PostGE2025 Mjumbe CCM, Buluba: Mimi nipo upande wa Tundu Lissu aachiwe huru, hili suala linatuchafua sana kama Taifa

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Buluba Mabelele, ametoa msimamo wake kuhusu sakata la mwanasiasa wa upinzani, Tundu Lissu, akieleza kuwa yuko upande wake na anatamani kuona anaachiwa huru ili arejee kwenye maisha ya kawaida ya uraiani.

Buluba amebainisha kuwa nchi inamhitaji Lissu, na iwapo kuna masuala ya kisheria yanayomkabili, basi ni vyema mahakama ikatoa uamuzi na hukumu stahiki ili kuondoa sintofahamu iliyopo sasa.

Aidha, Buluba amesisitiza kuwa msimamo wake huo haulengi kuingilia au kuifundisha mahakama jinsi ya kutekeleza majukumu yake ya kutoa haki. Hata hivyo, ameweka wazi kuwa kuendelea kuwepo kwa suala hilo bila utatuzi wa mwisho kunaathiri taswira ya nchi, akisema kuwa jambo hilo linaichafua sana Tanzania kama Taifa, hivyo kuna haja ya mamlaka husika kuliangazia upya ili lipatiwe ufumbuzi wa haraka.

Buluba Mabelele, MJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CCM TAIFA amesema; “Mimi Nipo Upande wa Tundu Lissu, aachiwe huru arudi uraiani haitufundishi mahakama kufanya kazi yake lakini hili suala la Lissu linachafua sana kama Taifa”

Ndio maanq bara la Afrika lipo nyuma. Wenye akili wanarudishwa nyuma ili wasiwafungue watu macho. Nirudie maneno ya professor Lumumba wa Kenya "Ina Afrika we elect fools to the office ".
 
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Buluba Mabelele, ametoa msimamo wake kuhusu sakata la mwanasiasa wa upinzani, Tundu Lissu, akieleza kuwa yuko upande wake na anatamani kuona anaachiwa huru ili arejee kwenye maisha ya kawaida ya uraiani.

Buluba amebainisha kuwa nchi inamhitaji Lissu, na iwapo kuna masuala ya kisheria yanayomkabili, basi ni vyema mahakama ikatoa uamuzi na hukumu stahiki ili kuondoa sintofahamu iliyopo sasa.

Aidha, Buluba amesisitiza kuwa msimamo wake huo haulengi kuingilia au kuifundisha mahakama jinsi ya kutekeleza majukumu yake ya kutoa haki. Hata hivyo, ameweka wazi kuwa kuendelea kuwepo kwa suala hilo bila utatuzi wa mwisho kunaathiri taswira ya nchi, akisema kuwa jambo hilo linaichafua sana Tanzania kama Taifa, hivyo kuna haja ya mamlaka husika kuliangazia upya ili lipatiwe ufumbuzi wa haraka.

Huyu jamaa awe makini
Bi mkola anaweza kuwa mbogo akimsikia.
 
Mjumbe Buluba, Lissu yuko magereza amepewa kesi inayopigwa danadana kwa zaidi ya mwaka sasa, tangu muda wote huo yuko magereza na anahudhuria kesi inayomkabili kulingana na maelekezo ya mahakama inayotegemea maelekezo kutoka juu.
Mjumbe Buluba mbona hukuwahi kujitokeza kumtetea Lissu na kuwa upande wake hadi leo yanapoimbwa maridhiano? :4Shrug:
 
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Buluba Mabelele, ametoa msimamo wake kuhusu sakata la mwanasiasa wa upinzani, Tundu Lissu, akieleza kuwa yuko upande wake na anatamani kuona anaachiwa huru ili arejee kwenye maisha ya kawaida ya uraiani.

Buluba amebainisha kuwa nchi inamhitaji Lissu, na iwapo kuna masuala ya kisheria yanayomkabili, basi ni vyema mahakama ikatoa uamuzi na hukumu stahiki ili kuondoa sintofahamu iliyopo sasa.

Aidha, Buluba amesisitiza kuwa msimamo wake huo haulengi kuingilia au kuifundisha mahakama jinsi ya kutekeleza majukumu yake ya kutoa haki. Hata hivyo, ameweka wazi kuwa kuendelea kuwepo kwa suala hilo bila utatuzi wa mwisho kunaathiri taswira ya nchi, akisema kuwa jambo hilo linaichafua sana Tanzania kama Taifa, hivyo kuna haja ya mamlaka husika kuliangazia upya ili lipatiwe ufumbuzi wa haraka.

Naunga mkono hoja!.

P
 
Kila kundi la waovu hawakosekani wachache katikati yao wanaokinai uovu na kusema sasa uovu basi na ndiyo anachokifanya huyu.
Sahihi kabisa..Baada ya Uchaguzi Mkuu-2015 nilibahatika kujumuika na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM-Taifa,tena Mwanamke kwenye Sherehe Moja kubwa ya Kijamii pale Morogoro Mjini.Katika kubarizi yaliingia mambo ya Siasa ambayo chanzo kilikuwa ni Siasa za Kenya,kipindi hicho Hayati Odinga amepinga Mahakamani ushindi wa Ruto.
Yule Mwanamama kwa Uchungu na uwazi aliongea wazi mbinu ovu na za hila zote ambazo CCM walizitumia kumtangaza Magufuli Mshindi wa kiti Cha Urais dhidi ya Marehemu Lowassa,watu tukashikwa na butwaa.Tangu hapo Mimi CCM niliwashusha kiwango Cha Zero kabisa.
Kumbe Laigwanani Edward Ngoyai Lowassa aliwapiga mwereka kabisa CCM kwenye Urais na inafahamika wazi ndani ya Mfumo wao.
 
Back
Top Bottom