Mji wa Dar es Salaam ni mishe mishe

Thank you very much. Niliposoma hio comment na zilizofuata nilitaka kujibu kama hivi ila nikaona sitaeleweka.
 
Daslam kila mtu yuko bize ukienda sokoni ni ukitoa mguu mwingine anaweka hakuna kujuana juana inapunguza na majungu fitina umbea na uchawi
 
Dar hu mji una shida sana.
Tofauti na zamani hata mbagala kwetu hapakua hivi ila iliyokuja darlive mambo yakabadilika
Miaka ya 2014-15 tulikuwa hapo mtaa wa Nyuma ya bar ya Masakuu ilikuwa shida wanaanza kupiga mziki mida ya saa 10 jioni mpaka asubuhi halafu kuna siku walikuwa na shoo za kusaula,mziki na makelele yote unayasikia ukiwa chumbani kwako ni balaa tupu,watoto wa mitaa hiyo walikuwa wanajifunza matusi kupitia masakuu.
 
 
Dar kero nyingi sana. Ukiwa na hela sawa ila sasa wenye hela ni asilimia ndogo sana wengi maisha yakwaida tu.

Juzi nimeona mwanamke amebanwa kwenye mwendokasi mpaka anataka kukata roho analia tu "yesuuuuuu nakufaaaa".

Shida zote hizo za nini?
Huwezi kuniambia chochote kuhusu Dar ,hao wanaoishi mikoa mingine huko wao waendelee tu kuishi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…