mtafuta-maisha
JF-Expert Member
- Nov 5, 2016
- 1,982
- 2,931
Bwana Allan Swift raia wa Marekani aliyekuwa akiishi huko Massachusetts alizaliwa mwaka 1908 ma kufariki mwaka 2010, alimiliki na kuendesha gai moja kwa miaka 82.
Bwana Allan alipewa gari aina ya Rolls-Royce Phantom-P1 Roadster kutoka kwa baba yake kama zawadi ya kuhitimu masomo yake mwaka 1928.
Alilitumia gari hilo muda wote mpaka umauti ulivyomfikia akiwa na umri wa miaka 102.
Baada ya kufariki gari hilo lilitolewa wa ajili kuwekwa kwenye jumba la makumbusho la Springfield.
Ilikuwa imetembea maili 1,070,000 na ilikuwa bado inafanya kazi vizuri huku ilkiwa haina makelele hata ikiwa spidi kali yani engine yake ilikuwa bado safi kabisa.
Hapo ndipo utastaajabu maajabu ya makandarasi wa Kiingereza gari kutumika miaka 82 bila tatizo.