Fidelis big
Senior Member
- Aug 31, 2011
- 114
- 34
Naombeni ushauri wadau,nilikuwa miangaikoni nje ya mkoa ninaoishi takribani miezi miwili,nikiwa safarini siku moja mjomba(mdogo wake mama yangu tumbo moja) alikwenda arusha kikazi na huko ndo nilipomwacha mke wangu,mjomba alikwenda kuisabai familia yangu mchana ilipofika usiku akaanza kumwandikia mke wangu sms za mapenzi akamtongoza na kumwaidi kuwa endapo atampa penzi angemwambia kitu cha muhimu kuhusu mimi,wife alimkatalia na kumwambia hawazi nisaliti coz ananipenda sana,kesho yake mjomba alirudi nyumbani kwangu akaendelea kumlazimisha wife amkubalie ila alikataa katakata na kumwambia amemchukia milele na nikirudi lazima amshitaki kwangu,mjomba alipoona karata yake imegonga mwamba akabadili mada na kusema alikuwa anamtega ajue msimamo wake kama nimwaminifu kwangu! Na kumsisitiza asinieleze na afute zile sms alizomtumia. Nimerudi arusha wife amenieleza story nzima na zile sms kanionyesha ila amenisii nisimfanye chochote uncle coz ndugu zangu watamuona mchonganishi. Hivyo wadau naombeni ushauri nifanyaje?