watoto wanufaika wa mali za marehemu yumo Peter Mrema (37), ambaye ameteuliwa kuwa msimamizi wa mirathi, huku mahakama ikilikataa pingamizi lake la kutaka ajumuishwe kuwa msimamizi mwenza.
Alitaka hivyo akijenga hoja kuwa Peter Mrema ambaye aliteuliwa na kikao cha familia kuwa msimamizi, alimbagua kuhusu mali za marehemu na kumwacha katika orodha ya wanufaika na kuwaacha watoto wanne waliozaliwa nje ya ndoa.
Kwa mujibu wa Jaji, mvutano ulikuwa baina ya makundi mawili, kundi moja likiwa ni na mke wa marehemu na watoto waliozaliwa nje ya ndoa na Peter Mrema aliyeungana na watoto wengine wa marehemu Mrema.
Akipinga Doreen kuwa msimamizi mwenza, mtoto huyo wa marehemu (Peter) alidai Doreen sio mtu wa kumwamini na aliolewa na baba yao wakati ndoa yake (Doreen) ya awali haijavunjwa na amekuwa akibadili majina yake mara kwa mara.
Doreen alipinga madai hayo akisema walishaachana kwa talaka na mume wake wa kwanza na hivyo ndoa kati yake na Mrema ilikuwa ni halali, hoja ambayo pia ilikubaliwa na Jaji kwamba kulikuwa hakuna uthibitisho ana ndoa nyingine.
Kuhusu Doreen kuwa msimamizi Kuhusu ombi la Doreen kama anastahili kuwa msimamizi mwenza na Peter wa mirathi ya mumewe, Jaji alisema mtu yeyote anaweza kuteuliwa kuwa msimamizi hata kama sio mwanafamilia au mnufaika ilimradi tu asimamie mali vizuri.
"Hakuna ubishi kuwa muombaji(Peter) ana umri wa miaka 37 na hakuna ubishi ni mtoto wa marehemu na ndio maana alipendekezwa ili asimame kama msimamizi na ameiambia mahakama atatenda haki katika usimamizi huo" alisema Jaji.
Kwa upande mwingine, Jaji alisema Doreen ni mjane wa marehemu na kulingana na ushahidi, hayuko katika uhusiano mzuri na muombaji Peter Mrema. Kulingana na ushahidi wake, walifunga ndoa Machi 24, 2022 na mumewe alifariki Agosti 21, 2022 na muda mwingi mumewe alikuwa mgonjwa na ndio maana waliondoka Moshi na kwenda Hospitali ya Taifa Muhimnbili (MNH) kwa matibabu.
"Katika kuamua hili, nashawishika kusema kwa kuwa Doreen hana uhusiano mzuri na Peter, sio sahihi kumteua kuwa msimamizi mwenza kwa kuwa wawili hawatakubaliana katika masuala muhimu," alisema Jaji Rwizile.
Nani wanastahili kuwa wanufaika?
Jaji alisema kuhusu nani wana uhalali wa kisheria wa kuwa wanufaika, alisema mali hizo zinapaswa kuganywa kwa mke na watoto wa marehemu kama sheria inavyoelekeza pale mtu anapokufa bila kuacha wosia.
"Ni ushahidi wa muombaji (Peter) kuwa watoto wanaotajwa kwenye pingamizi lililowasilishwa na mjane sio watoto wa marehemu hivyo wasiwemo kwenye orodha ya wanufaika na ushahidi wake uliungwa mkono na dada yake," alisema.
Kulingana na Jaji, muombaji huyo ambaye ni mtoto wa marehemu alisema wakati wa uhai wake, baba yake hakuwahi kuwatambulisha kwenye familia yao na wala hajawahi kutamka au kuthibitisha kuwa hao ni watoto wake pia.
Hata hivyo, watoto hao, Goodlove Mrema, Elizabeth Mrema na Elizabeth Mrema Junior walitoa ushahidi kuwa wao ni watoto halali wa Mrema na katika kuthibitisha hilo waliwasilisha vyeti vya kuzaliwa, Jaji alisema ushahidi pekee uliopo ni vyeti vya kuzaliwa ambavyo watoto hao waliviwasilisha kortini na havijawahi kuthibitishwa kuwa ni feki au vilipatikana isivyo halali na vilipokelewa mahakamani kama vielelezo bila pingamizi lolote.
Kwa mujibu wa Jaji, sheria iko wazi kuwa jina la mzazi linaloingizwa kwenye rejista ya msajili na kutunzwa inatosha kabisa kuthibitisha kuhusu nani ni mzazi halali wa mtoto.
"Kwa hiyo nasema Godlove, Elizabeth Senior na Elizabeth Junior nao ni watoto wa marehemu na waorodheshwe katika orodha ya vilivyopokelewa kama ushahidi.
Hatari sana hiiiNa mimi nimeshangaa. Ukizingatia Tanzania kupata vyeti vya kuzaliwa ni rahisi mno. Yaani mtu anaweza kuwa na cheti cha kuzaliwa kinachoonyesha Jakaya kikwete ndo Baba yake.
km amefariki naona kuna mtiti hapo..Mama yao si ndio kafariki, halafu sasa waende kwa mume na watoto halali wa marehemu mama yao kudai mali, mali ambazo mume halali kachuma kwa msaada wa mke wake na watoto wake. hiyo inakaaje kaaje. Ukizingatia baba yao ambae ndiye mchepuko tu kwa marehemu mama yao nae ndio anasubiri wapewe mgao ili achukue mali ambazo hajachuma kupitia watoto wake haramu?
Sheria inaruhusu hilo, sheria hiyo ilitungwa na wendawazimu au watu wenye akili timamu?
Bwana mdogo acha porojo aseeSheria ya serikali inatambua mtoto halali Kwa nasaba sio ndoa
Kuna namna ya kwenda kupinga hilo jamboNa mimi nimeshangaa. Ukizingatia Tanzania kupata vyeti vya kuzaliwa ni rahisi mno. Yaani mtu anaweza kuwa na cheti cha kuzaliwa kinachoonyesha Jakaya kikwete ndo Baba yake.
ashukuru mungu amepata bonus bure...MIEZI MITANO na Siku Kadhaa....Walichuma Nini ??...
angekuwa ameolewa na mtu wa kawaida asiye na mali hiyo miezi mitano angeishia kupata vyombo vya harusi tu na kurudi kwao...Miezi MITANO na Siku Kadhaa....!!!
mi sijali sheria inasemaje kuhusu kurithi mali kwa mtoto wangu wa nje ni lazima naye apate mgao sawa na watoto wa mke anayedaiwa ni wa ndoa. Watoto ni watoto tu hata wazaliwe na mama kumi mbalimbali kwa baba mmoja, hata wa wa michepuko nao wapate urithi wa baba yaoSheria ya zamani ilikuwa inamkataa mtoto wa nje ya ndoa.
Ila sheria ya mirathi inayotumika siku hizi inamkubali mtoto wa nje ya ndoa na urithi anapata
Sasa fanya in reverse, kwamba ni baba ndio kafariki, halafu watoto wake wa nje wanakuja kudai mali zilizochumwa kwa pamoja na mke na watotRo halali wa ndoa..,km amefariki naona kuna mtiti hapo..
Wewe ndo ukitafakari vizuri,Sheria za Tanzania zinawakubali watoto wote ili mradi wawe kweli ni watoto wa marehemu.Mambo ya nje ya ndoa ni mambo yasiyo zingatiwa tena na Sheria za nchi.Yaani watoto wa nje ya ndoa? Huyu jaji kachanganyikiwa.
Mahakama Kuu ya Tanzania, masjala ndogo ya Temeke jijini Dar es Salaam, imemaliza mvutano kuhusu nani wanastahili kunufaika na mali za aliyekuwa mwanasiasa mkongwe, Augustino Mrema aliyefariki Agosti 21 mwaka