Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Wakaazi wa Chato wakihojiwa na BBC mwaka mmoja tangu aondoke Magufuli wametoa hisia zao tangu aondoke mpendwa wao mzawa wa Chato ikiwemo sekta ya biashara na maendeleo.
Wakazi hao wamelalamikia mzunguko mgumu wa biashara kwasasa Chato huku viwanja navyo vikiporomoka bei kulinganishwa wakati hayati Magufuli akiwa Rais.
Moja ya mjasiriamali aliyekuwa anafanya biashara ya chakula, anasema wateja wake wakubwa walikuwa maafisa usalama lakini sasa mauzo yamepungua kwa wastani zaidi ya nusu na mikopo wanayoweka kwenye biashara haiendi hivyo kufanya urejeshaji wake kuwa mgumu.
Moja ya mjasiriamali ameomba Rais aliye madarakani aongeze ziara zake Chato ili kuchangamsha uchumi kutokana na wageni hivyo kupata mauzo mazuri lakini sasa hata wapangaji waliohamia na walionunua viwanja kuwekeza wameacha, amedai Chato ilikuwa inajengwa na wageni.
Amemuomba Rais awe anawatembelea na anajua wageni watakuja wawe wanafurahi kama alivyokuwa Rais aliyepita na wala hawachukii bali walizubaa sana.
Mwananchi wa mwisho ameomba miradi yote aliyoanzisha Magufuli Chato ikamilike ili kurejesha mzunguko wa fedha ikiwemo mbuga ya Burigi, chuo kikuu nk