Mjue Rais wa Ethiopia Sahle-Work Zewde atakayeitembea Tanzania 25 January 2020

Mjue Rais wa Ethiopia Sahle-Work Zewde atakayeitembea Tanzania 25 January 2020

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Kesho (Januari 25, 2021) Tanzania itampokea Mhe. Sahle-Work Zewde, Mwanadiplomasia nguli na Rais wa Ethiopia.

Mama huyu alizaliwa Jijini Addis Ababa mnamo Februari 21, 1950 na kupata elimu ya msingi na sekondari katika shule ya Lycee Gibre-Maryam na kisha akajiunga na Chuo Kikuu cha Montepillier nchini Ufaransa ambapo alisomea Sayansi Asilia (Natural Science).

Mhe. Zewde ana weledi wa lugha ya Kifaransa, KiAmhara (Amharic) na Kingereza.

KAZI ZA KIDIPLOMASIA

1989-1993:

Balozi wa Ethiopia nchini Senegal ambapo pia alikuwa akiliwakilisha nchi yake kwenye mataifa ya Mali, Guinea-Bissau, Cape Verde, Gambia na Guinea.

1993-2002:
Balozi wa Ethiopia nchini Djibouti huku akiiwakilisha Ethiopia katika Mamlaka ya Maendeleo (IGAD). Baadae aliteuliwa kuwa Balozi wa Ethiopia nchini Ufaransa.

2002-2006:
Mhe. Zewde alikuwa Mwakilishi kwenye UNESCO ambapo alifanya kazi huko Tunisia na Morocco.

Mwanadiplomasia huyu pia alikuwa Mwakilishi wa Ethiopia kwenye Umoja wa Afrika na chombo cha UN kinachoshughulikia Uchumi wa Afrika (ECA). Pamoja na vyeo hivyo, Mhe. Zewde alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mambo ya Afrika kwenye Wizara ya Mambo ya Nje ya Ethiopia.

AFANYA KAZI NA UMOJA WA MATAIFA
Mpaka 2011, Mhe. Zewde alikua ni Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa UN Mh. Ban Ki Moon pia alikua Mkuu wa Ofisi ya UN inayoshughulikia amani huko Afrika ya Kati (BINUCA).

Mwaka 2011, Ban alimteua Mhe. Zewde kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya UN Jijini Nairobi (UNON). Katika kipindi cha uongozi wake, Nairobi ikawa sehemu muhimu ya UN katika eneo la Afrika Mashariki na Kati.

Mnamo Julai 2018, Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres akamteua Mhe. Zewde kuwa Mwakilishi Maalum wa UN kwenye Umoja wa Afrika na Mkuu wa Ofisi ya UN kwenye Umoja wa Afrika (UNOAU) katika ngazi ya Under-Secretary General of the United Nation.

Ni mwanamke wa kwanza kushika nafasi hiyo nyeti Ethiopia.

RAIS WA ETHIOPIA
Mnamo Oktoba 25, 2018 Mhe. Zewde alichaguliwa na Bunge la Ethiopia kuwa Rais baada ya mtangulizi wake Mhe. Mukatu Teshome kujiuzulu kwa sababu zisizojulikana.

Mhe. Zewde anatarajiwa kuliongoza Taifa hilo kwa mihula miwili kila muhula ukiwa na miaka sita.

Mhe. Zewde ni Mwanamke wa kwanza kuwa Rais katika Taifa hilo la Ethiopia.

PIA SOMA

 
Mhe. Zewde ana weledi wa lugha ya Kifaransa, KiAmhara (Amharic) na Kingereza.
Nyongeza ni kuwa huyu Rais wa Ethiopia pia anaongea lugha ya Kiswahili.

Mwaka 2011 - 2018 alihudumu ktk Ofisi ya Umoja wa Mataifa iliyo Kitovu cha kuhudumia Mashirika ya UN yenye makao yake jijini Nairobi, Kenya kama ofisa wa ngazi ya Juu wa Umoja wa Mataifa.
 
Naomba kujuzwa huyu ki mamlaka nchinu Ethiopia yukoje, maana anayesikaka sana ni waziri mkuu.
Ethiopia wanatumia Mfumo wa uongozi kama wa India, Ujerumani, Israel nk ambapo Rais anakuwa Mkuu wa Nchi tu kwa hiyo cheo chake ni cha heshima (Ceremonial) tu, Serikali inaongozwa na Waziri Mkuu ambaye anaunda Baraza la Mawaziri na anatokana na Chama chenye Wabunge wengi Bungeni.

Mfumo wa kwetu ambao haufai kabisa, Rais ndio kiongozi wa Nchi na Serikali akisaidiwa na Makamu ambaye ni Rais mtarajiwa endapo Mungu atampenda zaidi Rais akiwa madarakani. Rais ndiye anateua Mawaziri na Waziri Mkuu ambao lazima wawe Wabunge na ndio wanaunda Baraza la Mawaziri na Waziri Mkuu akiwa Mkuu wao na kiongozi wa shughuli za Serikali Bungeni.

Rais wa kwetu ndo pia anateua watumishi wote muhimu Serikalini na Mashirika ya Umma ndio maana nchi ikipata Rais dhaifu mambo mengi yanakwama kwa sababu wateule ni wengi mno kwa mtu mmoja kufuatilia utendaji kazi wao. Pamoja na kuwa ni wajibu wa mteuwa kuteua na kutengua (hire & fire), lakini teua/tengua zikizidi unakuwa ni uthitisho wa udhaifu wa mteuwa.
 
Huyu si ni ceremonial president, mwenye madaraka ni PM au nakosea.
 
Abiy Ahmed ambaye ndio Prime minister wa Ethiopia ana nguvu zaidi kimamlaka kuliko huyu President Sahle-Work Zewde.
 
" Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja" Ahadi ya 1 Mwana TANU.Natamani Rais wetu abatilishe baadhi sheria uhamiaji tulizo copy kwa Wazungu, dhidi ya madhila ndugu zetu wa Ethiopia na Somalia wanaopita njia kujitafutia riziki. Tunapoteza kipato utalii wa ndani pia wangeweka ada kidogo na kibali mpakani, boda. Mh. Kabudi amkumbushe mzee Baba kwa hili tuwe na utu na kufufua ndoto za Africa moja.
 
ZEWDE NDIYE RAIS WA KWANZA MWANAMKE NCHINI ETHIOPIA. JE UTAWALA WAO UKOJE?

Na Elius Ndabila
0768239284

Leo Tanzania itapokea ugeni mzito kutoka Ethiopia. Taarifa iliyotolewa Jana na Waziri wa Afrika Mashariki Mh Prof Kabudi alisema Rais wa Bi Zewde wa Ethiopia atatua leo nchini akipokelewa na Mwenyeji wake Rais wa Tanzania. Alisema Rais huyo atapokelewa Chato Mkoani geita kutokana na mwaliko wa mwenyeji wake. Katika makala hii nitajaribu kumuangazia Rais huyu wa Ethiopia ambaye ni mwanadiplomasia mkubwa Afrika.

Nchi ya Ethiopia inapatikana kasikazini Magharibi mwa bara la Afrika. Inazungukwa na nchi za Sudani na Sudani kusini kwa upande wa Magharibi, Eritrie na Jibuti upande wa kask, Somalia upande wa Mashariki na Kenya upande wa kusini. Ethiopia ni miongoni mwa nchi mbili barani Afrika zinazoandikwa Kuwa hazikutawaliwa na ukoloni. Idadi ya watu wake ni 109,223,404.

Tunapouangazia utawala wa Ethiopia, pia tunajaribu kuonyesha nguvu ya Rais Zewde katika nchi yake. Ninaamini watu wengi hawamfahamu ijapo umaarufu wake ni mkubwa Afrika na Duniani kwa ujumla.

Huyu ni rais wa kwanza mwanamke nchini Ethiopia na Rais wa tano kwa bara la Afrika akitanguliwa na Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia, Jocy Banda wa Malawi, Saara Kuugongelwa-Amadhila wa Namibia na Ameenah Gurib- Fakim wa Mauritius. Ni sehemu ya Wanawake wanaojibu kwa vitendo juu ya ubora wa demokrasia ya Afrika. Mh Sahle si Rais tu wavEthiopia bali ni mama aliyepikwa vizuri kwenye diplomasia. Website ya serikali ya Ethiopia inamtaja Kama mwanamke wa Pili kuteuliwa kuwa balozi kuwakilisha nchi hiyo.

Bunge la Ethiopia lilimchagua Sahle-Work Zewde kuwa rais wa kwanza mwanamke wa nchi hiyo. Kuchaguliwa kwake katika wadhifa huo, kunafuatia kuteuliwa kwa baraza la mawaziri lenye idadi sawa ya wanaume na wanawake. Kwa dhana hiyo tunaweza kuitaja Ethiopia kuwa mfumo wa 50/50 ambao huku kwetu ulipiganiwa sana na Mama Mongera na wenzake kule Ethiopia wanaupractice kama ilivyo kwa Rwanda na Ushelisheli.

Sahle-Work Zewde ambaye ni mwanadiplomasia wa muda mrefu, alichukuwa nafasi ya Mulatu Teshome ambaye alijiuzulu wadhifa wa urais ambao nchini Ethiopia ni wa heshima tu, si kama huu wa nchi yetu ambao hupitia michakato mingi. Kwa mujibu wa katiba ya Ethiopia , rais hana nguvu ikilinganishwa na wadhifa wa waziri mkuu ambaye yeye ndiye, aliye na nguvu za kisiasa nchini, nafasi ya Rais ni Ceremonial. Ethiopia inaongozwa na waziri mkuu Abiy Ahmed ambaye kwa kiasi kikubwa amejitahidi kudhibiti vita vya ukabila. Katiba ya Ethiopia ya mwaka 1995 imewekeza nguvu zote za kisiasa na kiutendaji kwa Waziri Mkuu. Hivyo, kiuhalisia, Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Bw Abiy Ahmed ananguvu zaidi ya Rais wake Bi Zewde. Ahmed ni mkuu wa serikali na Zewde ni mkuu wa nchi. Hivyo power of decisions making inafanywa na Waziri Mkuu.

Ethipoia si nchi pekee yenye mfumo kama huo. Mauritius ni nchi nyingine ya Afrika inayotumia mfumo huo. Duniani baadhi ya nchi zenye mfumo kama huo ni India, Ujerumani, Italia na Israeli. Kiongozi mkuu anayefahamika zaidi wa Ujerumani ni Kansela Angela Markel na yeye ndiye mwenye mamlaka ya kuongoza serikali. Rais wa Ujerumani ambaye wengi nje ya nchi hiyo wanaweza kuwa hawajahi kumskia anaitwa Frank-Walter Steinmeier.Kwa upande wa India mwenye mamlaka ya kiutendaji na maamuzi ya kiserikali ni Waziri Mkuu Narendra Modi. Rais wa India anaitwa Ram Nath Kovind. Kwa upande wa Israeli mwenye hatamu za kuingoza serikali ni Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu. Rais wa nchi hiyo ni Reuven Rivlin.

Katika mfumo huo, miongoni mwa kazi za rais ambaye ni mkuu wa nchi ni kuishauri serikali inayoongozwa na Waziri Mkuu na baraza la mawaziri. Kutangaza hali ya vita baada ya kushauriwa na bunge, kupokea hati za mabalozi wa kigeni, kuitisha uchaguzi na kutaja jina la mshindi wa uwaziri mkuu. Rais pia hukubali na kutangaza kujiuzulu kwa waziri mkuu na serikali pale hali hiyo inapotokea. Kwa baadhi ya nchi zenye mfumo wa kifalme, cheo na madaraka ya rais wa Ethipoia huwa ni ya Malkia ama Mfalme. Mfano mzuri ni Uingereza ambapo malkia Elizabeth ni mkuu wa nchi na Waziri Mkuu Bi Theresa May ni kiongozi wa serikali na hivyo mamlaka yote ya kiutawala wa dola yapo chini yake.

Tanganyika ilipopata uhuru mwaka 1961, Mwalimu Julius Nyerere alikuwa Waziri Mkuu na kiongozi wa serikali. Mkuu wa nchi alikuwa Malkia Elizabeth wa Uingereza. Januari 22, 1962 Nyerere alijiuzulu wadhifa huo na Rashidi Kawawa kuchukua nafasi yake. Mabadiliko ya katiba ikaifanya Tanganyika kuwa Jamuhuri Desemba 9,1962 na Nyerere kuwa Rais. Malkia wa Uingereza akakoma kuwa mkuu wa nchi ya Tanganyika.

Ethiopia ilikuwa ni nchi ya mfumo dume, ujio wa mwanadiplomasia huyu nguli uliweka Ethiopia kwenye ramani mpya. Ifahamike mwana Mama huyu alitajwa na gazeti la Forbes mwaka 2012 kwa kushika nafasi ya 96 kwa watu mashuhuri duniani na nafasi ya kwanza kwa Afrika.Wanawake wa Ethiopia wanamuona kama ndiye mtetezi wao na amekuja maalumu kwa kuijenga upya Ethiopia ambayo ilikuwa ikitawaliwa kwa mfumo dume.

Mtangulizi wa Sahle-Work katika nafasi ya rais Mulatu Teshome Wirtu ambaye alihudumu kwa miaka 5, alijiuzulu ukisalia mwaka mmoja kabla ya kumaliza muhula wake, akisema anataka kuchangia katika mabadiliko yaliyokuwa yakiendelea nchini humo.Baadhi ya wachambuzi walisema kujiuzulu kwake kunaweza kuwa na malengo ya kuweka urari wa kikabila, kwa sababu alikuwa anatoka jamii ya Oromo kama alivyo waziri mkuu Abiy Ahmed.

Bi Sahle-Work ni wa nne katika wadhifa huo tangu mseto wa vyama wa EPRDF ulipoingia madarakani mwaka 1988, kufuatia ushindi katika vita vya wenyewe kwa wenyewe, Lakini ni Mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo.

Ni mwanaplomasia wa muda mrefu, akiwa ameiwakilisha nchi yake katika nchi za Ufaransa, Djibouti, Senegal na katika Jumuiya ya Ushirikiano ya nchi za Upembe wa Afrika, IGAD. Akiwa anachaguliwa Bi Sahle-Work Zewde alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, na mjumbe maalumu wa Katibu mkuu wa umoja huo katika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa.

Kwa mkutadha huu ni dhahiri Kuwa ujio wa Bi Zewde nchini Ethiopia ulikuwa na maana kubwa hasa ya kuhakikisha Kuwa Ethiopia inatulia na kuondoa mifumo kandamizi. Pamoja na hayo bado Uchumi wa Ethiopia haujatulia na Mara kwa Mara tumeona Raia wake wakikimbilia Afrika kusini. Lakini idadi hii kubwa ya watu wa Ethiopia inaweza kutumika Kama fursa kwa Tanzania kufanya biashara nao kwani population yao ni zaidi ya mara mbili ya Tanzania.
 
Nadhani suala demokrasia halitajadiliwa. mwanzoni utawala awamu 5 mifano ilikuwa Ethiopia tu ukusanyaji kodi , centralization mifumobyote, serikali kuhodhi kila kitu ikiwemo biashara, PPP ilikuwapo sasa imefutwa huko lakini ghafla dunia inakimbia zaidi ya muda, sasa wanaita wawekezaji sekta zote ikiwemo telecom ambapo malaika alisema telecom yao inatoa $1bil mwaka gawio kwa serikali, ndio ilikuwa benchmark bila kujali hapa Tanzania telecom zimefanya nini na zitafanya nini miaka ijayo ajira, kodi, uwekezaji etc sasa sijui wataongea nini zaidi Nina wasi wasi wanapotezeana muda. Kuna MTU anataka arudi wenzako wanakotoka!
 
Malkia wa Shaba alimtembelea mfalme Solomon alimpelekea zawadi za vito vyenye gharama kubwa.

Inasemekana mfalme alimtunuku malkia zawadi ya ujauzito.

Ukisoma maandiko kadhaa huyo kijana mwana wa mfalme miaka fulani alienda kumtembelea babaye, wakati huo Solomon akiwa mzee wa miaka mingi.

Kijana alikwapua lile sanduku la agano la Mungu akarejea kwao Ethiopia, mwisho akafanya utalii Tanzania na lile sanduku akaliacha Tanzania,

Ndiyo hivyo, unabisha nini, niambie wewe

Karibu nyumbani mgeni wetu.
 
Nimesoma mpaka nikakuta sentensi kuwa WAZIRI MKUU WA UINGEREZA ni THERESA MAY!, Hapo nikapumzika kwanza. Ku-rewind akili yangu kwanza.
 
Wewe bila shaka hata mkeo humkubali kabisa.

Hii ethiopia ndio huwa mfano mbovu kwa tanzania na umasikini wake, japo ina mandege kibao.

Ifike hatua tujue tatizo letu la msingi na ni kipi hasa tunahitaji.
 
" Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja" Ahadi ya 1 Mwana TANU.Natamani Rais wetu abatilishe baadhi sheria uhamiaji tulizo copy kwa Wazungu, dhidi ya madhila ndugu zetu wa Ethiopia na Somalia wanaopita njia kujitafutia riziki. Tunapoteza kipato utalii wa ndani pia wangeweka ada kidogo na kibali mpakani,boda.Mh.Kabudi amkumbushe mzee Baba kwa hili tuwe na utu na kufufua ndoto za Africa moja.
Africa moja inawezekana majukwaani na sio kiuhalisia sababu ya ubinafsi.nchi na nchi tu jirani haziwezi ungana sembuse afrika nzima.
 
Historia ya mama imetukuka huoni hata sehemu moja alihamasisha upumbavu!
 
Nyongeza ni kuwa huyu Rais wa Ethiopia pia anaongea lugha ya Kiswahili.

Mwaka 2011 - 2018 alihudumu ktk Ofisi ya Umoja wa Mataifa iliyo Kitovu cha kuhudumia Mashirika ya UN yenye makao yake jijini Nairobi, Kenya kama ofisa wa ngazi ya Juu wa Umoja wa Mataifa.
Isije akawa anajua kusema mambo, habari gani, halafu kafika mwisho
 
Tungekuwa na mfumo Kama wa ethiopia huyu akupaswa kabisa kuwa hapo juu angeishia u PM angalau tusingeharibikiwa hivi juu panahitaji reasoning capacity.
 
Back
Top Bottom