Pre GE2025 Mjumbe wa INEC, Jaji wa Mahakama Kuu, Asina Omari: Wasimamizi wa maboresho ya Daftari la Kupiga Kura mfanye kazi kwa uadilifu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama Kuu, Asina Omari, amewataka watendaji wa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ngazi ya Halmashauri, katika Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli mkoani Tanga, kusoma maelekezo ya Tume kupitia vitabu vya maelekezo walivyopewa ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi huku wakizingatia sheria.

Asina amesema hayo Februari 23, 2025, alipotembelea na kukagua mafunzo kwa Watendaji hao ambayo yamefanyika katika Shule ya Sekondari Kwadoe.

Mafunzo hayo ni sehemu ya maandalizi ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, unaotarajiwa kuanza Machi 01, 2025 hadi Machi 07, 2025, katika mikoa ya Morogoro na Tanga katika Halmashauri za Wilaya ya Bumbuli, Handeni, Pangani na Mkinga.
Snapinst.app_480905887_1807179020082006_1491909755304779048_n_1080.jpg

Snapinst.app_480607166_1807179060082002_2162581544177508406_n_1080.jpg

Snapinst.app_480795066_1807179150081993_4421309572947240455_n_1080.jpg
 
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama Kuu, Asina Omari, amewataka watendaji wa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ngazi ya Halmashauri, katika Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli mkoani Tanga, kusoma maelekezo ya Tume kupitia vitabu vya maelekezo walivyopewa ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi huku wakizingatia sheria.

Asina amesema hayo Februari 23, 2025, alipotembelea na kukagua mafunzo kwa Watendaji hao ambayo yamefanyika katika Shule ya Sekondari Kwadoe.

Mafunzo hayo ni sehemu ya maandalizi ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, unaotarajiwa kuanza Machi 01, 2025 hadi Machi 07, 2025, katika mikoa ya Morogoro na Tanga katika Halmashauri za Wilaya ya Bumbuli, Handeni, Pangani na Mkinga.
Hizo ni Ghiriba za kiutawala tu, hakuna lolote jipya la maana hapa.

Uadilifu wa kweli kwenye suala hili ni lazima kabisa utaanzia na kufanya hatua muhimu za kubadilisha katiba ya Nchi pamoja na Sheria zingine zote kabisa zinazosimamia masuala haya ya Chaguzi za Siasa hapa Tanzania. Bila ya kufanya hivyo, basi itakuwa ni kazi bure, hakutakuwa na uadilifu wowote ule.
 
Back
Top Bottom