Nimekuwa nikijizuia sana kuandika kuhusu hii topic lakini ngoja niseme machache kuhusu concept ya kujiajiri na kuajiriwa kwa wahitimu/vijana.
Katika dunia ya leo, vijana wengi wabunifu na wanaojiajiri wanatoka katika nchi zinazoeendelea na masikini kama Tanzania. Swala la kwamba nchi tajiri kama Marekani na nchi za bara la ulaya zinaandaa wanafunzi wake wajiajiri ni uongo wa wazi wazi kabisa.
Nadhani hili swala la viongozi wengi wa siasa kupigia kelele swala la vijana kujiajiri ni wao kukukosa ubunifu wa kutengeneza ajira na kuanza kupeleka lawana kwa vijana kwamba wao ndo wanabweteka na hawataki kujiajiri. Serikali ndo inatakiwa itengeneze ajira, hizi kelele za vijana kujiajiri ni serikali kukosa ubunifu katika uchumi.
Statistics zinaonyesha vijana wanajiajiri sana kwenye nchi masikini kuliko nchi tajiri na zilizoendelea.
This chart shows the share of self-employed workers in selected countries in 2019.
www.google.com
Self employment statistics 2018
1. low income countries = 81%
2. Middle income = 47%
3. High income = 12%
Marekani ni 6% tu ya watu ndo wamejiajiri
Mwaka jana Burundi ndio iliongoza kwa kuwa na asilimia karibu ya 94% ya self-employment sasa haya malamiko kwamba vijana wa nchi masikini hawataki kujiajiri yanatoka wapi?
Serikali ijitahidi kutengeneza ajira, vijana wanapigana vya kutosha na sio wa kulaumiwa.
View attachment 1268554