Mjomba wangu anataka kuchomwa akifa, familia yake imekataa kaja kwangu, Nichukue uamuzi upi??

Kama Kuna 200k nikuunganishe na jamaa mmoja wa Mara yeye ndio kazi zake. Ila pia Kuna mwingine wa 50k sema yeye hachomi vizuri sana. Na Kuna wa 1m huyu yupo dar fundi Sana wa kuchoma, anachoma mpaka unatamani kula nyama ya mtu.
 
Kifo ni fumbo la kiimani!

Je unajuaje kama yeye ndiye atakayetangulia kuonja mauti?

Yaani tayari ulishamjaji mjombao kwamba atatangulia kudanja, mbona unaidanganya sana nafsi yako?

Tayari umeshajilaani kimawazo na unaweza tangulia kufa wewe kweli.

Hakuna kitu kibaya na kitakachokuandama maisha yako yote kama kubatilisha osia wa mtu, hasa aliyekuamini na kukupenda.

Kwa kuwa gharama za kuteketeza zaweza kuwa ni kubwa, basi suala hilo mlifuatilie pamoja na yeye mwenyewe na atoe ufafanuzi wa jinsi gani maiti yake itakavyosafirishwa toka mahali atapofia, gharama za usafiri, akishachomwa majivu yahifadhiwe au yakamwagwe wapi nk nk.

Hilo la mtiririko mzima wa zoezi hilo ni muhimu kulijadili naye kwa utulivu na adabu,kisha mtafuteni wakili awasaidie kuandika osia wa kisheria.

Hii ya kusema umkubalie kwa kumzuga halafu akitangulia mbele za haki uje umzike, ni kujikaribishia laana isiyokuwa na ulazima wowote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…