ESCORT 1
JF-Expert Member
- Dec 7, 2015
- 1,517
- 3,399
Leo tujikumbushe kuhusu Askofu Luwum, aliyemnyima usingizi Dikteta Iddi Amin Dada huko Uganda.
Janani Luwum alikuwa mmoja wa viongozi mashuhuri wa kidini nchini Uganda, na anaheshimiwa kama shujaa wa imani aliyejitolea maisha yake kwa ajili ya haki, amani na uadilifu katika kipindi kigumu cha utawala wa kidikteta wa Idd Amin Dada.
Jina lake kamili ni Janani Jakaliya Luwum ambapo alizaliwa mwaka 1922, Kitgum, huko Kaskazini mwa Uganda. Alifariki 16 Februari 1977, Kampala, Uganda. Alihudumu kama Askofu wa Kanisa la Anglikana nchini Uganda.
Janani Luwum aliteuliwa kuwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana nchini Uganda mwaka 1974. Alikuwa kiongozi jasiri, mcha Mungu na mwenye msimamo wa kutetea haki. Katika kipindi cha utawala wa Iddi Amin, Luwum alianza kukosoa hadharani ukiukwaji wa haki za binadamu, mauaji ya raia, na vitendo vya kikatili vilivyokuwa vinafanywa na majeshi ya serikali.
Ukosoaji wa Askofu Luwum haukumfurahisha Idd Amin na wenzake. Safari moja, Askofu Luwum aliitwa kwenye Ikulu ya Entebbe na Jenerali Isac Maliyamungu na kupewa onyo kali, aachane na siasa na ajikite kwenye dini tu. Hilo lilipuuzwa na Askofu Luwum.
Askofu Luwum akaendelea kumwaga moto, huku asijue mchoro mzima juu ya kifo chake ulishaandaliwa na Isac Malyamungu aliyekuwa mpambe mtiifu wa Idd Amin.
Alifikia hatua ya kuandika barua ya malalamiko rasmi kwa Amin, akieleza hofu ya makanisa juu ya mateso ya wananchi.
Mnamo Februari 1977, Janani Luwum alikamatwa pamoja na mawaziri wawili wa serikali kwa tuhuma za uhaini.
Luwum alikamatwa pamoja na mawaziri wawili wa serikali: Charles Oboth Ofumbi (Waziri wa Mambo ya Ndani) na Lt. Col. Erinayo Oryema (Waziri wa Usalama).
Walituhumiwa kupanga njama ya mapinduzi dhidi ya serikali. Walifikishwa mbele ya mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Idi Amin na kisha walipotezwa.
Baadaye serikali ilidai kuwa walifariki katika ajali ya gari walipojaribu kutoroka kutoka kizuizini lakini ushahidi kutoka kwa mashuhuda ulionyesha kuwa waliteswa, kisha walipigwa risasi na kuuawa na maafisa wa usalama kwa amri ya Rais Iddi Amin. Mwili wa Janani Luwum ulipatikana ukiwa na majeraha ya risasi, si ya ajali.
Waganda wakawa wamepoteza mtu muhimu anayewapazia sauti.
Tarehe 16 Februari huadhimishwa kila mwaka nchini Uganda kama Siku ya Janani Luwum, kuenzi ujasiri wake.
Sanamu yake ipo kwenye kanisa la Westminster Abbey, London, miongoni mwa mashujaa wa imani wa karne ya 20. Baadhi ya makanisa ya Anglikana yalimpa Utakatifu.
Waganda wa miaka ile wanamkumbuka Askofu Luwum kwa kauli yake maarufu;