Mjomba wangu amemtongoza mke wangu

Mjomba wangu amemtongoza mke wangu

Fidelis big

Senior Member
Joined
Aug 31, 2011
Posts
114
Reaction score
34
Naombeni ushauri wadau,nilikuwa miangaikoni nje ya mkoa ninaoishi takribani miezi miwili,nikiwa safarini siku moja mjomba(mdogo wake mama yangu tumbo moja) alikwenda arusha kikazi na huko ndo nilipomwacha mke wangu,mjomba alikwenda kuisabai familia yangu mchana ilipofika usiku akaanza kumwandikia mke wangu sms za mapenzi akamtongoza na kumwaidi kuwa endapo atampa penzi angemwambia kitu cha muhimu kuhusu mimi,wife alimkatalia na kumwambia hawazi nisaliti coz ananipenda sana,kesho yake mjomba alirudi nyumbani kwangu akaendelea kumlazimisha wife amkubalie ila alikataa katakata na kumwambia amemchukia milele na nikirudi lazima amshitaki kwangu,mjomba alipoona karata yake imegonga mwamba akabadili mada na kusema alikuwa anamtega ajue msimamo wake kama nimwaminifu kwangu! Na kumsisitiza asinieleze na afute zile sms alizomtumia. Nimerudi arusha wife amenieleza story nzima na zile sms kanionyesha ila amenisii nisimfanye chochote uncle coz ndugu zangu watamuona mchonganishi. Hivyo wadau naombeni ushauri nifanyaje?

Kama kweli mkeo alimkatalia katukatu na kama anayokuambia yote ni ya ukweli basi nampa heko huyo mkeo. Wewe usifanye chochote kwani yeye keshamaliza kila kitu (kama unayosema wewe na aliyokuambia yeye ni ya ukweli).

Na kama ni kweli basi huyo mkeo ni mfano wa kuigwa na wanawake wengine ingawa kuiga iga nayo si nzuri.

Kaka una mke wa maana sana! Katika mazingira mengi najua wanawake wengi wangekataa ila wasingewaambia waume zao, ( Hii tabia inaniudhi!) Kama mtu umekataa kweli kwanini usiseme? Eti utasikia 'niliogopa kuwagombanisha' Bull shit!...................

Na wewe mtongoze mkewe!!ngoma draw huku awana msaadawowote

Muambie uncle aache mizaa ktk mali za watu, hato rudia tena.

Jamani kuna vitu vingine vigumu! Kama mjomba alijuta na kuomba msamaha kwa mkeo kwa nini mkeo amshtaki kwako?! Si anagombanisha ndugu?!

Mimi naona alichofanya mke ni sasa kabisa (kama ni kweli, of course). Kwa nini amfiche mumewe kama anampenda kwa dhati na kama aliapa kuwa mkweli na mwaminifu kwake?

Ideally that's the kind of wife that I would want to have.

Kama kweli mkeo alimkatalia katukatu na kama anayokuambia yote ni ya ukweli basi nampa heko huyo mkeo. Wewe usifanye chochote kwani yeye keshamaliza kila kitu (kama unayosema wewe na aliyokuambia yeye ni ya ukweli).

Na kama ni kweli basi huyo mkeo ni mfano wa kuigwa na wanawake wengine ingawa kuiga iga nayo si nzuri.

<br / nyani hii ishu ni ya kweli na wife alitunza zile sms hadi niliporudi, roho inaniuma uncle anaponipigia simu huwa nashindwa kuficha hisia zangu na sijui siku nikikutana naye uso kwa uso itakuwaje! Nilikuwa namuheshimu sana na huwa tunasaidiana katika maisha yetu kama ndugu.

Jamani kuna vitu vingine vigumu! Kama mjomba alijuta na kuomba msamaha kwa mkeo kwa nini mkeo amshtaki kwako?! Si anagombanisha ndugu?!

Si unaona?

Alafu siku ikija kujulikana kuwa ulitongozwa na hukusema itakuwaje? Kwangu nitajua hukusema sababu na wewe una interest unajua siku moja unaweza kukubali au hukusema sababu unajua utamvunjia heshima mjomba kwahiyo unaogopa kumuudhi, wakati yeye amekuona 'maharage ya mbeya' ndio maana akajua akikutongoza utakubali na kwa maana hiyo kakuvunjia heshima kwanini wewe umlindie heshima?

<br / nyani hii ishu ni ya kweli na wife alitunza zile sms hadi niliporudi, roho inaniuma uncle anaponipigia simu huwa nashindwa kuficha hisia zangu na sijui siku nikikutana naye uso kwa uso itakuwaje! Nilikuwa namuheshimu sana na huwa tunasaidiana katika maisha yetu kama ndugu.

Kaka wala huna sababu ya kujisikia vibaya wala kuumia. Alichofanya mkeo ni sahihi kabisa na alichofanya mjomba wako si sahihi hata chembe. Wewe mpuuze tu na kama ana akili ataomba radhi na kuonyesha majuto ya kosa lake na kufanya ipasavyo.

Na kama mke yuko consistent na uaminifu wake kwako basi huyo mkeo ni tunu. Mtendee vyema.

<br / nyani hii ishu ni ya kweli na wife alitunza zile sms hadi niliporudi, roho inaniuma uncle anaponipigia simu huwa nashindwa kuficha hisia zangu na sijui siku nikikutana naye uso kwa uso itakuwaje! Nilikuwa namuheshimu sana na huwa tunasaidiana katika maisha yetu kama ndugu.

Roho isikuume kiongozi! Unatakiwa ufurahie akili za mkeo na uwe proud sana tu. Badala ya kukaa kimya roho inakuuma wakati hilo limjomba lako linajiona lijanjaaaaa maana linaamini mkeo hajakwambia na wala roho hailiumi. Hakikisha anajua na yeye aumie. Ningekuwa mimi ndio wewe ningejifowadia hizo msg kwenye simu yangu alafu unazifowadi tena kwa hilo jomba lako, lijue zimetoka kwenye simu yako kwa hiyo umejua kisha unaendelea na maisha kama kawaida, wala usimuulize kitu we lifowadie tu hizo msg likome

Mtongoze na wewe huyo mjomba wako bila kumuogopa tena mwambie unamzimia sana mgongo wake na kiuno chake! Mbembeleze kuwa hata suna tu, kiingie kichwa tu we utaridhika!!

mpotezee tu mjomba hajui alitendalo! mwambie tu mama kama upo karibu sana nae bt kama haupo karibu nae acha;;; n mwambiea mjomba unajua n tabia yakea ujaipenda kabsa

Jamani kuna vitu vingine vigumu! Kama mjomba alijuta na kuomba msamaha kwa mkeo kwa nini mkeo amshtaki kwako?! Si anagombanisha ndugu?!

Shem, tamaa ni kama chapa, haifutiki kirahisi moyoni, huyo mjomba mkia wa komba atakuwa anajipanga upya na anatafuta triki ya kuingia na gia nyengine na nadhani angelitafuta blackmailing advantage kama ndio next step plan yake na hapo mdada angechinjwa kiulaini na anko fyoko. Inshort mdada amefanya busara sana kumwambia mume wake na mume inabidi amkabili mjomba kigomba kistaarabu na amkanye (kama yaliosemwa hapa yote ni kweli na ndivyo yalivyo)

Naombeni ushauri wadau,nilikuwa miangaikoni nje ya mkoa ninaoishi takribani miezi miwili,nikiwa safarini siku moja mjomba(mdogo wake mama yangu tumbo moja) alikwenda arusha kikazi na huko ndo nilipomwacha mke wangu,mjomba alikwenda kuisabai familia yangu mchana ilipofika usiku akaanza kumwandikia mke wangu sms za mapenzi akamtongoza na kumwaidi kuwa endapo atampa penzi angemwambia kitu cha muhimu kuhusu mimi,wife alimkatalia na kumwambia hawazi nisaliti coz ananipenda sana,kesho yake mjomba alirudi nyumbani kwangu akaendelea kumlazimisha wife amkubalie ila alikataa katakata na kumwambia amemchukia milele na nikirudi lazima amshitaki kwangu,mjomba alipoona karata yake imegonga mwamba akabadili mada na kusema alikuwa anamtega ajue msimamo wake kama nimwaminifu kwangu! Na kumsisitiza asinieleze na afute zile sms alizomtumia. Nimerudi arusha wife amenieleza story nzima na zile sms kanionyesha ila amenisii nisimfanye chochote uncle coz ndugu zangu watamuona mchonganishi. Hivyo wadau naombeni ushauri nifanyaje?
mnh! Dunia ina majaribu hii. Nasononeka sana na hadithi za namna hii.

Nakushauri usimuulize huyo mjomba , maana mtafaruku utakaoibuka utakuwa mkubwa sana. mshukuru Mungu mkeo kakwambia kwa hiyo
hakuna baya lolote litakalotokea

inawezekana kabisa alimchomolea mjomba ila kuna ***** ***** hapo mtaan huwa anampa me hawa watu siwaamini hata kidychu

Back
Top Bottom