Wanawake wengi wanaweza kukaa muda mrefu baada ya kufiwa na ndipo wakaamua kuolewa, na wengine wanaweza wasiolewe kabisa. Lakini yote haya yanategemea hali ya uchumi ya huyo mama, baba wa familia kabla hajafa je aliacha uchumi imara wa familia? je, ndugu wa mume wanaingilia namna ya ku-run mali alizoacha marehemu? na pia je mjane ana mahusiano mazuri ama mabaya na ndugu wa marehemu mume wake?
Pia umri wa mjane inaweza kuwa factor kubwa sana, suppose kama hajafikisha miaka 30? Wengi wakifiwa wakiwa na umri mdogo hutamani kuolewa tena, na wengi wakiwafiwa wakiwa na umri mkubwa huamua kubaki single na kuamua kumegwa kisiri siri pale anapohitahitaji huduma.
Kwa upande wa wanaume, wengi huoa haraka/mapema mara baada ya kufiwa, nadhani hili halina uhusiano na mambo ya kumega, bali ni swala zima kwamba nyumba ni mke. Nyumba anayoisha mwanaume single haiwezi ikawa as neat as nyumba inayokaliwa na wana ndoa. Na pia haiwezi kuwa organised (mpangilio wa vitu ndani ya nyumba) na ratiba ya milo inayoeleweka. Akina baba wa kibantu, tumezowea kupikiwa, kufuliwa na wakati mwingine kulelewa kama watoto wadogo.
Mke akifariki, nyumba lazima ikumbwe na matatizo ya usafi, hata kama familia ina msichana wa kazi lakini hawezi kuwajibika ipasavyo ikilinganishwa na mama mwenye nyumba anapokuwepo.
Personally siwezi kumpangia aolewe lini in case ikitokea nimefariki, hayo ni maamuzi yake, maana inawezekana anaweza kuwa anamegwa hata ukiwa hai, sasa je ukifa si ndio atamegwa vizuri tena kwa nafasi. Muhimu ni kwamba ahakikishe anatunza watoto kama tutakuwa tumejaaliwa kuwa na watoto, maana wengine wakioa/olewa wanasahau watoto kabisa.