Mjue Raisi wa Croatia mama Kolinda Grabar.

Mjue Raisi wa Croatia mama Kolinda Grabar.

radika

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2014
Posts
20,440
Reaction score
32,260
World Cup imemalizika na moja kati ya mambo yaliyovuta hisia za wengi ni Rais wa Croatia Mwanamama Kolinda Grabar. Wengi tumezoea kuona Rais akilindwa na walinzi lukuki lakini hali ni tofauti kwa Mwanamama Kolinda.

Baadhi ya Picha zake pia zimezua utata mwingi hata kuna video zikimuonyesha akiwakumbatia mashujaa wa Croatia walioloa jasho baada ya mechi kumalizika wengi wanajiuliza inawezekana vipi kwa Rais huyu Mwanamama kufanya yote haya? Kolinda Grabar mwanasiasa na mwanadiplomasia wa Croatia kwa muda mrefu sana amefanya historia yake ya uongozi kukumbukwa zaidi katika World Cup ya mwaka 2018 zilizofanyika nchi Russia.

Lakini leo nakugusia mambo usiyo yafahamu kutoka kwa Rais huyu.

1. Ni Rais mwenye umri mdogo kuchaguliwa Croatia kulinganisha na viongozi waliopita.

2. Ni Mwanamke wa kwanza kushika nyadhifa ya Urais katika nchi ya Croatia tangu wimbi la vyama vingi lilipoanza mwaka 1990.

3. Ni Mwanajeshi Commando mstaafu ambaye aliwahi kushika nafasi ya Naibu katibu Mkuu wa umoja wa Majeshi ya kujihami kwa nchi za Magharibi NATO (Haingiliki kirahisi si mtu wa mchezo mchezo unaambiwa kina cha bahari hakipimwi kwa kijiti)

4. Aliwahi kuwa balozi wa Croatia nchi Marekani mwaka 2007 -2011

5. Ni ACE Marksman Commando brigade unaambiwa akishika silaha hakosei pale anapolenga kama atapiga kichwa Sawa kama amelenga taya hakosi (Ina maana kuwa ni mtu wa Target kama mpo thelathi wote anawalaza chini)

Rais Kolinda enzi za kutumikia jeshi alikuwa ni mtu mwenye kupenda kuwatia Moyo wapiganaji hii ndiyo maana aliamua yeye mwenyewe kwenda nchi Russia kuwatia moyo wachezaji wa Taifa hilo katika michuano ya kombe la Dunia.
Chanzo kutoka mitandao mbalimbali.
FB_IMG_1531921751270.jpg
FB_IMG_1531921745709.jpg
FB_IMG_1531921739970.jpg
FB_IMG_1531921731623.jpg
 
Mbona mnasahau kuweka vitu muhimu?
Ameolewa, ana watoto..n.k

Lakini hii ni moja ya tukio muhimu sana kwenye kampeni zake zijazo endapo anampango wa kugombea tena urais.

Michezo huwaunganisha watu wa aina zote bila kujali vyama.
 
Mtoa mada unatudanganya sana huyo mama hajawahi kuwa mwanajeshi kabisa tena umeita comandoo....hajawahi na ameolewa Jacov Kitarovic na kuzaa watoto wawili Katarina na Luka
 
Hiyo taarifa kuwa huyo dada amewahi kuwa mwanajeshi komando na mlenga shabaha umeitoa wapi? Nina wasiwasi unatulisha matango pori maana taarifa nilizonazo ni kuwa hajapata kufanya kazi jeshini kama mwanajeshi maana hata huko NATO alikuwepo kama mwanadiplomasia tu
 
Mtoa mada unatudanganya sana huyo mama hajawahi kuwa mwanajeshi kabisa tena umeita comandoo....hajawahi na ameolewa Jacov Kitarovic na kuzaa watoto wawili Katarina na Luka
SIX THINGS YOU DIDN’T KNOW ABOUT CROATIAN PRESIDENT (SHE’S A COMMANDO)
















WhatsApp-Image-2018-07-18-at-10.56.31-524x350.jpg
Croatian President Kolinda Grabar Kitarovic is an army commando. PHOTO | COURTSEY
By NAHASHON MUSUNGU
Football fans who watched Croatian President Kolinda Grabar Kitarovic at the 2018 Fifa World Cup were struck by her beauty, affectionate smile and selfless support for her national team.

But what else is there to know about the Head of State, who arguably turned out to be the biggest celebrity outside the pitch during the football tournament in Russia?

Here are six things to know about the Croatian President.

1. She was born in Rijeka, Croatia, which was then part of the greater Yugoslavia. Her parents owned a butcher shop and a ranch.

2. A perfect example of ‘beauty and brains’. She studied at George Washington University, Harvard and John Hopkins University in the United States. She graduated with a degree in International Relations and a doctorate in the same.

3. She became the first woman to be the Nato Assistant Secretary General for public diplomacy. In Nato circles, she is known as SWAMBO which implies she who must be obeyed. She also boasts of full military training in her native country and is known to be a no-nonsense woman and a bold decision maker.

WhatsApp-Image-2018-07-18-at-10.56.13.jpg


WhatsApp-Image-2018-07-18-at-10.56.53.jpg


4. Look away stalkers and admirers. Madam President is married to Jakov Kitarovic. They got married in 1996 and the couple has two kids Katarina and Luca.

5. She served as the Croatian ambassador to the United States during the regimes of George W. Bush and Barack Obama.

6. While our lawmakers were banking on tax payers money to head to Russia for the bench marking trip, Kitarovic bought her own economy class ticket and travelled to Russia to cheer on the Croatia national team. She was often spotted mingling with spectators and hugging sweaty players in the dressing room.
 
Back
Top Bottom