Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Tamko alilolitoa Donald Trump akiwa na Benjamin Netanyahu akisema ataichukua Gaza na kuijenga upya kwa kuwaondosha wapalestina imepelekea mshtuko mkubwa kwa viongozi wa mataifa mengi pamoja na wanasiasa wa Marekani.
Wanasiasa waliokuwepo ukumbini wakati Trump akisema hayo kama hitimisho la mazungumzo yake na Netanyahu hapo majuzi baadhi yao walificha nyuso zao kwenye mikono kutokana na haya waliyoipata kwa tamko hilo la raisi wao.
Kuna wanasiasa nchini Ireland na mataifa mengine ambao wametoa matamko makali ya kumdharau Trump kwa matamshi yake hayo.Mmoja wao amesema ikulu ya Marekani kwa sasa ni kama haina mtu.
Kwa upande wake Al Green ambaye ni mjumbe wa Congress kutoka chama cha Democrat amesema atapeleka kwenye baraza vipengele vya kumshtaki Trump ili aachie madaraka (impeach)Akaongeza kwa kusema kuwa tamko kama hilo halingetajwa kama utani hasa kutamkwa na raisi wa taifa kubwa kama Marekani.
Mbali na hivyo hilo ni jambo kubwa kwa sera za nchi ambalo lingepaswa lipitie kwenye vikao rasmi vya kiserikali kabla ya kutamkwa hadharani kitu ambacho hakikufanyika.
Wanasias wengine wa Marekani wako waliosema matakwa ya Trump kuhusu Gaza hayatafanyika na hayatekelezeki.Wapalestina wenyewe wamemwita raisi huyo kuwa ni mwendawazimu.