TANZIA Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TPA, Renatus Mkinga afariki Dunia

Alikuwaga Mwanaharakati mzuri sana, namkumbuka kwa michango yake kwenye midahalo mbalimbali hasa ule wa Katiba Mpya. Pumzika kwa Amani baba.
 
Huyu dingi ilikuwa akipewa nafasi ya kuongea kwenye chombo cha habari au mdahalo, ni lazima ataropoka kuhusu issue ya Deep green, Meremeta au Richmond. Hata kama mada itakuwa ni mechi ya Simba na Yanga, mzee mkinga ataropoka hizo issue.
Videos
 
dah mzee namkumbuka akiongeaga hadi waandishi wa habari wanamkwepa anayvotema cheche za mate mdomoni
 
Kabla ya kuwa mjumbe wa bodi alikuwa mishen town
Kabla ya yote hayo alishafanya kazi NASACO baada ya hapo akawa mwanaharakati akipinga NASACO KUFA. ITV walikuwa wakimualika kwenye vipindi akawa anaelezea ni namna gani Serikali inaweza kuunda Kampuni ambayo itafanya kazi kama ilivyofanya NASACO. Kupitia vipindi katika ITV akielezea makosa ya Serikali kuivunja NASACO Mh. JPM akamteua kuwa mjumbe wa Bodi katika TASAC.Alikuwa ni mtu aliyejali sana matatizo ya watu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…