Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Wakuu, weekend hii nimeingia Mbeya kwa ku-drive toka Dar, na nikashangaa sana kukuta maendeleo kidogo sana ya ujenzi wa hii barabara ya kwenda Tunduma hadi Zambia toka nitembelee hapa miezi minne iliyopita. Nimeuliza wenyeji kwa nini kasi ya ujenzi wa barabara hii uko chini kiasi hiki? Nimeambiwa wakandarasi wa barabara wamesusa baada ya kuwa hawalipwi na serikali.
Sasa Mbeya ni jimbo la Spika wa Bunge Tulia, na huko nyuma tuliambiwa miradi ya maendeleo Mbeya haifanyiki kama adhabu kwa watu wa Mbeya kwa kumchagua mtu wa upinzani kama mbunge wao, Sugu. Sasa kulikoni tena Mbeya mambo hayaendi na mbunge wao ndio huyo Spika wa Bunge Tulia?
Au labda sasa serikali imewasusa tena kwa sababu ya Mwabukusi wa TLS?