Mjini mipango: Wasanii wengi waliounda kundi la East coast wanaishi vizuri hadi sasa, kongole kwao kwa mikakati ya kimaendeleo

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760
Kumekuwa na makundi mengi kama Tmk wanaume, wakali kwanza, solid ground, gangwe mob, watu pori, n.k. lakini wasanii wengi waa hayo mkundi wameyumba kiuchumi hasa baada ya kuacha muziki.

Hii ni tofauti na kundi la east cost team, members wake wengi wanadunda mpaka sasa

GK - Lecturer katika chuo mojawapo cha biashara




Mwana FA - Mbunge + naibu waziri



AY - Businessman



BONUS

Lady Jay Dee - Business + kula pensheni, kuna tetesi 2025 kugombea jimbo

Hakuwa moja kwa moja mwana east coast ila tunaweza kusema alikuwa mwana east coast kivuli, alikuwa na ukaribu zaidi na kushirikiana kufanya kazi kibao na wasanii wa east coast

 
Mbona o-ten yupo tu morogoro hana mbele wala nyuma

Kwa ufupi tu dawa zimemuharibu na sasa kawa chiz
 
Jay dee hajawah kua ect. Pauline zongo choka mbaya

Oficially sio ila Indirectly JIde ni mwana East Coast sana tu, Alikuwa karibu zaidi na kafanya kazi nyingi na wana east coast

East Coast Team - Ama Zangu ama Zao

Lady Jaydee Feat Mwana FA - Wanaume Kama Mabinti
MWANA FA FT LADY JAYDEE ALIKUFA KWA NGOMA
Mwanafalsafa Ft Lady Jaydee - Hawajui
MwanaFA Feat Lady Jaydee - Msiache kuongea

AY Feat LADY JAY DEE- Machoni Kama Watu
Mawazo Lady Jay Dee
AY - Asante Feat Dela
 
Labda kwakua hukuujua utaratibubwa wa ect ndio maana ukaongea hizo.
Ngoma ni moja tuu ya lady jay dee na ect nayo ni amazangu amazao basi.

Hizo zingine ni project binafsi za wasanii hao akina fa, hazikua kaz za ect
 
Vipi pauline zongo mkuu?
 
GK amekua lini lecturer?

Unaelewa maana ya lecturer wewe?
 
GK amekua lini lecturer?

Unaelewa maana ya lecturer wewe?
Mtu yeyote mwenye gpa ya 3.5 degree anaweza kuwa mkufunzi na kibongobongo kila mkufunzi tumezoea kumuita lecturer lakini technically kuna madaraja ya Tutorial Assistant, Assistant Lecturer, Lecturer, Senior Lecturer, Associate Professor mpaka Professor.
 
GK,AY na Mwana FA hao wote mambo safi watoto wa Upanga wazee wao walikuwa na connection kwenye system so kutoboa hao kwao siyo ngumu.

Tofauti na hao TMK wengi utakuta ni watoto wa wavuvi,wafanyakazi wa wahindi na washinda masokoni.
 
GK,AY na Mwana FA hao wote mambo safi watoto wa Upanga wazee wao walikuwa na connection kwenye system so kutoboa hao kwao siyo ngumu.

Tofauti na hao TMK wengi utakuta ni watoto wa wavuvi,wafanyakazi wa wahindi na washinda masokoni.
GK ndio mtoto wa kishua wa Upanga

Ay alianza maisha Dsm kigeto geto akitokea Mbeya

Mwana Fa kwao Muheza ila itakua alikuwa na ndugu wa kufikia Dsm, alijisomesha mwenyewe chuo pale IFM licha ya kufanya vizuri kwenye muziki, alipata kazi bank ila akaiacha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…