Mjukuu anaweza kupata mirathi kutoka kwa wazee wake bila maandishi?

Mjukuu anaweza kupata mirathi kutoka kwa wazee wake bila maandishi?

Wizo2024

New Member
Joined
Aug 11, 2024
Posts
2
Reaction score
5
Mimi Nina Rafiki yangu amefarikiwa na mama yake muda mrefu sasa na babu na bibi yake pia wamefariki karibuni vip anaweza pata miradhi kwa kupitia mama yake, Babu na bibi hawakuacha maandishi yoyote.
 
Mimi Nina Rafiki yangu amefarikiwa na mama yake muda mrefu sasa na babu na bibi yake pia wamefariki karibuni vip anaweza pata miradhi kwa kupitia mama yake, Babu na bibi hawakuacha maandishi yoyote.
Wosia wa marehemu unasemaje
 
aliyeteuliwa kuwa msimamiz wa mirathi ni nan? kama yupo nenda kaone kama amewaweka na nyie kama wanufaika mtarith kupitia mama yenu.na kama hajawaweka andika barua ya pingamizi kwenda kwa hakim mfawidhi elezea sababu.kama haitoshi omba wewe kuwa msimamiz wa mirathi na usimamie. kwa sasa nan aliyebaki?
 
Arithi kwa babu na bibi??
Mama alirithi nini au alikua na nini cha kurithi?
Au nae ndo alikua anatumia vitu vya babu na bibi mpaka kufa kwake??
 
Mimi Nina Rafiki yangu amefarikiwa na mama yake muda mrefu sasa na babu na bibi yake pia wamefariki karibuni vip anaweza pata miradhi kwa kupitia mama yake, Babu na bibi hawakuacha maandishi yoyote.
Mjukuu Anaweza kabisa kupata gawio la mirathi kwa kupitia wazazi wake hata kama wamefariki kabla ya babu na Bibi.
 
Mirathi hugawiwa watoto sio wajukuu, hapo labda kuwe na wosia tofayti na hapo hakuna sheri ya ninyi wajukuu kurithi hata kama ni watoto wa kiumeni, yaaani huyo babu yenu ni mzaaa baba ninyi hamna nguvu ya kurith mali
 
Mimi Nina Rafiki yangu amefarikiwa na mama yake muda mrefu sasa na babu na bibi yake pia wamefariki karibuni vip anaweza pata miradhi kwa kupitia mama yake, Babu na bibi hawakuacha maandishi yoyote.
Labda itembee dhulma na tamaa ya mali ya kutisha, lakini mgao wake upo pale pale hata bila ya maandishi.

Iko hivii, mjukuu ni kizazi cha pili hawezi kumrithi babu yake moja kwa moja.

Lakini kwa kisa hiki, mjukuu anarithi, kwa sababu kuna fungu la mirathi ya marehemu mama yake hapo katika mgao wa mirathi ya watoto wa marehemu babu yake.

Ndugu watakapokaa kugawa mali za marehemu babu yake, kutakuwa na fungu la mirathi ya marehemu mama yake.

Kama wazawa wa tumbo la mama yake ni wengi, baada ya mgao wa mirathi ya babu yao kwa wanaye kukamilika, itabidi wakae kikao cha kugawana fungu hilo la mirathi ya marehemu mama yao.

Na kama atakuwa mzawa pekee katika tumbo la mama yake, fungu la mgao wa marehemu mama yake atapokea yeye kwa niaba.
 
Hakuna kitu kama hicho, mama yake alipokufa kabla ya wazazi wakati automatically urithi wake ulifutika, watarithi watoto kama wapo na sio wajukuu
Wapi huko wanafanya hivyo mkuu?

Mgao wa mirathi ya marehemu mama yake ungelifutika iwapo angelikuwa hana mtoto.

Lakini kwa issue hii mgao wake upo na utakwenda kwa mwanaye/wanaye.
 
Wapi huko wanafanya hivyo mkuu?

Mgao wa mirathi ya marehemu mama yake ungelifutika iwapo angelikuwa hana mtoto.

Lakini kwa issue hii mgao wake upo na utakwenda kwa mwanaye/wanaye.
Naongelea sheria hapa siongelei mazoea wanayofanya watu
 
Naongelea sheria hapa siongelei mazoea wanayofanya watu
Sheria ipi hiyo mkuu? Kwa sheria ya Tanzania, ukiondoa kama familia haitachagua Mila au dini ya kiislam, basi mjukuu atarithi kupitia mzazi wake.
Pia mjukuu kama moja kwa moja aliishi na Bibi na babu yake na akasaidia kazi na biashara zako, basi Anaweza kurithi moja kwa moja bila kutegemea mzazi.
Unayoongelea wewe ndiyo yanaitwa "mazoea"
 
Acha ubishi leta kifungu iwe Cha sheria za kimila, za kiislamu au serikali inayomtambua mjukuu katika urithi, ukileta nakutumia 50k nisipofanya hivo tag mods wote nipigwe ban hata mwezi
 
Acha ubishi leta kifungu iwe Cha sheria za kimila, za kiislamu au serikali inayomtambua mjukuu katika urithi, ukileta nakutumia 50k nisipofanya hivo tag mods wote nipigwe ban hata mwezi
Indian Succession Act,1925 Section 40(2)(iii) and (iv).
As applied in Judicature and Application of Laws Act 1920.
 
Sheria ipi hiyo mkuu? Kwa sheria ya Tanzania, ukiondoa kama familia haitachagua Mila au dini ya kiislam, basi mjukuu atarithi kupitia mzazi wake.
Pia mjukuu kama moja kwa moja aliishi na Bibi na babu yake na akasaidia kazi na biashara zako, basi Anaweza kurithi moja kwa moja bila kutegemea mzazi.
Unayoongelea wewe ndiyo yanaitwa "mazoea"
na watu wengi naona wana sema mohamedan law ooh mjukuu harithi mjukuu harithi. nani aliwaambia.?? kwenye islamic law kuna makundi maalum yanayopata urithi kwa upande wa wanaume yapo 10 kwa wanawake yapo 15. na ishu ya mjukuu naweza kusema mjukuu yupo katika kundi la wanaostahik kupata mgao isipokuwa hawana fungu maalum.ni sheria ndefu kidogo kwa mfano katika marehem lets say babu kafa kaacha watoto wawili mmoja wa kike mmoja wa kiume na watoto wa marehem mwanae aliyefariki labda miaka mingi iliyopita i.e wajukuu. hapa wajukuuu wa huyu babu watazuiwa kurithi sababu liyowazuia ni kuwepo kwa huyu mtoto wa kiume wa babu.ila kwa mfano ingekuwa kabak mtoto mmoja wa kike na hawa grandchildren bas nusu ya mali ni ya huyu mtoto wa kike na nusu inaenda kwa ndugu wa karibu wa babu.sasa hapo ndio wataangaliwa kaka zake,shangaz zake baba zake wadogo, wakubwa.na hapa ni kama wajukuu baba yao alitangulia. ikiwa babu yao alifariki wanaingia moja kwa moja kwenye mirathi sabab wanarith alichopaswa kurithi baba yao na vizaz vyake na itaenda mpaka kwa vilembwe vinyingina mpaka vitukuu.nashangaa sana wanaropokwa watu bila kuchimba elimu na masheh sijui hawamo JF wawe wanazidefend accusation kama hizi.
kifupi mtoa mada nenda katafute locus stand. uwe na msingi wa madai yako na omba kisheria uwe msimamiz wa mirathi nenda kam rebovate huyo.msimamiz mlafi. na hata kwenye uislam babu kibusara alipaswa kuwapa nyie wajukuu kwa kuacha wosia ⅓ ya mali yake.isizidi ⅓ maana utakua umepunja warithi. eeh musijifiche kwneye sheria mukawa mnakula mali ya watu kwa mungu kuna moto
 
Back
Top Bottom