eden kimario
JF-Expert Member
- Jun 13, 2015
- 10,356
- 16,379
Konstantino Mkuu
Konstantino Mkuu (jina kamili: Flavius Valerius Constantinus; Niš, 27 Februari 272 – İzmit, 22 Mei 337) alikuwa Kaisari wa Dola la Roma tangu mwaka 306 akitawala peke yake tangu 324.
Anakumbukwa kama mtawala aliyefaulu kumaliza kipindi cha vita vya wenyewe kwa wenyewe na kukubali Ukristo kama dini huru katika dola.
Alihamisha mji mkuu kutoka Roma kwenda Bizanti iliyoitwa baadaye Konstantinopoli.
Alivyoingia ndani ya utawala
Baba yake Constantius alikuwa mmojawapo wa makaisari wanne walioshirikiana pamoja katika utawala wa dola. Baada ya kifo cha baba jeshi lake likamtangaza Konstantino kuwa Kaisari pia, lakini bila mawasiliano na wengine. Hata hivyo alikubaliwa kama Kaisari mdogo akihusika na majimbo ya Gallia na Britania.
Mwaka 311/312 fitina kati ya makaisari ilikuwa vita na Konstantino alilenga kupanua himaya yake. Mpinzani wake alikuwa hasa Maxentius aliyekaa Italia. Konstantino aliweza kumshinda kwenye mapigano kwenye daraja la Milvio mjini Roma.
Inasemekana kabla ya mapigano hayo alipatwa na ndoto alipoona msalaba wa Yesu Kristo katika jua akasikia sauti, "Utashinda chini ya alama hii!". Baadaye vikosi vya Konstatino vilikuwa na bendera iliyoonyesha herufi za chi-rho ambazo zilimaanisha jina la "Kristo".
Ushindi huu ulimfanya Konstantino awe mkuu wa nusu ya magharibi ya Dola la Roma.
Uhuru kwa Wakristo baada ya kuuawa sana
Hadi mwaka 311 Wakristo waliteswa vikali kwa amri ya Kaisari Diokletiano. Konstatino alibadilisha siasa hii baada ya ushindi na kukubali Ukristo kwa mara ya kwanza kama dini iliyoruhusiwa rasmi, akafaulu pia kupata kibali cha Kaisari mwenzake.
Mwaka 313 alikutana na Licinius, Kaisari wa mashariki ya dola. Pamoja makaisari hao wawili walipatana kutoa tamko la Milano lililotangaza mwisho wa dhuluma dhidi ya Wakristo: "Baada ya kukutana hapa Milano sisi Kaisari Konstantino na Kaisari Licinius tumeamua kuwapa Wakristo pamoja na watu wote uhuru wa kuchagua dini yao ili Mungu wa mbinguni atupe fadhili zake."
Konstantino hakufanya Ukristo kuwa dini rasmi na yeye mwenyewe hakupokea ubatizo hadi muda mfupi kabla ya kifo chake.
Hakuna hakika kuhusu sababu zake: inajulikana ya kwamba mama yake Helena alikuwa Mkristo lakini hakuna hakika alikuwa na athira gani katika malezi ya mwanawe.
Mtawala wa pekee
Tangu mwaka 316 Konstatino alianza kugongana na kaisari mwenzake wa mashariki Liceinius baada ya huyu kuonekana anasaidia mipango ya uasi dhidi ya Konstantino. Mwaka 324 alimshinda na kumkamata akawa mtawala wa pekee.
Hapa aliamua mara moja kuhamisha mji mkuu kutoka Roma kwenda Bizanti. Alitumia pesa nyingi kwa ujenzi wake na kuitangaza rasmi mwaka 330.
Aliratibu upya utawala wa dola akaweka misingi iliyoweza kudumu kwa miaka mingi baada yake.
Hata hivyo alipaswa kutetea mipaka ya dola dhidi ya Wagermanik na dhidi ya Waajemi
Haya ni machache tu kama unajua zaidi unakaribishwa