MTM, suala la mume kuonekana ndie anayestahili kutoa urithi katika jamii yetu ya leo ni hata kama mwenye kutafuta ni mke, hiyo inatokana na mabadiliko ya mifumo katika jamii. Historia inafundisha kuwa kabla ya binadamu hajaanza kuishi kama familia (wakatin ulw wa kina Zinja (Zinjanthropus) ambapo binadamu aliishi kwa kuhangaika na kula matunda na nyama za porini, dhana ya "mali" haikuwepo kichwani kwake. Lakini dunia ilivyozidi kubadilika matunda na wanyama kuanza kupotea katika mazingira ya karibu, ikiwa "mtu mke" kwa kuwa alikuwa anamajukumu ya kuzaa aliwajibika kutulia sehemu na hapo alipoamua kutulia pakawa ndo nyumbani kwake. Zama hzo mwanaume alikuwa na nguvu ya kuzunguka porini kuwinda na kutafuta matunda na mfumo uliokuwepo ni kama wa wanyama pori, unazalisha na kwenda hakuna jina baba kwenye familia!!.
Hali ilivyozidi kuwa mbaya kwenye maumbile ya dunia,ikalazimu wanaume waanze kutafuta kwa kuishi na kwa kuwa walikuwa na nguvu za kuzalisha mali na watoto, historia inasema ilikuwa rahisi kukubalika kukaa kwnye himaya za wanawake na wakati huo, mke alikuwa ndio anamiliki mali yaani eneo analoishi , watoto na mwanaume atakayejitokeza kuomba hifadhi!....Kukuwa kwa jamii kulileta mifarakano na tamaa ya kuwa na mali nyingi, hivyo mke kama mmiliki wa familia na mali akashindwa kukabiliana na cnagamoto hizo za kimaisha hivyo kwa kuwa mume alikuwa na nguvu za kuilinda familia na mali, ikawa yeye ndio kichwa na familia na kwa ajili ya usalama (security) kwenye mali binafsi (private property),jamii ilibadilika na tokea hapo mume akawa anaoekana ndie mwenye kuweza kusimamia mali katika jamii na hali hiyo imepata nguvu zaidi pale ulipoanza utaratibu wa kuoa na kuoana ambapo mke na mume wanapooana, mke anakuwa amepoteza hadhi ya kuendelea kuwa kwenye jamii yake (baba na mama yake) na badala yake, yeye na watoto atakao wazaa na mali atakayochuma inachukuliwa kuwa ni sehemu ya mali za mumewe!...(Lakini haipo hivyo kwa jamii zote).
Kwa wafuasi wa dini ya kikristu Bibilia inatafsiri ndoa kama muungano unaomtoa mume kwa wazazi wake na kumpeleka kwa mkewe ili wakaishi pamoja kwa nukuu ifuatayo " KWA SABABU HIYO, MTU MTU ATAMWACHA BABA YAKE NA MAMAN YAKE, ATAAMBATANA MKEWE NAO WAWILI WATAKUWA MWILI MMOJA" (Efe 5:31).
Kwa wafuasi wa Kikristo Bibilia kupitia Waraka wa Paulo Mtume kwa Waefeso sura ya 5:22 -25, inaelekeza zaidi wanawake kuwa na utii kwa waume zao ("enyi wake watiini waume zenu ...........kwa maana mume ni kichwa cha mkewe........kama vile kanisa limtiivyo Kristo vivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo).
Kuhusu waume, Bibilia inaweka msisitizo zaidi kwa wanaume kuwapenda wake zao na kukazia kuwa "ampendae Mkewe hujipenda mwenyewe....kwa maana nyingine ukimpenda mkeo utamlinda na usipotaka apate tabu ukifa, acha wosia kuhusu mali uliyoichuma nae akiwemo yeye mwenywe na watoto>.....[quote]KWA KUWA HAKUNA "MFUME JIKE", NI PIA RAHISI KUSEMA HATA HUO UNAOITWA "MFUMO DUME" NI PROPAGANDA TU ZA WANAHARAKATI AMBAO WENGI WAO KAMA HAWAN NDOA BASI WANAJARIBU KUKWEPA WAJIBU WAO KATIKA NDOA KWA POROJO ZA MANENO.......