Pulchra Animo
JF-Expert Member
- Jun 16, 2016
- 3,718
- 3,465
Kuliko endelea wahitimu wanaenda kuanzisha vibiashara vidogo vidogo halafu ndio unakuwa solution ya tatizo la ajira?
Muhitimu wa chuo atafanyaje biashara ya vitumbua ambayo ni kubwa kumletea maendeleo wakati hana mtaji, hana uzoefu, hajasomea kuhusu biashara? Wachache wanaweza kuanzia from scratch wakasota na wakafika scale kubwa baada ya muda, lakini hao ni asilimia ngapi ya wahitimu wote? Sio kila mtu amezaliwa kufanya biashara, ndio maana hata huko walikoendelea ni watu wachache sana wamejiajiri
Small and medium-sized businesses ndizo zimebeba the lion’s share ya workforces za hao walioendelea. Na hizo biashara ndogo nyingi zake ni ndogo kweli (sole proprietorships).
Ukikalia takwimu zetu utapotea bure, my dear; reliability yake iko chini sana. Kuna watu ni waajiriwa (e.g., houseworkers, sehemu kubwa ya makonda na matingo, waangalizi wa mifugo, etc.), lakini kitakwimu wanahesabika kama self-employed kwa sababu hakuna returns zozote zinazopelekwa serikalini kuonesha kuwa ni sehemu ya waajiriwa.