MwanajamiiOne
Platinum Member
- Jul 24, 2008
- 10,470
- 6,580
niliwahi kuulia swali hapa zamani na sikujibiwa
je mke akisema fulani kanitongoza ina maana kashaliwa?
na kama sio lazima awe ameshaliwa,why jamii ina amini hivyo?
nakumbuka ya shyrose banji na sugu ilikuwa hivyo hivyo....
na sasa nimemsoma faizafoxy hapo juu
naanza kuamini hivyo...
The Boss inawezekana wakawa bado hawajakulana but pengine MKE hakumpenda huyo nd maana kajashtaki. Na nadhani ndio maana wengine wameuliza kama kweli ku'semea' inamaanisha uaminifu wa mke kwa mumewe, je huwa anawa'shtaki' wote wanaomtongoza ? as ile ya ......ah mume wangu kuna jikonda limenkera kama nini! linansumbua kweli kwa kunitaka! au kuna jijamaa flani liko na gari kila siku linanipaga lift pale kituoni linantongoza?!! mimi jamani sidhani kama uaminifu wa Mwanamke unapimwa na idadi ya 'kesi' za kutongozwa anazoripoti kwa mumewe, kwa sababu hatuna kipimo au measure ya kujua kama anazileta zote kwa mumewe au anakuwa selective.
Uaminifu wa mwanamke ni vile anavyoji'carry' yeye mwenyewe mbele ya jamii na ndani ya nafsi yake. Mume wangu mie atajua kuwa mie ni mwaminifu kutokana na mienendo yangu na sifa za watu wanaotuzunguka na si kwa mimi kumgeuza yeye hakimu wa wale wanitongozao ambapo hana ushahidi kamili wa as ni kweli wamenitongoza nikawakatalia au nimejirahisi kwao wakanitolea nje so kujihami asijenisemea ninamshtaki mie kwanza!
Eh mie nahisi ntapewa talaka kabla ya ndoa wallahi.!!