Mjue Mtemi Milambo wa Tabora (1840-1884)

Mjue Mtemi Milambo wa Tabora (1840-1884)

Na declare interest....mimi ni mnyanyembe...

Milambo hakuwa mtemi kama mtawala wa nchi fulani au kabila fulani..ifahamike kipindi hicho hizi tawala zilijulikana kama ni nchi au wakati mwingine kabila...ndiyo maana kwetu tuliita nchi ya unyanyembe...milambo tunaweza kumfananisha na wale walioitwa 'guerilla' kipindi kile..ndiyo maana harakati zake zilikuwa zikikata kati ya tawala fulani hadi tawala fulani...

Tukirudi katika unyanyembe..sehemu ya kwanza kutokea na kuinuka kwa unyanyembe ni Nsyepa ambapo ipo mbele kiasi kutokea itetemya kama waenda sikonge..hata hilo jina la nsyepa linatokana kisa cha mnyanyembe wa kwanza alieitwa Nyembela...watemi wote wa mwanzo walitawala na kuishi hapo nsyepa..ndiyo maana hata isike alipofariki mabaki ya mwili wake ulipelekwa kuzikwa huko baada kugundulika kuwa wajerumani walitaka kuchukua hayo mabaki kama walivyofanya kwa mkwawa.

Mtemi wa kwanza kuhamisha makazi kutoka nsyepa hadi itetemya ni mtemi Swetu katika hatua za kupanua himaya yake ambapo ilifika hadi ilipo tabora mjini leo..alitawala na akafia na kuzikwa hapo..vizazi kadhaa vya utemi vikapita mpaka alipotawala isike mwana kiyungi ambae hakuridhishwa na hatua ya wajerumani kuja kujenga ngome yao pale boma.wajerumani walijenga boma iliyokuwa ni headquarter ya germany east africa..kitendo hicho kilimkera sana isike baada ya kuona wageni wanasimika ikulu ndani ya nchi yake..kaamua kupigana nao..na hali ilipokuwa ngumu baada ya kuishiwa rasilimali silaha na wapiganaji akaona bora ajilipue yeye na familia yake ya karibu ndani ya ikulu aliyoijenga baba yake (isyunula)..mpaka wa leo kuna ukuta mmoja wenye 'arc' uliobaki baada ya mlipuko huo...
 
D
 

Attachments

  • FB_IMG_1517584960016.jpg
    FB_IMG_1517584960016.jpg
    7.8 KB · Views: 135
leo nina haki ya kujisifu kuwa nimesoma kitu na nimekipenda.. hatuna tu historia ya utumwa bali tuna historia nzuri na tamu kama hizi! nimeipenda.
tunafundishwa mahistoria yawazungu kumbe tuna tunu zimehifadhiwa!
 
napenda sana historia kama hizi, ni wazi africa tilikuwa na mashujaa...natamani zitengenezwe movie za hawa mashujaa wetu na sisi tuwe na cha kujivunia na kufundisha vizazi vijavyo,

naomba kuuliza maana nimesoma na nimekuwa nawaza kwa sauti hivi kipindi hicho cha harakati za mtemi Milambo walikua wanaongea lugha gani..!!??
 
napenda sana historia kama hizi, ni wazi africa tilikuwa na mashujaa...natamani zitengenezwe movie za hawa mashujaa wetu na sisi tuwe na cha kujivunia na kufundisha vizazi vijavyo,

naomba kuuliza maana nimesoma na nimekuwa nawaza kwa sauti hivi kipindi hicho cha harakati za mtemi Milambo walikua wanaongea lugha gani..!!??
Kinyamwezi, kisumbwa kiarabu kiswahili nk. Lugha za makabila na kiswahili mixer kiarabu
 
Tabora tumerithi integrity. Kinachoitwa maendeleo katika sehemu nyingine ni matokeo ya ufisadi na wizi, mambo ambayo yametuchangia watu wenye integrity kuonekana hatuendelei kwa vile jitihada zetu kimanedeleo zimekuwa zinauawawa na mafisadi.

Sijui sawasawa mipaka ya himaya za Milambo na Isike, ila walikuwa watemi wakubwa sana wa Tabora. Nadhani Milambo alikuwa wa Uyanyembe akiwa na makao yake upande wa magharibi wa sehemu inayojulikana leo kama Tabora Mjini wakati himaya ya Isike ikiwa upande wa mashariki wa sehemu inayojulikana leo kama Tabora Mjini. Sina uhakika sawasa kwa sasa, ila nitatafuta data zaidi kutoka kwa ndugu zangu huko Taboraili kujibu swali hili kwa ufasaha. Yeyote mwenye kujua sawasawa anaweza kutusaidia.
mzee Kichuguu una fahamu chochote, Kuhusu mtemi shomari wa tabora igunga.??
 
Back
Top Bottom