A
Anonymous
Guest
Kero yangu ambayo pia naweza kusema ni kero yetu inahusu mamlaka ya Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA).
TARURA wameshindwa kusimamia Sheria ya Uzito wa Barabara na kumruhusu mkandarasi anayechimba mchanga katika Mto Tegeta kuharibu eneo kubwa la Barabara ya Mkupita katika Kata ya Goba pamoja na pacha wa barabara hiyo kupitia Uwanja wa Nyala kuelekea Mto tegeta wanakochimba mchanga huo.
Hali hiyo imesababisha kero kubwa kwa Watumiaji wa barabara hiyo na kukwamisha ufanisi.
Mara kadhaa sisi Watumiaji wa njia hizo tumekuwa tukupata wakati mgumu kupita ikiwemo kuchelewa kati mishe zetu kutokana na changamoto hiyo.
Picha zaidi: