Rais wangu pendwa 🔥John pombe joseph magufuli
Mkuu,Hapa unataka kuharibu mjadala mkuu, haina haja ya kutaja majina ya mtu ila angalia kwa kina na tafakuri kile kilichoandikwa halafu utoe mawazo yako
Kwa nini umempenda?Rais wangu pendwa 🔥
Mkuu !Mkuu,
Mimi naelewa sana umuhimu wa kufanya hoja dhahania bila kutaja majina.
Lakini pia, hata kwenye kufundisha, hoja dhahania inaanza, halafu mifano inafuatia kuiweka wazi zaidi.
Kwa hivyo majina kama JPM na Samia yanaweza kutumika kama mifano.
Kitu muhimu ni watu kujenga hoja tu kuhalalisha madai yao, na kuepuka maongezi kuingia katika kutukanana na ad hominem logical fallacies.
Kuna msemo unasema: “Mjinga akipata madaraka, cha kwanza atawanyamazisha wenye hekima; cha pili atawazungusha wajinga wenzake; na cha tatu ataanza kuharibu na kubomoa nchi.”
Ukiitazama historia ya siasa za Afrika, msemo huu una jambo la kutafakari.
Kwanza: Atawanyamazisha wenye hekima.
Kiongozi asiyejiamini katika uwezo wake huanza kuwaona watu wenye fikra huru kama tishio. Badala ya kusikiliza ushauri, anataka kusifiwa. Badala ya kukosolewa ili arekebishe makosa, anataka watu wamsifu hata anapokosea.
Hapo ndipo wasomi, waandishi, wanaharakati, wapinzani na watendaji wenye misimamo huru wanapoanza kutengwa, kudharauliwa au kunyamazishwa.
Tatizo si kwamba nchi imekosa watu wenye akili. Tatizo ni kwamba mfumo umeanza kuwaadhibu wale wanaothubutu kutumia akili zao.
Pili: Atawazungusha wajinga wenzake
Anapokuwa amewaondoa watu wanaoweza kumpa ushauri wa kweli, atajaza nafasi muhimu kwa watu wanaomwambia kile anachotaka kusikia.
Watu hawa hawapo kwa ajili ya kulinda maslahi ya taifa; mara nyingi wanalinda nafasi zao.
Matokeo yake ni serikali inayojizungumzia yenyewe, inayosifu mafanikio yake yenyewe na wakati mwingine kushindwa kuona matatizo ambayo wananchi wanayaona kila siku.
Tatu: Ataanza kubomoa nchi.
Uharibifu wa nchi hauanzii kwenye majengo kuanguka. Unaweza kuanza kwa kuanguka kwa taasisi.
Sheria inapopoteza nguvu, taasisi zinapodhoofishwa, rushwa inapokuwa kawaida, uwajibikaji unapopotea, wataalamu wanapopuuzwa na wananchi wanapoanza kuogopa kusema ukweli—hapo ndipo msingi wa taifa unapoanza kupasuka.
Na jambo la hatari zaidi ni kwamba wakati mwingine uharibifu huo hupewa jina la “maendeleo”, “utulivu”, “umoja” au “kulinda taifa.”
Afrika inapaswa kujifunza nini?
Tatizo la Afrika si ukosefu wa viongozi wenye akili pekee. Tatizo kubwa ni mifumo inayomruhusu mtu mmoja kuwa mkubwa kuliko taasisi, sheria na taifa lenyewe.
Kiongozi mzuri si yule anayezungukwa na watu wanaompigia makofi kila siku.
Kiongozi mzuri ni yule anayevumilia mtu anayemwambia:
“Hapana, hapa umekosea.”
Kwa sababu taifa haliwezi kujengwa kwa hofu, sifa na utii wa kipofu.
Taifa linajengwa kwa taasisi imara, sheria inayoheshimiwa, watu wenye uwezo, uhuru wa kutoa mawazo na viongozi wanaokubali kuwajibika.
Leo inaweza kuwa nchi nyingine.
Kesho inaweza kuwa yako.
Kwa hiyo tusijadili tu nani yuko madarakani; tujadili pia ni taasisi gani zitamzuia mtu yeyote mwenye madaraka kuibomoa nchi.
Una kazi kubwa, kwa sababu Watanzania wengi hawawezi abstract thinking.Mkuu !
Nakubaliana na hoja yako, lakini ndiyo maana nasisitiza tusianze na majina. Tukitaja viongozi mapema, mjadala wa dhana unaweza haraka kugeuka kuwa mjadala wa watu
Hoja ikisimama yenyewe bila jina, ndipo nguvu yake inapopimika. Mifano inaweza kuja baadaye kuthibitisha hoja, lakini isiwe sababu ya mjadala kupoteza mwelekeo
Lengo hapa ni kuchambua siasa na mifumo ya Afrika, sio kutafuta kasoro za mavazi au muonekano wa kiongozi fulani

Hio picha haina mchango wowote kwenye hoja ya huu mjadala, inaleta tu chokochoko na kupeleka mjadala kwenye personal attacks. Tujadili sera, mifumo, taasisi na matokeo ya uongozi sio vikaragosi
Samahani kama utakuwa umekwazika
Alitubeba sana machinga.Kwa nini umempenda?
Sawa.Alitubeba sana machinga.
Ok.Sawa.
Kiongozi kasema anapendelea tujadili hoja kwanza, si watu.
HakikaKuna msemo unasema: “Mjinga akipata madaraka, cha kwanza atawanyamazisha wenye hekima; cha pili atawazungusha wajinga wenzake; na cha tatu ataanza kuharibu na kubomoa nchi.”