Mbowe alitetea sana uteuzi huu siku ya uzinduzi wa kampeni za chadema. Mimi nina mashaka CHADEMA kuifanyia majaribio nafasi ya Makamu wa Rais. Wana JF hebu nisadieni kuniondoa mashaka ya Makamu wa Rais huyu endapo haya hapo chini yatatokea.
Sina nia ya kubeza elimu ya mtu lakini naweza kuamini kwamba chadema walikuwa hawajiandaa kwenda kushika dola.
1. Ikitokea Rais akienda safari makamu wa Rais darasa la saba ndiye atakaimu nafasi yake
2. Endapo kiti cha Rais kitakuwa wazi kutokana na Rais kufariki dunia, kujiuzulu au kupoteza sifa za uchaguzi basi makamu wa rais ataapishwa na atakuwa Rais kwa muda uliobaki katika kipindi cha miaka mitano.
3. Makamu wa Rais huyu ndiye atakutana na viongozi na wageni wa kimataifa katika majukumu yake na kujadili masula mbalimbali yanayohitaji tafakari ya kina.
4. Endapo itaonekana kuwa Rais hawezi kumudu kazi zake kwa sababu ya maradhi ya mwili na akili basi itahesabika kwamba kiti ya Rais ki wazi, kazi na shughuli za Rais zitatekelezwa na makamu wa rais.
Je, Dr Slaa kamkubali darasa la saba ili kushika hatamu za uongozi peke yake au anahitaji mtu wa ndio mzee.
Je, jambo hili haliwezi kuathiri uchumi wetu?
Je Makamu darasa la saba ana sifa zote za kumudu changamoto za dunia ya utandawazi?