Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Kesho (Januari 25, 2021) Tanzania itampokea Mhe. Sahle-Work Zewde, Mwanadiplomasia nguli na Rais wa Ethiopia.
Mama huyu alizaliwa Jijini Addis Ababa mnamo Februari 21, 1950 na kupata elimu ya msingi na sekondari katika shule ya Lycee Gibre-Maryam na kisha akajiunga na Chuo Kikuu cha Montepillier nchini Ufaransa ambapo alisomea Sayansi Asilia (Natural Science).
Mhe. Zewde ana weledi wa lugha ya Kifaransa, KiAmhara (Amharic) na Kingereza.
KAZI ZA KIDIPLOMASIA
1989-1993:
Balozi wa Ethiopia nchini Senegal ambapo pia alikuwa akiliwakilisha nchi yake kwenye mataifa ya Mali, Guinea-Bissau, Cape Verde, Gambia na Guinea.
1993-2002:
Balozi wa Ethiopia nchini Djibouti huku akiiwakilisha Ethiopia katika Mamlaka ya Maendeleo (IGAD). Baadae aliteuliwa kuwa Balozi wa Ethiopia nchini Ufaransa.
2002-2006:
Mhe. Zewde alikuwa Mwakilishi kwenye UNESCO ambapo alifanya kazi huko Tunisia na Morocco.
Mwanadiplomasia huyu pia alikuwa Mwakilishi wa Ethiopia kwenye Umoja wa Afrika na chombo cha UN kinachoshughulikia Uchumi wa Afrika (ECA). Pamoja na vyeo hivyo, Mhe. Zewde alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mambo ya Afrika kwenye Wizara ya Mambo ya Nje ya Ethiopia.
AFANYA KAZI NA UMOJA WA MATAIFA
Mpaka 2011, Mhe. Zewde alikua ni Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa UN Mh. Ban Ki Moon pia alikua Mkuu wa Ofisi ya UN inayoshughulikia amani huko Afrika ya Kati (BINUCA).
Mwaka 2011, Ban alimteua Mhe. Zewde kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya UN Jijini Nairobi (UNON). Katika kipindi cha uongozi wake, Nairobi ikawa sehemu muhimu ya UN katika eneo la Afrika Mashariki na Kati.
Mnamo Julai 2018, Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres akamteua Mhe. Zewde kuwa Mwakilishi Maalum wa UN kwenye Umoja wa Afrika na Mkuu wa Ofisi ya UN kwenye Umoja wa Afrika (UNOAU) katika ngazi ya Under-Secretary General of the United Nation.
Ni mwanamke wa kwanza kushika nafasi hiyo nyeti Ethiopia.
RAIS WA ETHIOPIA
Mnamo Oktoba 25, 2018 Mhe. Zewde alichaguliwa na Bunge la Ethiopia kuwa Rais baada ya mtangulizi wake Mhe. Mukatu Teshome kujiuzulu kwa sababu zisizojulikana.
Mhe. Zewde anatarajiwa kuliongoza Taifa hilo kwa mihula miwili kila muhula ukiwa na miaka sita.
Mhe. Zewde ni Mwanamke wa kwanza kuwa Rais katika Taifa hilo la Ethiopia.
PIA SOMA
www.jamiiforums.com

Rais wa Ethiopia kutembelea Tanzania kwa ziara ya siku moja
Rais huyo wa nchi ya Ethiopia Mheshimiwa Sahle Work Zewde atawasili nchini kesho Januari 25, 2021 kwa ziara rasmi ya Kiserikali ya siku moja Taarifa kwa mujibu wa Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi