Mji wa Dar es Salaam ni mishe mishe

Nakubaliana na wewe namba 2, dar sio mji mzuri kabisa kwenye malezi ya watoto.....hapafai.
 
Sana aisee
 
Watu wa mbagala tumeingiaingia vipi hapo mbona watu waliovurugwa hata mererani wapo
 
Dar kero nyingi sana. Ukiwa na hela sawa ila sasa wenye hela ni asilimia ndogo sana wengi maisha yakwaida tu.

Juzi nimeona mwanamke amebanwa kwenye mwendokasi mpaka anataka kukata roho analia tu "yesuuuuuu nakufaaaa".

Shida zote hizo za nini?
na ukimwambia aame dar huyo anakutukana kabisa..fa mchezo nini!
 
Kwamba ukiwa Masaki, Oysterbay, Mikocheni huwezi kulea watoto? Mkuu uswahilini ndio tatizo hilo lipo mm nipo Mwanza hata hapa Mwanza ukiwa Ghana, Kilimahewa, Mabatini huwezi kulea watoto masikini wana changamoto nyingi sana
 
Namba 3
 
hiyo namba 2.Adam na Hawa mbona walishindwa kulea watoto hadi wakauana. walikuwa Dar?
 
Wapo waliotoboa nje ya Dar

Kuna wengi wanang'ang'ania Dar na kupoteza muda na maisha yanawachapa

Ni ujinga tu eti niko Dar na hauna mishe ya maana kula kwa shida
Hata kama wametoboa lakini Ni lazima wafike hata kuliona jiji
 
Kwamba ukiwa Masaki, Oysterbay, Mikocheni huwezi kulea watoto? Mkuu uswahilini ndio tatizo hilo lipo mm nipo Mwanza hata hapa Mwanza ukiwa Ghana, Kilimahewa, Mabatini huwezi kulea watoto masikini wana changamoto nyingi sana

Huwezi elewa,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…