Mjinga mmoja wa IT ameniulia gari langu

Okay sawa

Yule dereva wa break down naomba kujua siku ya ajali analipwa na nani, polisi?
Halipwi chochote pale .. Kumbuka ile ni ajali ni jambo la dharura ... Labda kama tu mwenye gari hatataka gari yake iende polisi au ilale polisi hapo ndio anaweza kumalizana na mwenye gari
Wao hesabu yao sio ya siku
 
Kumbe ni wewe mkuu.....hii ajali ilitokea mida ya saa 2 au 3 hivi ucku...nilikuwa natoka Dar naenda Mbeya...tulikaa hapo almost 2 hrs.
Pole mkuu
 
Pole sana mkuu. Barabarani unaweza kuwa na tahadhari zote lakini bado mzembe mwingine akakutoa roho au kukutia hasara kama hiyo.
 
Hii ni Total Loss


Kama una bima kubwa chukua mpunga wote kanunue gari mpya , usichukue Salvage.


IT hakuna madereva , hawana uzoefu na wengi ni deiwaka wanakimbiza ili warudi dar wadandie kazi nyingine
 
Hii ni Total Loss


Kama una bima kubwa chukua mpunga wote kanunue gari mpya , usichukue Salvage.


IT hakuna madereva , hawana uzoefu na wengi ni deiwaka wanakimbiza ili warudi dar wadandie kazi nyingine
Ana third party hivyo atalipwa na bima ya aliyemgonga
 
Pole mkuu kwa majanga....Vipi huyo dereva wa IT gari lake liliweza kuendelea na safaei au nalo liliishia hapo hapo..?
 
1.Kesi tayari iko mahakamani, ndio kwanza imeandikishwa hata kutajwa haijatajwa na sijui itachukua muda gani.

2.Gari ilikaa siku 2 tu kituo cha polisi Chalinze, nilipoenda kupeleka claim form na cover note ya bima yangu, mkuu wa kituo akanikomalia, kuwa pale sio gereji so nitoe mkweche wangu, nililazimika kuingia mfukoni(300k) kuchukua breakdown toka Chalinze mpaka Kibamba ninakoishi.

3.Vehicle inspector naye akataka mpunga ili aniandikie kile yeye anadai "Ripoti nzuri".

Kifupi, niko mwanzoni tu,lakini nishaanza kuona ugumu wa mchakato wenyewe! Kama kuna mtu ana uzoefu na hizi habari naomba tuwasiliane kwa msaada zaidi!
 
Kwani ni gari ya aina gani hio mkuu?
 
nilishawaii kutana na kirikuu nacho kinanianzishia ligi barabarani usiku kuchek naona ni IT... kinakimbia hatari
 
Niuzie hiyo gari niirudishe kwenye mstari
 
Exactly..... Exaaaaactly!

Mchakato wa bima na ajali ni mrefu, costly, corrupt, exploitative and stressfull!

Mshana Jr. anachukulia mambo kirahisi rahisi anatuambia hatujui mambo ya BIMA eti jamaa a-relax kwa sababu kagongwa yeye, atalipwa na bima ya yule mwingine, vipi kama yule mwingine hana bima ?

Eti beak down tow truck ni bure siku ya ajali kwa vile ajali ni dharura hakuna aliyepanga. Basi wagonjwa wangetibiwa bure na maiti zisingeshikiliwa maana hakuna aliyepanga kuumwa wala kufa.
 
Kuna mkasa kama huo ulitokea kibaha.

Gari iligongwa na canter. Wakapelekwa kituo cha polisi palepale kibaha.

Gharama za kuvuta gari zilikuja kulipwa na bima ya aliemgonga.

Kesi ikaenda mahakamani, ndani ya miezi miwili hukumu ikatoka na gari ikachukuliwa kupelekwa garage kutengenezwa.

Kiuhalisia gari haitakiwi kutolewa polisi bila hukumu ya mahakama. Maana bado kuna kesi mahakamani na huo ni ushahidi.

Unaweza kulichukua ukaliharibu zaidi na kampuni ya bima ikagoma kulipa.

Huyo polisi amekufanyia unyama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…