Yaani CIA hawana elimu ya black magic? Are you serious mkuu..... Kweli hujui kuhusu project MK ultra ilivyotumia exorcism na telepathy? Je yale ni mazingaombwe. Nilishauri just google Dr Mulholland uone kitabu chake kuhusu mafunzo ya dark arts jeshini utaelewa nachokisema.
Kuhusu kiini macho sio kweli nmekupa mfano wa Mai Mai huko Ituri, kamanda wao akiwa anatembea risasi alipigwa kabisa kifuani zinapenya ila alipopanda juu ya gari na kukimbia alipopigwa kifuani akauawa. Kwahyo trick ilikua miguu ikigusa ardhi tu anakua brickwall kwa risasi kabisa.
Ambacho nashangaa kma kuna watu wanaweza potea,kutembea juu ya maji,kupaa,kuvunjaa mnyororo kwa maneno tu, kwanni mnagoma hamna anayeweza kudefy a point blank bullet?
Kwanza mkuu ni lazima uelewe hakuna jambo lolote liwe black magic or whatever linaloweza ku defy laws of Physics, inatakiwa unieleze inakuwaje baadhi ya vitu risasi hazipenyi na baadhi risasi zinapenya?? Inatakiwa unieleze inakuaje mtu huyo anapotembea ardhini risasi zisimuingie once alipopanda gari risasi ikamuingia, haya yote ni lazima yafafanuliwe ki sayansi (physics).
Mimi nasema, kama huyo mtu uliyemtaja hakuwa kavaa Bullet vest basi narudi pale pale kwamba ni wazi alipokuwa anatembea alikuwa na nguvu ya kuwafanya wapiga risasi wawe "off target", wao waliona wapo "on target" kumbe sio!!, na alipofika kwenye gari lake bila shaka gari lilikuwa halina kinga au kama ulivyosema, kitendo cha kutoa miguu ardhini hiyo kinga ikawa "nullified" na akawa exposed (akawa on target) ndipo akapigwa risasi.--- hakuna cha ajabu hapo ndugu zaidi ya hicho ninachokuambia!!!, hakuna kinga, dawa, zindiko nk, zinazoweza kuuimarisha (fortify) mwili wa mtu ukawa mgumu kuliko chuma na risasi isipenye, hakuna.
Kuna bunduki zina nguvu kubwa mara kadhaa kuliko, mfano, AK 47, G3 ambazo hizo zimeundwa kwa ajili ya kuua watu tu (bunduki za kijeshi) kuna bunduki za kuua Tembo, nyati rifles au Shot gun nk, sasa mpige mtu bunduki ya aina hiyo atakuwa salama???.
"Off target" principle ndiyo inayofanya kazi hakuna cha ajabu mkuu, msingi wa hiyo principle ndiyo msingi wa wachawi kuchukua misukule, nyinyi mnakwenda kumzika ndugu yenu mkidhani ni maiti kumbe mnaenda kuzika mgomba ndugu yenu mumemuacha hai ndani na anachukuliwa msukule, nyinyi mnakuwa mmefungwa macho (sighting power) na ndivyo hivyo walengaji wanakuwa wamefungwa macho na wanaona kitu kipo "on target" kumbe kipo "off target" na hata inawezekana huyo jamaa alipigwa na "stray bullet" kipindi anapanda gari yake.
Kwanini watu tunaweza kuona mchana na hatuwezi kuona usiku??
Macho ya binadamu yanaona vitu baada ya vitu hivyo kuakisi nuru inayogonga kwenye hivyo vitu, nuru ni nishati bila nuru macho yetu hayawezi kuona, nuru tunayoweza kuona ni ile iliyokuwa ndani ya "visible range of frequencies " maana yake ni hii kwamba vipo vitu au rangi nyingi sana hapa duniani hatuzioni sababu frequencies zake zipo beyond (ultra or infra) the range of visible frequencies, sasa waganga, Wachawi or whatever name you can call them, wanayo elimu ya kuchezea hizo frequencies kwa kutumia madawa au nguvu fulani (nguvu ya giza) inayotia macho GIZANI na mtu akashindwa kugundua uhalisia wa mambo, na hayo ndiyo huitwa mazingaombwe yamo ndani ya elimu pana sana ya Hypnotism (mesmerism).
Narudia tena HAKUNA MTU AWEZAYE KUSIMAMA MBELE YA BUNDUKI NA IFYATULIWE NA ATOKE SALAMA, na ninakuasa asije mtu na akakudanganya na ukakubali.
Risasi inatoka ikiwa na energy kubwa kuweza kupenya watu 5-6 waliojipanga in line na kuwauuwa wote kwa pamoja.