Mirathi kwa Tanzania zina utata sana, kwa kuwa zinaendeshwa kwa sheria tatu kama siyo nne tofauti.
Kuna sheria za Kiislam. Waislam hawafati sheria za nchi au mila na desturi mpaka ithibitike kuwa walijitowa kwenye Uislam.
Kiislam mirathi wala haina tatizo, imeshainishwa wazi kabisa kwenye Qur'an. nani warithi na vipi mali inawsanywe.
Kwanza kabisa Kiidslam, mtu anapokufa, mali yake imzike. Siyo kufanyiwa michango ya kitapeli.
Pili, mali yake ilipe madeni yake yoyote aliyoyaacha marehemu.
Kinachobaki ikiwa ni mali au madeni basi vigawanyishwe kwa mujibu wa Qur'an.
Mjukuu hamrithi babu wala bibi ka,a wameacha watoto n warithi wengine wanaokubalika.
Ikiwa babu au bibi aliwacha wposia, apewe mjukuu, basi hata kama alisema apewe zote, hatopeewa zqaidi ya ya moja ya tatu ya alivyowacha marehemu. Na hii ni kwa wote wanaoachiwa wosia, siyo kwa mjukuu tu.
Kiislam, ukisema uiseme huyu arithi au asirithi haifatwi kauli yako inafatwa mwongozo wa shwria a mirathi.
Kama unapenda kumpa mtu mali yako, mpe ukiwa hai, huingiliwi na mtu. Siyo utunge sheria mpya mirathi.