Mjukuu anaweza kupata mirathi kutoka kwa wazee wake bila maandishi?

Mjukuu anaweza kupata mirathi kutoka kwa wazee wake bila maandishi?

Labda babu na bibi hawakuwa na watoto wengine wakuwarithi au siyo Waislam.
Marehemu Angekuwa hajazaa sawa ila maadam alizaa na ni marehemu basi mgawa wake wa mirathi atapewa huyo mtoto ambaye ni mjukuu wa hao wazee.
 
Marehemu Angekuwa hajazaa sawa ila maadam alizaa na ni marehemu basi mgawa wake wa mirathi atapewa huyo mtoto ambaye ni mjukuu wa hao wazee.
Kiislam labda iwe kabaki yeye mjukuu tu ndiyo mrithi, lakini mzazi akiwa na watoto wengine, wanarithi watoto zake hawarithi wajukuu zake.
 
Hakuna sababu katika Uislam itaizidi Qur'an. Labda uoneshe kwa ushahidi unaokubalika Kiislam kuwa marehemu hakuwa Muislam (aliritadi).
Ushahidi siyo lazima uwe "unakublika kiislam" bali unakubalika kimahakama na hakimu anaweza kuwa mkristo na kuamua kesi isikilizwe kimila au kiseriakli kutokana na ushahidi uliokuwepo
Hakuna wosia hapo.

Hayo ni maneno ya kila siku ya wazazi.

. Wacheni tamaa, wajukuu hamna chenu hapo.
Kama kuna mashahidi oral wassiyah unakubalika katika sheria za kiislam.
Pia kuna obligatory wasiyah, ambapo kidini ni wajibu kutenga si zaidi ya theluthi moja kwa maskini au ndugu wa mbali (inahusisha wajukuu pia) hata kama sio waislam.
Kuipa madeni pia ni moja ya obligatory wassiyah, yaani ni lazima kidini.
Kwa hiyo mirathi ya kiislamu haipo kirahisi kama mnavyotafsiri na ndiyo maana kunahitajika kadhi, tofauti na Tanzania Bara ambapo hata jaji mkristo anaweza kuamua mirathi ya kiislam.
 
Back
Top Bottom