Hapa wanafunzi wanapofeli kuusingizia kuwa ni juu ya dini zao mimi napinga kwa nguvu moja! tena napinga kabisa, dhana hii ilikuwapo wakati wa marehemu Kighoma Ali Malima alipokuwa waziri wa elimu, na ili kuondoa dhana hii ukaletwa mfumo wa wanafunzi kuandika namba badala ya majina yao na walipendekeza mfumo huu ni waislam sasa iweje tena tunalalamika, na pia wasahishaji wa mitihani hii ni walimu wa shule zetu ina maana wao hawaoni haya na kusema! msiulaumu uislam, maana kati ya dini sinazosisitiza suala la elimu ni uislamu, Muhammad ( rehema za Mungu ziwe juu yake) kabla ya kupewa utume kitu cha kwanza aliambiwa "soma, soma kwa jina la mola wako" hakuambiwa achague elimu ya kusoma, ndio maana hata wakati wake alisisitiza" Itafuteni sana elimu hata kama ni uchina", so kosa sio uislam, kosa ni waislam wenyewe na hapa ni wale wachache wasiojali mbona kuna waislam wengi tu wamesoma na wanafanya vizuri mfano ni Prof. maghembe, Marehemu Haroub Othman, Prof Issa Shivji, Mwanaid Maajar na wengine tuache visingizio na kuutukanisha uislam!