Mjue mmiliki halali wa Wasafi Tv

Mjue mmiliki halali wa Wasafi Tv

Hakuna anayemuona ni Mungu mtu sema nyie mnamchukia na kumuonea wivu kwa sababu ya mafanikio yake tu na si vinginevyo na ndio maana na sisi tunamtetea,hatuwezi kukubali mtu aliyehustle kivyake mumshushe tu kwa sababu ya chuki zenu
Nazani umenielewa sema kwa sababu ni mungu wako ndio mana unafoka sababu yake.
Kwanini asiwe Mo?(bilionea)
Kwanini asiwe Masanja au vijana wengine? Acheni kumwabudu mtu. Mtakuja kusema hata Diamond jubilee ni ya kwake pia. Au Diamond gin spirit anamiliki yeye kwa upofu mliokuwa nao wajinga ninyi.
 
Iko hivi Clouds media ni family business ambayo ipo chini ya Kussaga Family yaaani iliazishwa kupitia Fedha za Marehemu Mzee Kussaga alafu mtoto wake huyu Kussaga Jr ndio akawa mkurungezi kutokana na yeye kuwa na experience kuwa na mshiko wa kutosha akaazisha Clouds media dubai, Rwanda na kampuni zingine lakini baadae akaona kama apati pesa za kutosha kutoka Clouds media bcz ya family ownership ndio akaazisha Wasafi Media from copy and paste ya Clouds media lakini akaingia makubaliano ya mkataba na Diamond ili watumie Wasafi brand kwa minajili ya kuipa Airtime kubwa huku Diamond akipata sehemu ya kuongelea mziki wake na matamasha yake ndio maana unaona Wasafi Media wanapita mule mule kwenye njia za Clouds media mfano Kuja kwa Koffi; Koffi anamawasiliano ya Karibu sana na Joseph Kussaga pia Tigo Wanaelewana sana na Kussaga ndio maana wameweza kukaa na Clouds media for more than 4 yrs to support Fiesta. Ukiangalia hata Vifaa wanavyotumia kwenye matamasha yao ni kutoka Prime time promotion. Clouds Media ilikuwa Ruge na Joseph. Ruge ni mtendaji lakini nyuma ya picha alikuwa chini ya Kussaga ndivyo ilivyo kwa Wasafi Media Diamond anaonekana ndio mmiliki lakini nyuma ya picha yupo chini ya Joseph Kussaga kupitia Mke wake.... Vijana tutafute pesa na tuwe na focus na vision.....
Asante sana kwa ufafanuzi makini.
Huyu dogo wajanja wanatumia jina lake kupiga pesa huku wapumbavu wakiamini biashara hizo anamiliki yeye kumbe ana mchango kidogo tu mf. Diamond karanga kuna mjinga atasema ni kampuni ya Diamond pia🤪🤪
 
Kwa hiyo ktk hili la uwekezaji wewe unaona kakosea?

Au kwa mtizamo wako labda kosa lake ni miliki hisa ndogo 45% kuliko Kusaga?

Basi kama ndivyo kwa akili yako basi hata Michael Jordan atakuwa kakosea,sababu nae ktk brand ya Jordan Nike wanashare kubwa kuliko Michael Jordan.
Sijasema anakosea ila asipewe sifa ambazo sio size yake. Kila kitu yeye kila bidhaa yeye
 
Wacha nitafute Ruby mie, hayo mambo ya kampuni sijui kinyama gani, watajuana wenyewe.
 
Sijasema anakosea ila asipewe sifa ambazo sio size yake. Kila kitu yeye kila bidhaa yeye
45% sio ndogo hizo sifa anazopewa anastahili na ukitizama yeye ndio anaipromoti radio kupitia brand yake.

Diamond akiindoa jina lake hamna Wasafi Media tena,sababu kusimamisha brand sio kazi ndogo ,ila Kusaga akisema achukue hela zake watu wengine watawekeza kupitia jina la Diamond.David Mosha yule anasukuma Lamborghini ana hela chafu ila radio alichemka kuiendesha,sababu brand yake ilikuwa haijulikani.

Diamond lazima asifiwe,kwanza hana shule ya kutisha lkn anajua kutumia jina lake kuingiza hela,ndicho wanachotumia akina Jordan,Cristiano roanldo na CR7 nk.

Tanzania tulikuwa na mastaa kibao wakubwa lkn walishindwa kutumia brand zao au brand zao hawakuzitumia kibiashara zaidi mf Sir Juma Kasim "Nature" Kiroboto ni msanii mkubwa na enzi yake aliikamata game ya mziki lkn hakufanikiwa kutengeneza hela kupitia brand yake,Mr Nice alikuwa mkubwa EA yote na Takeu style yake lkn bado nae hakufanikiwa kuingiza hela kupitia brand yake nk,ndio hapo upekee wa Diamond unaponekana na ana stahili sifa,kwani hakuna mwenye hati miliki ya huu mziki leo mkali kesho unachuja ila kama una vitega uchumi endelevu vinakubeba mziki ukikukataa.Hata sasa hivi tuna wasanii wakubwa kibao ila hawajui kukuza brand zao ili ziwaingizie hela nje ya mziki wao,kidogo labda Nandy anajitahidi.

Alafu "...usiseme kila kitu yeye...." siku zote makampuni haya ongozwi na mitazamo ya hizi team za kwenye mziki,bali wao wanakusanya data na kuangalia sehemu gani wakiweka hela basi watapata faida na brand yao itaonekana na wengi,mwisho wa siku Diamond ndio anakuwa chaguo lao,hata huyo Kusaga baada ya hela yake kukaa bank hazizai kaamua kuwekeza kupitia Wasafi Media now anatengeneza profits na Diamond nae anapiga kupitia brand yake.
 
Vijana wa kileo tunapenda sanaa ushabiki bila facts.

Ila hili la nani ana miliki WASAFI TV TCRA walishalitolea ufafanuzi zamaniii (tokea 2018)

Ukifupi mmiliki wa WASAFI TV ni Kusaga..!!

Kwanini nasema hivyo?

Hebu tuingie darasani...

Ukisoma Corporate Governance vizuri inakufundisha kwamba "The majority shareholder is the owner of the company"
Hili ndilo lililoifanya Simba SC. Kumnyima 50% of the shares MO na kumpa 49.
Kwasababu siku zotee anaemiliki 50% na zaidi ndio mmiliki mkubwa na mwenye sauti (high voting power).

WASAFI TV share holders...
Who is majority shareholder?
1. Zaghalulu Ajmy (Mke wa Kusaga) = 53%
2. Nasibu Abdul Juma (Diamond) = 45%
3. Ali Khatib Dai = 2%

Then the majority share holder is 1 = mke wa kusaga = Kusaga.

Related image

Juhayna na mumewe Joseph Kusaga

Yeye ndiye mmiliki wa Prime Times Promotion na yeye ndie muandaaji wa Tamasha la fiesta.

Kwahiyo kulihamishia WASAFI TV hakuna shida.

Mahindi ya heri
Shamba la heri
Mbuzi wa heri
YOTE HERI.

Nimemaliza.

#YNWA
Huyo Ali Khatib Dai ndio nani, picha tafadhali kama unayo!
 
Kwahiyo kujua kwako marketing ndo uanze kufatiria miradi ya watu? Je wewe una mradi gani pamoja na kusoma yote hayo?
Hii ni forum ya celebs na lazima wazungumziwe kwasababu ndo kinachofanyika kwa hii forum, kama ingekuwa kuwafuatilia sio poa basi TCRA wasingeanika ile doc ya mgawanyo wa shares. Kwahiyo kumdiss jamaa kwa hilo sio sawa.
 
Mkurugenzi wa CMG Joseph Kusaga amesema yeye siyo mmiliki wala mwanzilishi wa Wasafi media.

Amezungumza hayo leo akihojiwa na XXL. Kauli hiyo imekuja kutokana na pongezi ya Adam Mchomvu nanukuu

"Kwanza boss hongera kwa kuanzisha media nyingine ya Wasafi"

Joseph Kusaga " Wasafi media siyo mimi niliyeanzisha ni Diamond Platnumz na shareholders wengine, mimi nawashauri tu wakihitaji".

Swali lingine vipi haufikirii kuwa kiongozi wa kisiasa?

Joe "Mimi siyo mwanasiasa, you can't be master of everything..."

Pia amesema hajawahi kuwa na tatizo na Lady Jaydee ashauri nao XXL wasiwe na tatizo na wengine. Wakati akitoa ushauri huo ilisikika sauti ya Adam ikisema "it's order! It's order!".

Awataka vijana kuacha chuki atoa pole kwa Babu Tale.
 
Nazani umenielewa sema kwa sababu ni mungu wako ndio mana unafoka sababu yake.
Kwanini asiwe Mo?(bilionea)
Kwanini asiwe Masanja au vijana wengine? Acheni kumwabudu mtu. Mtakuja kusema hata Diamond jubilee ni ya kwake pia. Au Diamond gin spirit anamiliki yeye kwa upofu mliokuwa nao wajinga ninyi.
Doh,nafoka tena?

Usipanic ndugu,take it easy and slow

Hivyo vingine anavyomiliki ndio kwanza napata taarifa kutoka kwako,hata nilikuwa sijui,tafuta pesa bwashee acha chuki na wivu kwa watu na usipende sana kufuatilia maisha ya waliokuzidi sana kama utakuwa na roho ya choyo kama yako,utazidi kuumiza sana roho yako bure tu,huu ni ushauri wangu kwako.Inaonekana una stress kali sana za maisha.

Halafu mkibosho gani una roho nyeusi hivyo??
 
Doh,nafoka tena?

Usipanic ndugu,take it easy and slow

Hivyo vingine anavyomiliki ndio kwanza napata taarifa kutoka kwako,hata nilikuwa sijui,tafuta pesa bwashee acha chuki na wivu kwa watu na usipende sana kufuatilia maisha ya waliokuzidi sana kama utakuwa na roho ya choyo kama yako,utazidi kuumiza sana roho yako bure tu,huu ni ushauri wangu kwako.Inaonekana una stress kali sana za maisha.

Halafu mkibosho gani una roho nyeusi hivyo??
Mimi sina mpango wa kuwa msanii kwanini nitamani kuwa kama Mond? Hakuna mifano mingine ila yeye tu. Kwanini nisije kuwa kama Mo? Endelzeni ibada yenu kwake. Kijana anajitahidi lakini bado hana sifa ambazo mnampa
 
Mimi sina mpango wa kuwa msanii kwanini nitamani kuwa kama Mond? Hakuna mifano mingine ila yeye tu. Kwanini nisije kuwa kama Mo? Endelzeni ibada yenu kwake. Kijana anajitahidi lakini bado hana sifa ambazo mnampa
Sijaongelea kuwa unatamani kuwa msanii,usiende nje ya mada,usipanic kwa sababu ya maisha mazuri ya mtu,fanya kazi,acha wivu na husda zisizokuwa na msingi,unajizibia rizki bure kwa sababu ya chuki zako,hapewi sifa,ila.maisha aliyoyapitia kama una akili timamu yanamuispire yoyote aliye na malengo,hutaki acha
 
Back
Top Bottom