CCM MKAMBARANI
JF-Expert Member
- Mar 15, 2017
- 2,031
- 1,514
Habari zenu wakuu wangu?.(Mh.Lowata Ole Sanale- Mkuu wa mkoa),Mh.Regina Chonjo-Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Katibu Mkuu wizara ya Maji Mh.Kitila Mkumbo na wote mnaohusika bila kuwasahau Wana-JF mtakaounga mkono uzi na andiko hili muhimu.
Bila shaka ni wazima wa Afya
Kuhusiana na kichwa cha habari sisi wananchi wa Kijiji cha Mkambarani katika mkoa wa Morogoro tumepigana katika ngazi zote,kuanzaia kata hadi wilaya,Mkoani hadi Wizarani lakini kutokana na mambo na majukumu mengi yanayowakabili viongozi wetu imekuwa ngumu kupata majawabu badala ya majibu ya maswali yetu kwao kuhusiana na kero ya maji na mradi wake kwa ujumla.
Historia ya Mradi .
Kabla ya mwaka 2004 Kijiji cha Mkambarani kilikuwa na tatizo kubwa sana la maji kama ilivyo kwa vijiji vingi katika bara letu la Afrika hususani nchini Tanzania.Mnamo mwaka 2004 aibu ya ubinadamu na utu iliwaingia watendaji kutoka serikali ya wilaya Morogoro-DC walifika katika kijiji na kukusanya maoni ya wananchi kuhusiana na kipi hitaji lao kuu ambapo maoni yalionesha kuwa wananchi wanahitaji maji zaidi kuliko huduma yoyote ile ya kijamii.
Baada ya muda kupita wataalamu hao kutoka serikalini walitoa mrejesho kwa wananchi kuwa ombi la kupewa huduma ya maji limeridhiwa na serikali ilitoa shilingi 300 ml. kwa ajili ya maji ya bomba na kutandazwa kwake.Katika hili wananchi walitakiwa kuchangia asilimia 5 na wilaya asilimia 5. Jasho la wananchi wenye uwezo wa kufanya kazi ilibidi wachangie shilingi 5000.
Mradi ulipangwa ukajengwa na kukamilika kwa vituo 12 vya utoaji huduma kwa wananchi,chini ya Mwenyekiti Mzee Kinyaku.Kwa wakati huo mradi haukujitosheleza ikabidi Diwani wa muda huo Mzee Shawa kufika ofisi ya waziri wa maji ambapo alifanikiwa kupata shilingi ml 565 kwa kumalizia mradi,jitihada zote hizo hazikwenda bure kwani ilipofika mwaka 2007 mradi ulianza kutoa maji jambo lililoleta faraja kwa wananchi masikini haswa akina Mama.Kama zilivyo kanuni za maendeleo ya jamii wananchi walishirikishwa katika upangaji bei wa maji ambapo ndoo moja ya lita 20 ikaamriwa iuzwe kwa tsh.20.
Kuanza Kwa Matatizo katika Mradi wa maji-Mkambarani
Wataalamu kutoka wilayani waliendelea kutimiza masharti ya kitaaluma ya maendeleo ya jamii (Community Development Principles) kwani kabla ya mapendekezo yao ya kuanzishwa na kuanza kazi kwa kamati ndogondogo za maji wlifika kijijini na kutoa elimu juu ya namna bora ya kuendesha mradi.Baada ya mradi kuundiwa kamati yake ya maji (Jumuiya ya watumia maji Mkambarani) ile kamati iliyokuwa ikiongoza mradi iliyoitwa kamati kamati ya maji na usafi wa mazingira ikakabidhi kwa chombo kipya.Wkati wa makabidhiano ya mradi Benki kulikuwa na shilingi ml.14 na laki 7.Baada ya mradi kuwekwa chini ya Bw.REUBEN CHABALIKO kulianza kuonekana dhahiri kuwa mbele ni kiza kutokana na kutokuwepo utaratibu wa uwazi hasa katika matumizi,jambo ambalo kimsingi ni kinyume na matakwa ya kisheria na ukaguzi wa hesabu za umma.Mikutano haikuitishwa hata mara moja kwa ajili ya kuuonesha umma maendeleo ya mradi wao.Wananchi wanyonge walichoka na kuanza kuhoji katika ngazi zote bila mafanikio.
Safari ya Dodoma kupigania Uhai wa Mradi.
Baada ya mambo kushindikana kote ilibidi wananchi kuchangishana kwa ajili ya kufika ofisi ya katibu mkuu wizara ya maji Dodoma ambapo K/Mkuu wizara ya maji alishughulikia suala hili na kuagiza kuwa wananchi wasikilizwe.Baadae aliekuwa mkuu wa mkoa Mh.Dk.Kebwe Stephen alifika kijijini kwa dhumuni la kusikiliza wananchi kuhusiana na kero ya mradi wa maji,uhujumu na ukiritimba ktk mradi wa maji.Baada ya mkuu wa mkoa kusikiliza malalamiko hayo ya wananchi aliamuru kusimamishwa kwa kamati ya Mhujumu Bw.Chabaliko,mbali na hiyo Mkuu wa mkoa aliagiza kufanyike ukaguzi na ripoti itolewe kuhusiana na mradi unavyoendeshwa kifedha.Ukaguzi ulifanyika ndani ya miezi iwilili.Ripoti ilionesha madudu yaliyojumuisha uuzwaji wa kiwanja cha mradi,matumizi mabaya pesa na ulipanaji posho bila maelezo ya msingi wakati mradi ukiendelea kudidimia.
Harufu ya uhujumu pesa
Hisia za dhulma ziliendelea kujidhihiri pale ambapo uongozi mpya ulipopewa dhamana ya kusimamia mradi chini y Mr.Goliama ulipoingiza kiasi cha shilingi ml75 kwa miezi mine huku ule wa Chabaliko ukiiniza shilingi ml 14 kwa miaka mitano……..
Maajabu ya Chabaliko na kuwa mwenyekiti wa kijiji
Ni Tanzania pekee ambayo mtu huweza kuiba sehemu moja na bado akapewa ridhaa ya kuwa kiongozi katika serikali,hii inajionesha kupitia muhujumu huyu Bw.Chabaliko kwani maajabu ni pale alipopewa dhamana ya kuongoza kijiji kama mweneykiti wa serikali ya kijiji.Baada ya kupata nafasi hiyo alianza kuitumia kama mpini wa kuwakata wenzie,kwanza alianza na na mafundi kuwaondoa kasha mwenyekiti mpya wa mradi Mr.Goliama kwa hujuma mbalimbali ikiwemo kukata maji kwa kificho kwa kutumia mafundi wake haikuishia hapo kwani hata mhasibu wa mradi alifukuzwaa bila sababu za msingi.
Uuzwaji wa mali za mradi (Kiwanja).
Hadi sasa
kimeuzwa kiwanja cha mradi wa maji ambapo imejengwa nyumba na watu wanaishi ambapo taarifa zimefika katika vyombo kama polisi na takukuru lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa.
SISI wananchi wa Mkambarani kwa sauti moja tunashangaa kwanini mtu kama Huyu aliyeshindwa kuiongoza Jumuiya ya watumia maji atawezaje kuiongoza serikali ya kijiji bila mizengwe,rushwa na dhulma kwa wananchi?.
Swali hili ni kwako Mh.Ole na mkuu wako wa Wilaya Bi Chonjo,nyote mnatakiwa kuwa chonjo kwani mkizembea jambo hili litawatafuna na kuwaharibia sifa yenu nzuri ya utendaji serikalini nyakati hizi tukielekea ktk uchaguzi mkuu.Tunaomba hatua stahiki na za kisheria zichukuliwe.
Mateso Kwa wananchi(Akina Mama); Madhira na hila zinasababisha kero kubwa kwa akina mama,wananchi wanapata dumu mbili kila baada ya siku mbili hali inayosababisha kusinyaa kwa uchumi wa mkoa huku mkoa wenyewe ukiwa hauna mbele wala nyuma.Mkuu wa mkoa anahujumiwa usiku na mchana.Amkeni Kumekucha.
MAMBARANI.
C.c. Rais.J.P.Magufuli, Kitila Mkumbo.,Juma Aweso,Dr.Bashiru Ali(K/Mkuu CCM).