Mjue mmiliki halali wa Wasafi Tv

Hakuna anayemuona ni Mungu mtu sema nyie mnamchukia na kumuonea wivu kwa sababu ya mafanikio yake tu na si vinginevyo na ndio maana na sisi tunamtetea,hatuwezi kukubali mtu aliyehustle kivyake mumshushe tu kwa sababu ya chuki zenu
Nazani umenielewa sema kwa sababu ni mungu wako ndio mana unafoka sababu yake.
Kwanini asiwe Mo?(bilionea)
Kwanini asiwe Masanja au vijana wengine? Acheni kumwabudu mtu. Mtakuja kusema hata Diamond jubilee ni ya kwake pia. Au Diamond gin spirit anamiliki yeye kwa upofu mliokuwa nao wajinga ninyi.
 
Asante sana kwa ufafanuzi makini.
Huyu dogo wajanja wanatumia jina lake kupiga pesa huku wapumbavu wakiamini biashara hizo anamiliki yeye kumbe ana mchango kidogo tu mf. Diamond karanga kuna mjinga atasema ni kampuni ya Diamond pia🤪🤪
 
Sijasema anakosea ila asipewe sifa ambazo sio size yake. Kila kitu yeye kila bidhaa yeye
 
Wacha nitafute Ruby mie, hayo mambo ya kampuni sijui kinyama gani, watajuana wenyewe.
 
Sijasema anakosea ila asipewe sifa ambazo sio size yake. Kila kitu yeye kila bidhaa yeye
45% sio ndogo hizo sifa anazopewa anastahili na ukitizama yeye ndio anaipromoti radio kupitia brand yake.

Diamond akiindoa jina lake hamna Wasafi Media tena,sababu kusimamisha brand sio kazi ndogo ,ila Kusaga akisema achukue hela zake watu wengine watawekeza kupitia jina la Diamond.David Mosha yule anasukuma Lamborghini ana hela chafu ila radio alichemka kuiendesha,sababu brand yake ilikuwa haijulikani.

Diamond lazima asifiwe,kwanza hana shule ya kutisha lkn anajua kutumia jina lake kuingiza hela,ndicho wanachotumia akina Jordan,Cristiano roanldo na CR7 nk.

Tanzania tulikuwa na mastaa kibao wakubwa lkn walishindwa kutumia brand zao au brand zao hawakuzitumia kibiashara zaidi mf Sir Juma Kasim "Nature" Kiroboto ni msanii mkubwa na enzi yake aliikamata game ya mziki lkn hakufanikiwa kutengeneza hela kupitia brand yake,Mr Nice alikuwa mkubwa EA yote na Takeu style yake lkn bado nae hakufanikiwa kuingiza hela kupitia brand yake nk,ndio hapo upekee wa Diamond unaponekana na ana stahili sifa,kwani hakuna mwenye hati miliki ya huu mziki leo mkali kesho unachuja ila kama una vitega uchumi endelevu vinakubeba mziki ukikukataa.Hata sasa hivi tuna wasanii wakubwa kibao ila hawajui kukuza brand zao ili ziwaingizie hela nje ya mziki wao,kidogo labda Nandy anajitahidi.

Alafu "...usiseme kila kitu yeye...." siku zote makampuni haya ongozwi na mitazamo ya hizi team za kwenye mziki,bali wao wanakusanya data na kuangalia sehemu gani wakiweka hela basi watapata faida na brand yao itaonekana na wengi,mwisho wa siku Diamond ndio anakuwa chaguo lao,hata huyo Kusaga baada ya hela yake kukaa bank hazizai kaamua kuwekeza kupitia Wasafi Media now anatengeneza profits na Diamond nae anapiga kupitia brand yake.
 
Huyo Ali Khatib Dai ndio nani, picha tafadhali kama unayo!
 
Kwahiyo kujua kwako marketing ndo uanze kufatiria miradi ya watu? Je wewe una mradi gani pamoja na kusoma yote hayo?
Hii ni forum ya celebs na lazima wazungumziwe kwasababu ndo kinachofanyika kwa hii forum, kama ingekuwa kuwafuatilia sio poa basi TCRA wasingeanika ile doc ya mgawanyo wa shares. Kwahiyo kumdiss jamaa kwa hilo sio sawa.
 
 
Doh,nafoka tena?

Usipanic ndugu,take it easy and slow

Hivyo vingine anavyomiliki ndio kwanza napata taarifa kutoka kwako,hata nilikuwa sijui,tafuta pesa bwashee acha chuki na wivu kwa watu na usipende sana kufuatilia maisha ya waliokuzidi sana kama utakuwa na roho ya choyo kama yako,utazidi kuumiza sana roho yako bure tu,huu ni ushauri wangu kwako.Inaonekana una stress kali sana za maisha.

Halafu mkibosho gani una roho nyeusi hivyo??
 
Mimi sina mpango wa kuwa msanii kwanini nitamani kuwa kama Mond? Hakuna mifano mingine ila yeye tu. Kwanini nisije kuwa kama Mo? Endelzeni ibada yenu kwake. Kijana anajitahidi lakini bado hana sifa ambazo mnampa
 
Mimi sina mpango wa kuwa msanii kwanini nitamani kuwa kama Mond? Hakuna mifano mingine ila yeye tu. Kwanini nisije kuwa kama Mo? Endelzeni ibada yenu kwake. Kijana anajitahidi lakini bado hana sifa ambazo mnampa
Sijaongelea kuwa unatamani kuwa msanii,usiende nje ya mada,usipanic kwa sababu ya maisha mazuri ya mtu,fanya kazi,acha wivu na husda zisizokuwa na msingi,unajizibia rizki bure kwa sababu ya chuki zako,hapewi sifa,ila.maisha aliyoyapitia kama una akili timamu yanamuispire yoyote aliye na malengo,hutaki acha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…