Mji wa Dar es Salaam ni mishe mishe

Mji wa Dar es Salaam ni mishe mishe

Saad30

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2020
Posts
2,737
Reaction score
5,464
Salamu wakuu.

Mji huu Dar es salaam ni Mji mzuri sana katika mishe za hapa na pale. Mji huu haumkatai mtu kama usipoweka starehe mbele.

Pisi za Mji huu hazina upendo kwa apeche alolo. Pisi za Mji huu zinataka kuona unatembea na AC yako ili wakupe unapopataka lakini hawakupi moyo wao.

Huko Mbagala watu wamevurugwa yaani naweza kusema ule ni Mkoa ambao upo ndani ya Jiji hili Dar es salaam.

Huu ndio Mji unaotoa hela na kuzitawanyisha kwa watu wamikoani. Hata ufanye nini huwezi kuukataa huu Mji wa Dar.

HUU mji ni kama maji vile usipoyaoga, utakunywa au kunawa yaani huwezi kuukimbia.

Kwa ufupi Jiji la Dar es salaam hauna maadui
Yaani Rafiki kwa kila mkoa.


Utaitwa Handsome hata kama sura mbaya, na hii ndo Daslam unakana kwenu huna haya?
 
Nimeishi mikoa msingi sana, Dar es salaam ukiwa na pesa na kazi binafsi is one of the best city to live...

Ila Dar es salaam bila pesa hapafai hata kidogo, na nikisema pesa simaanishi vihela, hapana.

Ubaya wa Dar es salaam:

1. Ukiwa mwajiriwa hapafai.
2. Kulea watoto sio pazuri.
3. Ni mji wa watu waongo ongo.
 
Dar kero nyingi sana. Ukiwa na hela sawa ila sasa wenye hela ni asilimia ndogo sana wengi maisha yakwaida tu.

Juzi nimeona mwanamke amebanwa kwenye mwendokasi mpaka anataka kukata roho analia tu "yesuuuuuu nakufaaaa".

Shida zote hizo za nini?
 
Dar hata kama huna hela tutakupenda, wewe kuwa na roho nzuri tu.(Hapa ndio hujasema vizuri).

Heshima, mapambano, Usichoke kutafuta, Dar lazma upate hela, hulali njaa.

Na ukitaka hao mabinti wa zuri unowasema, kunywa pombe, tokea sana sehemu za starehe utawala sana. Dar hiyo.

Na pia ukitaka Kuishi tu, uwe dalali, uwe winga, jua kujichanganya na watu, kusaidia shughuli za kila siku, usiwe na dharau, Dar hela hukosi.

Hatuna baya Dar.
 
Nimeishi mikoa msingi sana, Dar es salaam ukiwa na pesa na kazi binafsi is one of the best city to live...

Ila Dar es salaam bila pesa hapafai hata kidogo, na nikisema pesa simaanishi vihela, hapana.

Ubaya wa Dar es salaam:

1. Ukiwa mwajiriwa hapafai.
2. Kulea watoto sio pazuri.
3. Ni mji wa watu waongo ongo.
Hela kiasi gani?
 
Back
Top Bottom