Mjomba wangu anataka kuchomwa akifa, familia yake imekataa kaja kwangu, Nichukue uamuzi upi??

Mjomba wangu anataka kuchomwa akifa, familia yake imekataa kaja kwangu, Nichukue uamuzi upi??

Kama Kuna 200k nikuunganishe na jamaa mmoja wa Mara yeye ndio kazi zake. Ila pia Kuna mwingine wa 50k sema yeye hachomi vizuri sana. Na Kuna wa 1m huyu yupo dar fundi Sana wa kuchoma, anachoma mpaka unatamani kula nyama ya mtu.
 
View attachment 2028527


Kwa kipindi kama cha miaka mitatu amekuwa akiwa na msimamo wa kutaka kufanyiwa mazshi kwa kuchomwa mauti yakimkuta

Sababu zake mpaka sasa hazijaniingia akilini, yeye hataki mwili wake uoze taratibu, sijui mambo ya mwili kutumika msukule, kuhofia kwamba ataamka akizikwa [emoji23] [emoji23] n.k.

Familia yake ilikataa kwa hio kaja kwangu, kaniomba nimsaidie hio ishu na pia niende kupeperusha majivu yake kijijini sehemu aliyokuwa akiipenda utotoni.

Huduma hii ya mazishi natambua kwamba ipo hata hapa nchini, inaitwa cremation, lakini imezoeleka kwa kiasi kikubwa kutumika na wahindi wanaofata mila na tamaduni zao.

Kwa tamaduni zetu hizi za hapa kwetu na hata kwa dini, huu utaratibu haujazoeleka kiukweli, kwa hiyo hata mimi siwezi kumtekelezea anachotaka, pia hata familia yake nayo imekataa, sipendi kuanzisha taharuki.

Huwa nampaga tu sapoti ya kinafki [emoji16] maana ni mjomba tuliezoeana sana.

Je nimwambie ukweli kwamba sitaweza kutekeleza anachotaka au nimdanganye tu ili kumfurahisha ila kama kawaida maafa yakimkuta atazikwa tu kwa utaratibu wa kawaida.
Kifo ni fumbo la kiimani!

Je unajuaje kama yeye ndiye atakayetangulia kuonja mauti?

Yaani tayari ulishamjaji mjombao kwamba atatangulia kudanja, mbona unaidanganya sana nafsi yako?

Tayari umeshajilaani kimawazo na unaweza tangulia kufa wewe kweli.

Hakuna kitu kibaya na kitakachokuandama maisha yako yote kama kubatilisha osia wa mtu, hasa aliyekuamini na kukupenda.

Kwa kuwa gharama za kuteketeza zaweza kuwa ni kubwa, basi suala hilo mlifuatilie pamoja na yeye mwenyewe na atoe ufafanuzi wa jinsi gani maiti yake itakavyosafirishwa toka mahali atapofia, gharama za usafiri, akishachomwa majivu yahifadhiwe au yakamwagwe wapi nk nk.

Hilo la mtiririko mzima wa zoezi hilo ni muhimu kulijadili naye kwa utulivu na adabu,kisha mtafuteni wakili awasaidie kuandika osia wa kisheria.

Hii ya kusema umkubalie kwa kumzuga halafu akitangulia mbele za haki uje umzike, ni kujikaribishia laana isiyokuwa na ulazima wowote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom