Tabora tumerithi integrity. Kinachoitwa maendeleo katika sehemu nyingine ni matokeo ya ufisadi na wizi, mambo ambayo yametuchangia watu wenye integrity kuonekana hatuendelei kwa vile jitihada zetu kimanedeleo zimekuwa zinauawawa na mafisadi.
Sijui sawasawa mipaka ya himaya za Milambo na Isike, ila walikuwa watemi wakubwa sana wa Tabora. Nadhani Milambo alikuwa wa Uyanyembe akiwa na makao yake upande wa magharibi wa sehemu inayojulikana leo kama Tabora Mjini wakati himaya ya Isike ikiwa upande wa mashariki wa sehemu inayojulikana leo kama Tabora Mjini. Sina uhakika sawasa kwa sasa, ila nitatafuta data zaidi kutoka kwa ndugu zangu huko Taboraili kujibu swali hili kwa ufasaha. Yeyote mwenye kujua sawasawa anaweza kutusaidia.