KikulachoChako
JF-Expert Member
- Jul 21, 2013
- 19,185
- 37,239
Wandugu tujitahidi kuzizuia jazba zetu......kukosana au kutokuelewana na mtu ni sehemu ya maumbile ya wanadamu.......tujitahidi kuzishika nafsi zetu.....pamoja na madhaifu na mapungufu lakini marehemu anabakia kuwa binadamu tu na mwanadamu mapungufu ni sehemu ya maumbile yake.....kumsengenya, kumtukana au kumdhihaki mtu aliyekufa inaonyesha ni jinsi gani tulivyo wafupi wa fikra na kusahau kuwa kifo ni njia ya kila mmoja wetu na kila mmoja ataondoka kwa wakati wake.......tuombeaneni mwisho mwema.....na mengine tumuachie Mungu maana yeye ndiye anamjua kiumbe wake....